Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Umepita mwaka mmoja sasa tangu marehemu Rais Magufuli alipoishutumu maabara ya taifa kwa kutoa majibu ya vipimo vya sampuli za mapapai, kware na mbuzi kuwa positive, kwa maana kwamba vitu hivyo vilionekana kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona. Tukio hili liliidhalilisha sana nchi yetu na lilisababisha nchi yetu kuonekana kuwa ni kituko cha dunia kwasababu njia hii haikuwa njia sahihi ya kuhakiki ubora wa vipimo vinavyofanywa na maabara hiyo. Cha kusikitisha zaidi ni kuwa rais Magufuli alifanya hivyo baada ya kupokea ushauri kutoka kwa aliyekuwa katibu mkuu wa wizara ya Afya, Prof. Mabula Mchembe.

Haijulikani sababu hasa zilizomfanya Prof. Mchembe kutoa ushauri ule, lakini, athari za ushauri ule zilikuwa ni kubwa kuliko ambavyo watanzania wengi wanafahamu. Watumishi wapatao 12 wa maabara hiyo hatimaye waliachishwa kazi kinyemela. Prof. Mchembe akishirikiana na mkurugenzi wa idara ya kinga, Dr. Leonard Subi na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu, Deodata Makani, wamewaondoa wafanyakazi 12 kutoka katika maabara hiyo na kuleta wafanyakazi wengine. Hata hivyo njia iliyotumika kuwapata watumishi wapya ilionekana kuwa na hila na upendeleo.

Prof. Mchembe na wenzake walitumia fursa hiyo kuwaingiza jamaa zao katika ajira ya mradi kuchukua nafasi ya watumishi walioondolewa bila kufuata taratibu halali. Inasemekana ameleta jamaa zake wawili, mtu na mkewe, walioletwa kutoka Simiyu na kuingizwa katika ajira hizo.

Watumishi wengi wa maabara hiyo, ikiwa ni pamoja na aliyekuwa mkurugenzi wa maabara, Dr. Nyambura Moremi, walikuwa wakifanya kazi kwa mkataba kupitia mradi wa Laboratory Support Program unaofadhiliwa na PEPFAR kupitia CDC. Kwa kawaida watumishi hawa husaini mikataba yao ya mwaka mmoja kila ifikapo Oktoba kulingana na mwaka wa fedha wa Marekani ambao ndio wafadhili.

Mwaka jana Oktoba 2020 wafanyakazi hao walipewa mikataba ya mwaka mmoja kama kawaida (Oktoba 2020 mpaka Septemba 2021) lakini zoezi la kuwapatia mikataba watumishi hao lilisitishwa na mikataba kurudishwa kwa maelekezo ya Mkurugenzi wa Utwala na Rasilimali watu, Deodata Makani. Kilichofuata, watumishi hao waliamriwa kuwasilisha nyaraka mbalimbali ikiwemo barua ya maombi ya kazi, CV, barua ya ajira, barua ya kukubali mkataba, barua ya kupangiwa kituo cha kazi, cheti cha kuzaliwa, vyeti vya elimu na barua ya kuomba kuhuisha mikataba.

Jambo la kushangaza ni kwamba nyaraka hizi zilikuwemo katika mafaili ya watumishi hao hapo wizarani tangu walipoajiriwa. Baada ya kuwasilisha nyaraka hizo, watumishi hao walipewa mikataba ya miezi mitano (5) tu kuanzia Oktoba 2020 mpaka Februari 2021 badala ya mkataba wa mwaka mzima kama ilivyo kawaida ya miaka yote. Hii ilimaanisha kwamba mikataba ya mwaka mmoja waliyosainishwa awali mwezi Oktoba 2020 ilifutwa kinyemela.

Mwezi Januari, 2020 watumishi hao walipewa barua iliyoandikwa tarehe 22 Desemba 2020 ikiwa imesainiwa na katibu mkuu Prof. Mabula D. Mchembe. Barua hiyo ilinukuliwa kusema:-

Kwa barua hii ninakutaarifu kuwa mara tu mkataba wako utakapokoma Wizara ya Afya haitakuongeza muda mwingine mpaka hapo taratibu za kiutumishi zitakapotolewa

Ilipofika tarehe 13 Februari 2021, Deodata Makani aliitisha kikao na kuongea na watumishi wa mradi wa maabara. Watumishi walitaka kujua hatima yao baada ya tarehe 28 Februari 2021 (ambayo ndio ilikuwa tarehe ya mwisho ya mkataba wa miezi mitano). Katika kikao hicho, Deodata Makani aliwaambia watumishi kwamba nafasi za kazi za watumishi wa mradi wa maabara hazitotangazwa na kwamba watumishi hao wangeitwa kwenye usaili.

Ilipofika tarehe 17 Februari watumishi hao walipigiwa simu kuitwa kwenye usaili tarehe 18, 19 na 20 Februari. Siku ya usaili, mbali na watumishi wa mradi wa maabara, kulijitokeza watu wengine ambao haijulikani walitoka wapi au walipataje taarifa za usaili ule. Kabla ya kuanza usaili, Deodata Makani aliongea na watu wote waliofika kuhudhuria usaili. Baadhi ya watu hao walioonekana kuwa ni wageni kwa wafanyakazi wa maabara, waliuliza wameitiwa nini hapo, na wengine waliuliza ni nafasi gani za kazi walizoitiwa. Hii ilionesha dhahiri kwamba hawakuwa na taarifa kamili za kinachoendelea hapo jambo ambalo linaleta shaka juu ya njia iliyotumika kuwapata.

Baada ya zoezi la usaili, matokeo ya usaili huo hayakutolewa. Hata hivyo kwasababu wafanyakazi walikuwa wameshapewa barua zinazowajulisha kwamba baada ya tarehe 28 Februari mikataba yao haitaongezwa mpaka hapo taratibu za kiutumishi zitakapotolewa, walijua kwamba huo ndio mwisho wa ajira yao. Wengi hawakuchukua hatua yoyote kutafuta haki yao kwakuwa walikuwa wamekatishwa tamaa na utawala usioheshimu sharia na haki za binadamu chini ya utawala wa rais Magufuli. Baadae ilikuja kufahamika kwamba kuna watumishi wapya wamepelekwa katika maabara ya Taifa kuchukua nafasi za watumishi 12 wa maabara walionyimwa mikataba.

Watumishi walionyang’nywa ajira zao hawakuwahi kukutwa na makosa yoyote ya kinidhamu wala ya kiutendaji, wala hawakuwahi kupewa hata barua ya onyo. Haijulikani ni sababu gani zilizopelekea kuachishwa kwao kazi.

Jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa miongoni mwa watumishi waliokatishiwa mikataba, wapo wataalam wenye uzoefu wa zaidi ya miaka mitano na waliopatiwa mafunzo mengi yanayoendana na kazi zao ikiwa ni pamoja na mafunzo yaliyoiwezesha maabara ya taifa kupata ithibati ya kimataifa (ISO accreditation). Mmoja wa waliokatishiwa mikataba alikuwa ni Biomedical Engineer aliyepata mafunzo ya kufanya Biosafety Cabinets Certification. Wataalam kama huyu wapo wachache sana hapa nchini. Inawezekana hawafiki hata watano. Mtaalam huyo alikuwa katika mchakato wa kuanzisha mafunzo ya namna hiyo hapa nchini kwa kupitia chuo cha MUHAS.

Wengine walioondolewa ni wataalam wa maabara wa fani tofautitofauti ikiwa ni pamoja na laboratory scientists, technologists, technicians, maafisa TEHAMA na madereva.

Mojawapo ya mapendekezo yaliyotolewa na tume iliyoundwa na rais Samia Suluhu Hassan kuishauri serikali kuhusu namna ya kushughulikia COVID-19 ilikuwa ni “serikali ikamilishe malipo ya madeni ya watoa huduma na watumishi waliokuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19”. Sambamba na pendekezo hilo, ingekuwa ni vyema na haki suala la watumishi walioporwa ajira zao liangaliwe pia na waliohusika na dhulma hii kuwajibishwa.
Wacha Mungu aitwe Mungi, tulikokuwa tunaelekea Mungu ndiye anaejuwa.
 
mama naomba uangalie wizara ya ardhi, hii wizara ni ngumu mno, ofisi za ardhi zina uozo mkubwa mama.

Kagua kuanzia ofisi za ardhi ngazi ya wilaya yaani hapa ndo kuna balaa la uozo, tunateseka.

Rushwa rushwa yaani ni balaa

Nchi hii kubwa sana, Tumuombee Mama Yetu.
 
JK was far way better president kuliko marais wengi sio Tz tu bali Afrika nzima.
Nitaomba kukupinga hapa mkuu.

Kumbukua ni awamu iliyomwaga pesa mtaani kama awamu ya pili! Ikawafanya ninyi wenye access ya upigaji na mbeleko mtembee juu ya ardhi, watu wakaua kabisa sekta ya kilimo kwa ike KILIMO KWANZA ambayo ilizalisha mapapaa wale, TASAF ikazalisha mapapaa fulani. Tumeshuhudia tambo za hao mapapaa wakimwaga manoti hadharani, TRA na Polisi wakiangalia, kodi ikikusanywa kwa wafanyakazi wanyonge tu, n.k

Hakika haya ndio yalikuwa maendeleo ya mtu na si watu kama mlivyosema chini ya raisi aliyetukanwa kila kona.

Ukimpa mtu pesa mtaani, atajenga St Mary's schools, watasoma watoto wa wenye uwezo, wale wanaopiga na kulindwa, 80% watasoma kayumba, ukiboresha vitu na mifumo, tutarudi kwenye kile kipindi cha kuona shule za serikali ni bora na fahari kubwa mtoto akisoma huko. Ni awamu gani haya mambo yalikufa?
 
Wakuu Salaam,

Jana Mh. Rais Samia Suluhu Hassan, wakati akizindua kiwanda cha ushonaji cha Polisi kuna kauli alizitoa ambazo binafsi naona hakupaswa kuzitoa hasa kwa kuzingatia kuwa yeye ndiye mtu mwenye nguvu na mamlaka na dhamana kubwa kabisa kwa sasa ndani ya JMT.

Jambo la kwanza alionyesha kushangazwa na vitendo vya matapeli wa kwenye mitandao ya simu ilhali sote tumesajiliwa kwa alama za vidole, jambo hili ni kweli linatushangaza wengi inakuaje hawakamatwi na kushughulikiwa kirahisi na bado wanaendelea, lakini yeye kwa nafasi na mamla aliyonayo alitakiwa kusimama kwenye zamu na nafasi yake kwanza kwa kuonyesha kutoridhishwa na kufutahishwa na jinsi watendaji wanavyoshughulikia swala hilo na pili atoe maelekezo ya nini anataka kuona kinafanyika tena haraka, lakini si kusema tu kuwa na yeye anashangaa, swali linabaki kuwa uongozi wake juu ya jambo hili ni upi?

Jambo la pili ni kuhusu kesi za kubambikiza, ameonyesha kuridhishwa na TAKUKURU kufuta kesi nyingi ambazo wameona hazikua sahihi, halafu akawaambia Polisi wajitafakari. Kama kiongozi liko tatizo ameliona ilikua jambo zuri angeonyesha alichokiona kisha atoe maelekezo ya utekelezaji, mfano ili kupunguza msongamano wa wafungwa JPM hakumwambia DPP ajitafakari bali alimwagiza aende magerezani aonane na mahabusi ili aone kesi za kufuta lakini pia azungumze na watu walio tayari kulipa fedha waachiwe. Hadi akafikia hatua ya kusema hayo ina maana yako mambo ambayo yeye ameyaona ambayo inawezekana watendaji wa maeneo husika either hawajayaona au wanayaona ni ya kawaida, sasa kiongozi kama mbeba maono jukumu lake ni kuwaonyesha yale anayoyaona na kuwaelekeza wayafanye.

Kama mimi kila siku ninapotoka nyumbani kwangu napita mlangoni kwa kupiga sarakasi, ukiniona ukashangaa kuwa nafanya kitu cha ajabu halafu ukaniambia nijitafakari wakati mimi naona ni kitu cha kawaida, usitegemee kuona mabadiliko.

Mama usishangae, kama sisi wananchi tusio na mamlaka, wewe ndiye kiongozi wetu uliye mbele yetu, toa maelekezo, kemea, amrisha mambo yaende.
Taifa zima limekuwa la kushangaa kuanzia mwananchi wa kawaida hadi mkuu wa nchi, sijui tunaelekea wapi...!!!
 
Wenzetu wa kutoka visiwani ndio hulka yao ni watu wenye busara wasiotaka papara! Nakumbuka hata Mwalimu Nyerere aliwahi kumsihi Alhaji Mzee Mwinyi kuwa alikuwa mpole sana hivyo alimshauri AONGEZE UKALI KIDOGO!!!

Mpeni muda mama Samia mtaona mambo mazuri! Anapowapa muda Viongozi kujitafakari maana yake ni kwamba ameona dosari mahari na hivyo anawapa muda wahusika kujirekebisha kabla ya yeye kuchukua hatua . Huo ni muda unaompa yeye nafasi ya kuchunguza na kupata ukweli wa jambo husika badala ya kukurupuka na kutoa uamuzi kama mlivyozoeleshwa!
Kuna watu hufanya mambo kimya kimya, lakini matokeo huwa ndiyo yanazungumza kwa sauti kubwa.

