Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Kuna ukame ktk hazina ya dola... Serikali haina Money !! Ndo wanafanya uvamizi huu...badala ya kuomba kwa hiyari!!!!
MAHANJU huoni sherehe zimefutwa.....


Hivi mkuu mnataka mabadiliko yapi maana ueleweki kabisa...achane asafishe nchi kinachokuumiza kwamba anasafisha uchafu wa vasco da gama
 
Last edited by a moderator:
Mh. Rais, usisahau kwenda kutumbua jipu NIDA, UHAMIAJI, na POLISI, haya ndio maeneo mengine ambayo yamekithiri kwa rushwa. Ukianza na NIDA pale ni pachafu, mabilioni ya fedha yameibiwa, viongozi wa NIDA wamenunua na kujenga Mahekalu yasiyosemekana.

Ukienda uhamiaji huku nako ni kuchafu sana, Wachina wanaingia na kufanya kazi bila vibali, rushwa imekithiri sana. Nikukumbushe tu zile nafasi mia 200 za kazi zilizotangazwa mwaka jana zilivyojaa rushwa, undugu na urafiki, nafikiri pa kuanzia unapo.

Kuhusu Polisi naomba Watanzania mseme.
 
Mh rais Uhamiaji ,polisi na tra walioko Mipaka yote ya nchi yetu sio Wazalendo bali ni mitandao ya Wakubwa wahizo Idara nandio Maana Wamejaa viburi? huko Namanga kuna Mfanyabiashara Wa Arusha anaitwa Kalanga huyu ni Mungu mtu hakuna Wakumuhoji?

Mungu akupe Afya njema Rais wangu Ili Utumbue Majipu yote? na Uweze kufanikiwa Adhima yako yakuleta Mabadiriko yakweli Kwa Watanzania Maana gape la Walionacho na Wasionacho linazidi Kujenga Chuki Kwa Wananchi na Serikali yao?
 
umenikumbusha nafasi 200 za UHAMIAJI. mkuu afanye fasta nna hasira nao wale, na wafilisiwe kabisa
 
Nimuombe waziri mkuu hebu nenda uhamiaji kuhusu viza za wafanyakazi wageni hasa hii viza ya cta.hawa wafanyakazi wageni huwa hawatoki nchini badala yake ujanja tu unafanyika na maofisa wa uhamiaji ktk mipaka yetu naomba ushtukize na hasa viwandani matransporter sana sana migodini na viza hii ipigwe stop wawe na work permits kazi nyingi za watanzania wamehodhi hawa wageni kisa muwekezaji
 
Nida ni hatari sana, nashauri waende kule ili yatumbuliwe. Watu wamekaa pale wanatafuna pesa tu, yaani ni hatari.
 
Mi naona kama ni hivyo, atembelee kila idara na kila kijiji!! Nchi yote imeoza mpaka balozi wa nyumba kumi anahongwa kama si pesa, basi kuku!!! Nimeenda Ardhi kwa kipindi cha miaka mitatu kubadili jina la umiliki wa kiwanja changu, hadi leo file halijaonekana. Kesho narudi.

Naomba kaka Magu awepo pale anisaidie.
 
Jamani tumechoka na huu udhalimu wa mitandao tafadhali Mheshimiwa JPM fanya yako TTCL irudi tuwakimbie akina Voda, airtel, zantel, tigo, smart na halotel.
 
Airport hapo mtu na four yake anafanya kazi Uhamiaji Ila una mkuta ana Gari tano ndani ya miaka Mitatu. wakati mwalimu na Degree yake ndani ya miaka miwili hata kununuwa Bajaji hawezi
 
Hivi kuna haja ya yeye kutembelea kila idara,
wakuu wa idara wenyewe wajichunguze, kama mtu anaona nafasi hiyo haiwezi aende kwa mh pombe amwambie mkuu mimi kasi yako siiwezi naomba nitoke kabla hujaniondoa kwa aibu
akitembelea akikuta uozo isiwe kumfukuza kazi ila kifungo tu maana atakuwa ametumia pesa ya sirikali kwa matakwa yake kwani tulishamuomba atoke akakataa.
 
Polisi,uhamiaji na hao akinani sijui wote hao ni cha Mtoto kwa rushwa,Magufuli akitaka kumaliza rushwa apambane na wanasiasa ndio wanaongoza kwa kutoa na kupokea rushwa,hasa wanasiasa wa CCM ambao wamepambwa na rushwa mpaka kwenye nyayo za miguuni hadi kucha zao zinatoa harufu ya rushwa.
 
NIDA nadhani kwa sasa ni bora akaifuta kabisa! Ili kuokoa pesa! Toka wawaandikishe watu miaka mitatu iliyopita mpaka leo dhani hata 10% ya ID hawajawakabidhi wahusika!. Nadhani ilikuwa mradi wa ulaji tu na kupeana kazi!
 
Kuna harufu ya majungu na fitna...cha msingi tufanyekazi sio kila mtumishi wa umma ni mwizi
 
Tunakuomba sana mheshimiwa rais ukifika Arusha usisahau kupitia viwanda hivi vinavyomilikiwa na wawekekezaji wa Kihindi, kuna baadhi ya haki za wafanyakazi hazifuatwi na wamiliki wa viwanda hivi, ikiwepo muda wa kazi na malipo ya mshahara haueleweki wananchi wanaofanya kazi kwenye kiwanda hiki wengi wananyonywa na kupoteza haki zao, please usiache kufika mheshimiwa Rais MAGUFULI.
 
Miaka mitano ni mingi.... Mwachen aende taratibu ili asiharibu... Maana kama nyumba ya kum kutoka nyumban kwako imebomolewa na kimbunga... We utaaka hapo kufanya nin! Watajitoa wenyewe siku znavozd kwenda
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom