Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Sehemu kubwa ya mapato hayaelekezwi kwenye kuleta maendeleo kama elimu, afya na sehemu muhimu kwa jamii. Badala yake individual budgets zipo kwenye michango kama ya Kitchen parties, Send off, Harusi, Mazishi na michango ya kanisani isiyokuwa na feedback wala haiongezi maadili yoyote zaidi ya kujenga hofu ya muda tu, baadae maovu yana zidi kushamiri kila kukicha. Michango hii hudumisha sio tu umasikini, bali ufukara.

Kwenye mipango ya mazishi kuna gharama nyingi sana mfano sanda, sanduku, kuutreat mwili, kuuhifadhi mortuary, usafiri.... yanini yoote hayo. Mwili hauna thamani, ni vema ukachomwa na umeme na sio kuni. Majivu ya wekwe kwenye mkebe, kwa kufanya hivyo: kaburi moja tu linaweza likajengwa vema na kuweka mikebe zaidi ya 100 na juu kukawa na kibao cha watu wa ukoo waliozikwa kwenye hilo kabuli moja la watu 100. Kuusafirisha majivu kwenye mikebe ni rahisi kuliko jeneza. Miti itapona na sehemu ya kuzikia zitatutosha.

Mwili hauna thamani bali roho ndio yenye thamani. Mwili hufa lakini roho haifi. Kazi kwenu kuchambua hili. Naomba msinitukane mie.

Lingine, tembelea vituo mbali mbali vya afya uone maajabu, sijui ni baraka au???? watu wanajifungua watoto kwa wingi sana. Wakati hali ya kuwatunza na kujitunza hamuna kabisa. Hii pia inaleta sio tu umasikini, bali ufukara.

Tumuunge mkono Mh. Rais wetu kupunguza matatizo yetu haya ya ufukara.

Kama namekosea kwa kusema hayo munisamehe mie.
 
Mkuu, mianya ikizibwa vilivyo, wale watoaji wa million moja kwenye arusi ili wapate sifa watapotea automatically.
 
Tupunguze pia michango ya makanisani na misikitini kubana matumizi.
 
Tena leo nina kikao cha kitchen part niwahi tuu! Nifanye tuu haraka! Niwahi tuu c bora michango hiyo ya kitchen party, sendoff, arusi huwa tunaona inakoelekea na kutushibisha zetu our stomach kuliko hii mara sijui kodi PAYEE inawapeperusha watu angani na kufanyia mambo yaooo
 
Tupunguze pia michango ya makanisani na misikitini kubana matumizi.
Hilo halijakaa sawa, kwa kuwa hata maandishi kwenye vitabu vitakatifu vya dini imeeandikwa kuwa mpeni Kaisari vilivyo vya Kaisari na mpeni Mungu vilivyo vya Mungu.
 
Who is magufuli?Ndo wa wapi?Umeandika sijui manini?Ondoa upuuzi.
 
Mkuu ulishaoa/kuolewa nini?
Mkuu nimeshaoa, ila lengo kuu la mada hii ni kuchangia maendeleo kuanzia individuals, families na Taifa kwa ujumla. Kuwa na budget ya mishahara yetu inaweza kutufanya tuishi maisha mazuri.

Kwenye ufukara mfano mdogo, kwa wakati huu mtu akiambiwa kuwa umekaribia kustaafu, anachanganyikiwa na kuanza kupanga mipango isiyotekelezeka kama ufugaji wa kuku, bustani za mbogamboga, kuuza ubuyu n.k. Wengi hatujipangi, tunategemea kusaidiwa tu. Tunaweza kuanza sasa kujipanga na tufanikiwa.
 
Mawazo halisi na mtambuka. Mfano harusi iliyogharimu milioniu 15 kwa mtu asiye hata na nyumba zikiwekezwa vizuri zinaweza kumsaidia kujenga familia imara mbeleni badala ya kuzimaliza usiku mmoja tena kuanzia saa 2 jioni mpaka 5.30 usiku!
Kuna umuhimu wa kuzaa ili kupata nguvu kazi lakini angalizo hapa ukiwa na idadi kubwa ya raia wajinga ni tatizo zaidi.
 
