bado teuzi zake haziakisi kujenga umoja na mshikamano wa taifa letu,
teuzi zinaegemea sana upande mmoja, hakuna uwiano jambo linaloweza kuleta mpasuku siku za mbeleni.
kinacho takiwa ni kuweka uwiano, huwezi kufanikiwa kujenga nchi yenye umoja na mshikamano kwa kujaza zaidi kundi la watu wa aina moja na kuwaacha wengine wengi nje.
kama kweli unataka kujenga uzalendo wa kweli ni lazima kuweka mseto wenye uwiano sawia. sio upendeleo.
unaweza kufanya utafiti ktk idara mbali mbali za serikali na utaona uwiano unao lalamikiwa, ambao kimsingi unapaswa uzingatiwe kwa lengo la kuimarisha umoja wetu na utulivu.
mamlaka zinazo husika na uteuzi na kuteua lazima waliangalie hili bila kuoneana aibu, jambo hili limekuwa likilalamikiwa mara kwa mara hivyo sio sahihi kulipuuzia au kujifanya halionekani.
tunahitaji nchi yetu iwe imara zaidi kuliko watu kulalamika na kuto aminiana.