Bado hatujui kama Rais Samia Suluhu Hassan ni kiongozi wa aina hii.

Ngoja, wakati ndio mwamuzi sahihi. Matokeo yataonekana au hayataonekana.

Kama hayataonekana, atakuwa ni rais wa maneno matamu tu basi!
 
Being a leader, an individual needs to be creative on various issues concerning with national development in different angles, and then if it comes to a time a national leader is wandering to various state on going manners it is a stressing state to the national correspondent citizen(s). This implies that she is not creative for any thing in fact she is only waiting for abroad states aids and not to look for solutions on different state matters.

The death of Hon. Magufuli is a threat to our nation, since he used his position effectively to solve different social matters to some instances though he had his own weaknesses as all other human beings we are too.

We have been sold under a lowest price in fact. Tunahitaji kujitathmin kama taifa.

# 666 sir 100
 
Habari wanabodi..!
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu .Jana kwenye mkutano wa viongozi wa CCM na waandishi wa habari moja ya swali lililoulizwa na mwandishi wa habari ni kwamba,je kama CCM wapo pamoja?

Kiukweli ni swali ambalo unaweza ukaona la kizushi lakini mwenye kuuliza swali sio mjinga ,inawezekana kuna kitu amekiona ndani ya Chama cha Mapinduzi hakipo sawa.

Ila bila shaka Mh Daniel Chongolo alilijibu kama ilivyotakiwa kujibu kwamba tupo sawa kabisa .

Ila kwa maoni yangu binafsi naona kama ndani ya CCM kumeibuka waumini wa imani au nadharia mbili kuna wale waliokuwa wanaamini nadharia ya Hayati JPM na kuna wale walio amua kubadilika na kukubaliana na nadharia mpya ya uongozi ya mheshimiwa Samia Hassani.

Hawa wanaoshikiria nadharia ya JPM ndio wale waliogoma kumzika JPM katika mioyo yao,hivyo basi mwenyekiti wa chama,Shaka,Chongolo wanatakiwa wajipe assignment ya kuhakikisha kwamba wanaishi katika kivuli na maono ya JPM kwa sana kuendeleza yale yalio mazuri ili wale ambao hawaja mzika hayati JPM kwenye mioyo yao waendelee kuona kama bado JPM yupo madarakani mpaka pale atakapozikwa.Maana hawa ambao bado hawajamzika JPM mioyoni mwao ndio wale wanaoamini JPM bado ni rais wa JMT.

Sijuhia naeleweka hapa kweli,kam haujaelewa bora tu utulie maana uta mix madesa?
 
Habari wanabodi..!
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu .Jana kwenye mkutano wa viongozi wa CCM na waandishi wa habari moja ya swali lililoulizwa na mwandishi wa habari ni kwamba,je kama CCM wapo pamoja?

Kiukweli ni swali ambalo unaweza ukaona la kizushi lakini mwenye kuuliza swali sio mjinga ,inawezekana kuna kitu amekiona ndani ya Chama cha Mapinduzi hakipo sawa.

Ila bila shaka Mh Daniel Chongolo alilijibu kama ilivyotakiwa kujibu kwamba tupo sawa kabisa .

Ila kwa maoni yangu binafsi naona kama ndani ya CCM kumeibuka waumini wa imani au nadharia mbili kuna wale waliokuwa wanaamini nadharia ya Hayati JPM na kuna wale walio kubaliana na nadharia mpya ya uongozi ya mheshimiwa Samia Hassani.

Hawa wanaoshikiria nadharia ya JPM ndio wale waliogoma kumzika JPM katika mioyo yao,hivyo basi mwenyekiti wa chama,Shaka,Chongolo wanatakiwa wajipe assignment ya kuhakikisha kwamba wanaishi katika kivuli na maono ya JPM kwa sana kuendeleza yale yalio mazuri ili wale ambao hawaja mzika hayati JPM kwenye mioyo yao waendelee kuona kama bado JPM yupo madarakani mpaka pale atakapozikwa.Maana hawa ambao bado hawajamzika JPM mioyoni mwao ndio wale wanaoamini JPM bado ni rais wa JMT.

Sijuhia naeleweka hapa kweli,kam haujaelewa bora tu utulie maana uta mix madesa?
Itachukua muda sana mama kumfuta JPM mioyoni mwa watu
 
Back
Top Bottom