Mh. Rais, usisahau kwenda kutumbua jipu NIDA, UHAMIAJI, na POLISI, haya ndio maeneo mengine ambayo yamekithiri kwa rushwa. Ukianza na NIDA pale ni pachafu, mabilioni ya fedha yameibiwa, viongozi wa NIDA wamenunua na kujenga Mahekalu yasiyosemekana.
Ukienda uhamiaji huku nako ni kuchafu sana, Wachina wanaingia na kufanya kazi bila vibali, rushwa imekithiri sana. Nikukumbushe tu zile nafasi mia 200 za kazi zilizotangazwa mwaka jana zilivyojaa rushwa, undugu na urafiki, nafikiri pa kuanzia unapo.
Kuhusu Polisi naomba Watanzania mseme.