Unapoongelea uzembe na ufisadi uliotokea kila wizara, uwezi kumuweka pembeni Katibu mkuu kiongozi Ombeni Sifue. Kwa mujibu wa Cheo cha katibu mkuu kiongozi, yeye ndie anaesimamia makatibu wa wizara zote. Ufisadi na uzembe wote uliotokea ni chini ya Ombeni Sifue. Ni jambo la ajabu sana kulaumu kwanini vifaa tiba vya Muhimbili havifanyi kazi bila kumgusa Ombeni Sifue, maana yeye pia ni msimamizi wa wizara ya Afya pia. Wakati wa Kikwete Sifue alitetea vizuri ufisadi wa Escrow, alikuwa msitari wa mbele kutetea ufisadi. Kwa sasa anajaribu kujionesha kwa Watanzania as if ana utu, juzi kwa mara ya kwanza amekwenda kukagua utengenezaji wa MRI Muhimbili, alikuwa wapi ziliposimama kufanya kazi miezi miwili?. Mtu huyu ni mnafiki mkubwa, Magufuli Muondoe, fisadi pacha wake tayari kaondoka kwa mujibu wa katiba, bado huyu
 

You have writen very well, huyu atamharibia ni jipu hilo litumbuliwe ASAP

Kwa ulichokiandika umemtendea haki huyo kwenye Avatar yako
 
Kuna Malofa sijui huwa wanalewa uji wa ulezi. Balozi Ombeni Sefue ndio alikuwa anafanya shughuli zote za serikali wakati mawaziri walipokuwa kwenye kampeni,Mizengo Pinda alikuwa ana recover na shock ya kukatwa. I think Balozi Sefue ni mojawapo ya watendaji wazuri kabisa katika serikali ya Jk na hii serikali mpya ya Magufuli.
 
Bunge si mali ya Rais,hapaswi hata kwa sekunde moja kuliingilia. Ule ni Mhimili Huru, kama ilivyo Executive na Judiciary. Bunge ndilo lenye wajibu wa kuisimamia Serikali,ila si Serikali kulisimamia Bunge! Jukumu ulilompa unamwonea tu.

Kwa muda na wakati tofauti kila muhimili huwa unapata wakati wa kusimamia muhimili mwingine kwa namna fulani.Bunge linaweza kumwondoa Rais na Rais anaweza kulingilia na kulivunja Bunge.Hii inaitwa check and balances!!.Rais anachagua Majaji na kuwaapisha japo hawezi kumfukuza moja kwa moja.
 
Natanguliza shukrani kwa uteuzi wako na mungu akupe maisha marefu na yenye afya.Tunaamini maendeleo ya nchi yanaanzia katika halmashauri za wilaya na ndiko ambako fedha na miradi mingi ya maendeleo iko huko. ila kimsingi watekelezaji na watendaji wake wamekuwa ni miungu wadogo hivyo ufanyaji wa kazi unakuwa dhaifu. Na katika awamu iliyopita tumeshuhudia uanzishwaji wa halmashauri nyingi mpya .lakini utendaji wa hizi halmashauri mpya ni dhaifu sana.Tunaomba serikali yako makini iliangalie hili na hasa zile halmashauri za mikoa ya pembezoni. Hasa Taratibu za Tender na maendeleo yako. Asante.
 
Huu ni mtazamo wangu. Napendekeza hawa mawaziri wasiwepo awepo waziri mkuu tu ambaye atakuwa anawakilisha shughuli za serikali bungeni. Mimi naona mawaziri wako kisiasa zaidi, maana raisi wetu anajaribu kupunguza matumizi ni bora kusiwepo na baraza la mawaziri ili tusonge mbele.

Ni maoni yangu tu.
 
Kwa ubora wa rais tulienae nakubaliana na wewe kabisa kwa asilimia kubwa tu. Hivi vichwa viwili vinatosha kabisa kuendesha nchi hii, yani rais na PM wake tu.

Ila kwa kuwa rais kaapa kuilinda katiba ya nchi, lazima afanye uteuzi wa mawaziri na manaibu kama katiba inavyo elekeza.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…