Habari wadau wa JF ,
Kwanza nikiri wazi kwamba sijakuchagua kabisa kabisa kuwa Rais wa JMT ,Kura yangu ilienda kwa Lowassa,Lengo la kumchagua Lowassa lilitokana na sera zake za kufanya maamuzi magumu na kuleta mabadiliko yatakayomkomboa mwananchi.Nlikuwa siamini kabisa kwamba atatokea mtu ndani ya ccm kuleta mabadiliko aliyotaka kuyaleta Lowassa.
Mh. Rais kwa mwendo huu ulioanza nao ni Mzuri na nimepata taarifa kwamba katika hizi siku zako 21 za mchakamchaka umekusanya/save fedha nyingi sana.Nadhani umetambua kwamba serikali ikikusanya kodi ipasavyo yaani zile zinazokwepa na misamaha zinaweza kusomesha wanafunzi bure ,kulipa mishahara mizuri wafanyakazi wote wa serikali na kutekeleza miradi/Ahadi za serikali.
Mh kwa Niaba ya wafanyakazi na watanzania kwa ujumla tunaomba ufute kabisa hizi service charge tunazomlipa ndugu rugemalila na Singh seti abinder maana ni wizi wa mchana kweupe,Haiwezekani unikate kila mwezi 6700 hata nisipotumia umeme,mbona makampuni ya simu yaliyoinvest gharama kubwa kuliko tanesco hawakati service charge unaponunua vocha? ukinunua vocha ya buku unapata buku Kama ilivyo kwanini tanesco watukate Hiyo 6700 ambayo inaenda kwa Singh na ruge? Futa Kabisa Huo wizi.
Swala Jingine ni hili la P.A.Y.E,Kiukweli Mh Rais hili swala la Paye linatuumiza sana sisi wafanyakazi,natambua ni muhimu kuchangia kodi lakini tunavyokatwa Hiyo paye sio kabisa,kwanini mfanyabiashara Huyo kodi yake inaktwa kwenye Faida lakini mfanyakazi kodi inakatwa kabla ya kutoa makato yake? Mfanyabiashara kwanza anatoa kodi ya pango,nauli ,msingi ,hela ya cha Kula,nauli iliyobaki ndio percentage flani inakatwa kodi tofauti na mfanyakazi ambaye analimwa kodi kabla. Hizo Paye mnazopunguza kwa mwaka kwa 1% tunapata nyongeza ya 2000 tu kwenye mishahara ambapo hatuoni hata umuhimu wake,tunaomba magufuli mbadilishe formula ya kodi ambayo ndio itakayompa nafuhu mtu na si hiki kiini macho cha kusema unashusha 1% halafu inayoongezeka ni sh 2000,badilisheni formula naumia nikianglia slip navyoona nalimwa kodi karibia laki 6 wakati Nina madeni kibao ambayo net inakuja kuwa laki 4,tupunguzieni kodi angalau kwa nusu Kama mtu alikuwa anakatwa laki nne kodi akatwe laki 2 Hiyo mbili iende kwenye net hapo maisha yatakuwa Bora.Inawezekana kwa sababu umeziba mianya yote ya kupoteza pesa za serikali ,umefuta matumizi ya anasa ya serikali ,umefuta safari za nje etc.
Nawasilisha.