Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.

Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo:

Kwanza, usiturudishe nyuma tena. Awamu ya tano imetuonyesha nini maana ya uhuru na kujitegemea. Tanzania haina mjomba wala shangazi huko nje. Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe. Jukumu lako ni kutupanga, kutuvuvia, kutushawishi na kutuonyesha kwa mfano wako wewe mwenyewe kwamba inawezekana, tunaweza, tusonge mbele.

Pili, Mzee Magufuli amefariki, lakini spirit yake inaishi. Ni askari aliyefia vitani akiwa mstari wa mbele, katika kupambania uhuru wetu na kujitegemea kwetu. Usije kufanya kosa kufanya mapungufu ya style ya Magufuli ya uongozi, iwe kigezo cha wewe kubadili uelekeo wa nchi yetu katika kujiamini na kuthubutu. Magufuli amefariki lakini kaacha alama na kaacha spirit. Wenye hiyo spirit wamo ndani ya chama tawala, vyama vya upinzani, serikalini, sekta binafsi, kwa wakulima na wafanyakazi. Hili ni jeshi kubwa sana, usicheze nalo.

Tatu, tutakusikiliza kwa umakini, tutakuangalia sana mienendo yako, tutatizama sana namna zako kama zinaturudisha nyuma au zinatupeleka mbele. Nisiseme sana katika hili, lakini itoshe tu kwamba spirit ya Mzee Magufuli inaishi. Tukiona tu dalili kwamba unakotupeleka siko hatutakuvumilia. Tushaonjeshwa uhuru hatutarudi tena kwenye utumwa. Tushaonjeshwa kujitegemea hatutarudi kwenye utegemezi tena.

Mwisho, Mungu akupe hekima ya kuongoza watu milioni 60 kwa akili na ujasiri. Ninaamini utatuvusha salama, karama ya uongozi unayo, itendee haki. Tegemea ushirikano wetu.

Pia soma: Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
expand...
Wandugu ambia huyo mtawala mwanamke, amuogope "MUNGU" kwani si-niyeye kwa kinywa chake? Alitamka ya kwamba atafanya mabadiliko makubwa ht yakimgharimu ki-siasa? Sasa anapambana na nani tena? Ashasahau yeye ndo alitamka?!!!! KITI alichokalia kina DAMU, uovu ni mwingi mno kwa hicho KITI... vilio juu ya hicho KITI ni-vikubwa mno vimefika hadi Mbinguni, ndo maana kila anayekalia hicho KITI mwanzoni huanza vizuri sn, lkn baada ya muda roho za uovu ndani ya hicho KITI huanza tena kutenda kazi.... swali rahisi, ni-nani kakashifu/kachambua dini ya mtu mwingine? ukweli hayupo, TEC wametoa waraka wao wamemaliza wako kimya, hizo ni sababu tu za kuhalalisha jambo fulani, sasa nasema MUNGU HADHIHAKIWI anaujua ukweli wote, nasema, bado kuna mambo MUNGU anataka kuyatenda juu ya hii Nchi, mwenye masikio na asikie..............
 
C.AG yeye kazi yake ni kuandika tu walio fanya ubadhilifu na ushauri wake uwa ni kuwa wasichukuliwe hatua wapewe nafasi ya kudhibitisha kile walichoshutumiwa.

TiSS tuseme wameshindwa je nani wa kumsaidia rais dhidi ya wezi hao anbao anawataja kila uchao anapolalamA?
 
C.AG yeye kazi yake ni kuandika tu walio fanya ubadhilifu na ushauri wake uwa ni kuwa wasichukuliwe hatua wapewe nafasi ya kudhibitisha kile walichoshutumiwa.

TiSS tuseme wameshindwa je nani wa kumsaidia rais dhidi ya wezi hao anbao anawataja kila uchao anapolalamA?
Anayemwangusha Samia ni Samia mwenyewe hakuna mtu mwingine wa kulaumiwa.

Aliyekufa ni Magufuli watendaji wamebaki ni walewale kwa nini wamshinde?
 
Naona wanatumia nguvu kubwa sana kumpamba hizo nguvu wanayotumia si bora wangeielekeza kwenye maendeleo tu!

Mtu mwenyewe hana mvuto amepwaya nguvu ya malori ndio inatumika huko Lindi.

Kwa maajabu gani aliyonayo? Hatuna mtu pale. Uwezo wake wa kuongoza ni mdogo sana na vyeti vyake vya kuunga unga.

Ogopa sana mtu asietamani kusikia kero za watu wake kwa masikio yake mwenyewe. Ogopa sana mtu anaeamua kuwa kimya pale anapokosea ili msahau madhambi yake.

Tuna katiba la hovyo sana.
 
Naona wanatumia nguvu kubwa sana kumpamba hizo nguvu wanayotumia si bora wangeielekeza kwenye maendeleo tu

Mtu mwenyewe hana mvuto amepwaya nguvu ya malori ndo inatumika huko Lindi

Kwa maajab gani aliyonayo? Hatuna mtu pale

Uwezo wake wa kuongoza ni mdogo sana na vyeti vyake vya kuunga unga

Tuna likatiba la hovyo sana

Kapicha kidogo
 
Back
Top Bottom