Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwanini asikuteue wewe au dada yako ???Nikusalimu kwa jina la jamhuri....ikumbukwe huyu mama (Janeth) alikuwa bado ni mtumishi wa umma hivyo akachukua likizo bila malipo...ni muda sasa amrudishe ale nae mema ya nchi
Kwanini asikuteue wewe au dada yako ???
[/QUOTE
acha ubinafsi bwana mdogo...kuna shida gani ukitetea maslahi ya wengine?
Dooh..Nikusalimu kwa jina la Jamhuri....ikumbukwe huyu mama (Janeth) alikuwa bado ni Mtumishi wa Umma hivyo akachukua likizo bila malipo...
Ni muda sasa umrudishe katika utumishi wa Umma amalizie muda wake wa kustaafu
😂😂Kwanini asikuteue wewe au dada yako ???
"KUJIKOMBA"Bado tunasafari ndefu sana kama TAIFA katika kupiga hatua. Inabidi tuondokane na watu wa kujikomba kwenye system na tuondokane na maprofesa waliogushi elimu.
kwamba hiyo nafasi inatolewa kama shukurani? hongo au kujipendekeza?Nikusalimu kwa jina la Jamhuri....ikumbukwe huyu mama (Janeth) alikuwa bado ni Mtumishi wa Umma hivyo akachukua likizo bila malipo...
Ni muda sasa umrudishe katika utumishi wa Umma amalizie muda wake wa kustaafu
Hiyo familia haijikwezi kwa fadhila hizo na naamini hauwezi kukubali mambo ya siasa tena. Hata watoto wake usitarajie wakajiingiza hukoHongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.
Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo:
Kwanza, usiturudishe nyuma tena. Awamu ya tano imetuonyesha nini maana ya uhuru na kujitegemea. Tanzania haina mjomba wala shangazi huko nje. Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe. Jukumu lako ni kutupanga, kutuvuvia, kutushawishi na kutuonyesha kwa mfano wako wewe mwenyewe kwamba inawezekana, tunaweza, tusonge mbele.
Pili, Mzee Magufuli kafa, lakini spirit yake haijafa. Ni askari aliyefia vitani akiwa mstari wa mbele, katika kupambania uhuru wetu na kujitegemea kwetu. Usije kufanya kosa kufanya mapungufu ya style ya Magufuli ya uongozi iwe kigezo cha wewe kubadili uelekeo wa nchi yetu, katika kujiamini na kuthubutu. Magufuli kafa lakini kaacha alama na kaacha spirit. Wenye hiyo spirit wamo ndani ya chama tawala, vyama vya upinzani, serikalini, sekta binafsi, na kwa wakulima na wafanyakazi. Hili ni jeshi kubwa sana usicheze nalo.
Tatu, tutakusikiliza kwa umakini, tutakuangalia sana mienendo yako, tutatizama sana namna zako kama zinaturudisha nyuma au zinatupeleka mbele. Nisiseme sana katika hili lakini itoshe tu kwamba spirit ya Mzee Magufuli haijafa. Tukiona tu dalili kwamba unakotupeleka siko hatutakuvumilia. Tushaonjeshwa uhuru hatutarudi tena kwenye utumwa. Tushaonjeshwa kujitegemea hatutarudi kwenye utegemezi tena.
Mwisho, Mungu akupe hekima ya kuongoza watu milioni 60, kwa akili na ujasiri. Ninaamini utatuvusha salama, karama ya uongozi unayo, itendee haki. Tegemea ushirikano wetu.
Pia soma: Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli