Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
mi nashauri usiwaweke nchemba, kawambwa, membe, January, nyalandu kwenye baraza lako
 
[Nianze kwa kukupongeza kwa uzalendo unaouonesha kwa kututumikia Watanzania bila woga wowote.


Enzi za mwalimu wanafunzi Wa UDSM waliwahi fanya mgomo na kuharibu mali. Mwalimu akawatia ndani. Kisha akawaeleza kuwa "The objectives you had are genuine but the methods you used to achieve those objectives were improper". Kwa nini hamkunitaarifu matatizo yenu kabla ya kugoma? Matatizo yenu ni sahihi kabisa ila njia mliyoitumia siyo sahihi.

Kuna rafiki yangu alinipigia simu jana usiku na kuniuliza "mbona waislamu Tu!? Mkurugenzi Wa muhimbili alieondolewa muislamu. Leo tena Wa TRA muislamu. Kulikoni!?". Nilimjibu kuwa Nina imani na magufuli. Ni coincidence tu lakini halengi waislamu.

Nikirejelea kauli ya mwalimu nyerere kwa wanachuo, muh magufuli upo sahihi kabisa lakini tafadhali fuata ushauri wangu ufuatao;


Endelea na oparesheni tumbua majibu. Amini kuwa sisi watanzania tupo nyuma yako. Ninachokuomba, unapoamua wizara au shirika lipi litumbuliwe, angalia dini ya mhusika. Changanya uwajibishaji kwa mujibu Wa dini. Leo muislamu kesho mkristu kwa sababu waliokosea ni mchanganyiko Wa dini mbalimbali. Ikitokea kigogo mwengine atakaeguswa ni muislamu, kazi yako iliyotukuka itaingiwa nchanga. Waislamu wataanza kulalamika.


Uongozi unahitaji kucheza na akili za watu. Kumbuka kuwa imani INA nguvu sana.

Usimbakishe fisadi yeyote serikalini. Fagia wote ila cheza karata zako vizuri kwa kufanya mkasi utue kwenye dini zote kwa sababu nina hakika wanaokosea si Wa dini moja Tu. Marejeo (reference) ya escrow, maliasili Nk... Ni kielelezo kuwa dini siyo kigezo cha ufisadi.



TANBIHI
Nimesukumwa na uzalendo kuandika makala hii na siyo udini!]


Mkuu hapa hamna hoja ya msingi! Tunaoengelea masilahi ya taifa kwa upana wake...These are mere coincidencies tu!
Kwani hao Waislam wameufanyia nini Uislam usonge mbele zaidi ya kujinufaisha wao na familia zao tu tena kwa kufanya maisha ya Watanzania/waislamu wengine kuwa magumu? Huyo wa TRA amewahi hata kujenga chumba kimoja cha Madrassa? Hata Mwenyezimungu kwenye Uislam hakusema kwamba kama Muislam anakiuka maadili asiadhibiwe....Mimi namuunga Mh. raisi mkono....
 
ACT na CCM NI ndugu moja!

Inawezekana ACT na CCM kuwa ni kitu kimoja....ila huyu mama na CCM ni vitu viwili tofauti. Huyu mama yuko consious sana, nadhani ni mwanasiasa bora wa mwaka huu, kama umemfuatilia sera na mazungumzo yake mbalimbali hauwezi kwenda kinyume na hili
 
Naanza na wachache;

1. Shubashi Patel

2. Salum Mpuchu

3. RA

4. R1

5. Home Shopping Centre

6. GMS

Ongeza unao wajua

Kina Peter,Paulo hawakwepagi kodi?

GNLD,Forever Living Products hawa ndiyo wanaongoza kwa kukwepa kodi kufanya biashara mkononi na kuingiza bidhaa kwa njia za panya
 
Mkuu hapa hamna hoja ya msingi! Tunaoengelea masilahi ya taifa kwa upana wake...These are mere coincidencies tu!
Kwani hao Waislam wameufanyia nini Uislam usonge mbele zaidi ya kujinufaisha wao na familia zao tu tena kwa kufanya maisha ya Watanzania/waislamu wengine kuwa magumu?

Huyo wa TRA amewahi hata kujenga chumba kimoja cha Madrassa? Hata Mwenyezimungu kwenye Uislam hakusema kwamba kama Muislam anakiuka maadili asiadhibiwe....Mimi namuunga Mh. raisi mkono....
 
Kwa mara ya kwanza kabisa!! Faiza foxy leo tuko timu moja! Huyu mama ni potential sana kwa taifa letu. Tukiacha maoni na dira aliyonayo ibaki kichwani mwake kwaajiri ya itikadi ya uvyama, tutakuwa tumejidhulumu sisi na vizazi vijavyo.

Laiti kama watanzania wangetulia na kumsikiliza, na kumuelewa kipindi cha kampeni leo hii tungekuwa tunaongea story nyingine kabisa
 
Huyu bwana maghembe asipewe uwazir jimbo peke yake limemshinda ...kumpa uwazir nikutaka Wana Mwanga waendelee kuwa maskin hohehahe....

tuombe mungu jina lake limtoke mheshimiwa asimkumbuke kabisaa
 
tuombe mungu jina lake limtoke mheshimiwa asimkumbuke kabisaa

Ila hili jimbo linatia huruma ...wananchi wake kwa mkoa wa kilimanjaro ndo maskin....sana ...maendeleo yana legalega sana.....vijana wanakimbia ...hapafi kuishi .....mbunge yuko busy kujisifia kuwa yeye ni profesa.....barabara ya sehem kama kilomen sasa ni ndoto haifikiki...kabisa.......inatia huruma sana .....
 
Habari wadau wa JF ,

Kwanza nikiri wazi kwamba sijakuchagua kabisa kabisa kuwa Rais wa JMT ,Kura yangu ilienda kwa Lowassa,Lengo la kumchagua Lowassa lilitokana na sera zake za kufanya maamuzi magumu na kuleta mabadiliko yatakayomkomboa mwananchi.Nlikuwa siamini kabisa kwamba atatokea mtu ndani ya ccm kuleta mabadiliko aliyotaka kuyaleta Lowassa.

Mh. Rais kwa mwendo huu ulioanza nao ni Mzuri na nimepata taarifa kwamba katika hizi siku zako 21 za mchakamchaka umekusanya/save fedha nyingi sana.Nadhani umetambua kwamba serikali ikikusanya kodi ipasavyo yaani zile zinazokwepa na misamaha zinaweza kusomesha wanafunzi bure ,kulipa mishahara mizuri wafanyakazi wote wa serikali na kutekeleza miradi/Ahadi za serikali.

Mh kwa Niaba ya wafanyakazi na watanzania kwa ujumla tunaomba ufute kabisa hizi service charge tunazomlipa ndugu rugemalila na Singh seti abinder maana ni wizi wa mchana kweupe,Haiwezekani unikate kila mwezi 6700 hata nisipotumia umeme,mbona makampuni ya simu yaliyoinvest gharama kubwa kuliko tanesco hawakati service charge unaponunua vocha? ukinunua vocha ya buku unapata buku Kama ilivyo kwanini tanesco watukate Hiyo 6700 ambayo inaenda kwa Singh na ruge? Futa Kabisa Huo wizi.

Swala Jingine ni hili la P.A.Y.E,Kiukweli Mh Rais hili swala la Paye linatuumiza sana sisi wafanyakazi,natambua ni muhimu kuchangia kodi lakini tunavyokatwa Hiyo paye sio kabisa,kwanini mfanyabiashara Huyo kodi yake inaktwa kwenye Faida lakini mfanyakazi kodi inakatwa kabla ya kutoa makato yake? Mfanyabiashara kwanza anatoa kodi ya pango,nauli ,msingi ,hela ya cha Kula,nauli iliyobaki ndio percentage flani inakatwa kodi tofauti na mfanyakazi ambaye analimwa kodi kabla. Hizo Paye mnazopunguza kwa mwaka kwa 1% tunapata nyongeza ya 2000 tu kwenye mishahara ambapo hatuoni hata umuhimu wake,tunaomba magufuli mbadilishe formula ya kodi ambayo ndio itakayompa nafuhu mtu na si hiki kiini macho cha kusema unashusha 1% halafu inayoongezeka ni sh 2000,badilisheni formula naumia nikianglia slip navyoona nalimwa kodi karibia laki 6 wakati Nina madeni kibao ambayo net inakuja kuwa laki 4,tupunguzieni kodi angalau kwa nusu Kama mtu alikuwa anakatwa laki nne kodi akatwe laki 2 Hiyo mbili iende kwenye net hapo maisha yatakuwa Bora.Inawezekana kwa sababu umeziba mianya yote ya kupoteza pesa za serikali ,umefuta matumizi ya anasa ya serikali ,umefuta safari za nje etc.

Nawasilisha.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom