Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Mheshimiwa Raisi JPM,
Kwanza nikupongeze kwa kazi nzuri uliyoanza kuonyesha kwa siku hizi chache baada ya kuapishwa, watanzania wengi tumefurahishwa sana na jinsi unavyoitekeleza kauli mbiu yako ya ''Hapa Kazi tuu''
Mheshimiwa Raisi, Wizara ya ardhi ni miongoni mwa wizara zenye kero nyingi sana hapa nchini.
Kama ilivyo maeneo mengine Tanzania, Sisi wakazi wa Kibamba Dar Es Salaam, kwa muda mrefu sasa tangu 2010 tulipopimiwa maeneo yetu katika kata ya kibamba na tukalipia kwa ajili ya kupatiwa hati, hadi leo hatujapata hati zetu, kila tukifuatilia hatupewi majibu ya maana.Najua kibamba ni mfano mdogo sana wa kero nyingine nyingi za ardhi katika nchi hii, lakini tunaomba kwa kauli mbiu yako ya Hapa Kazi tuu, utusaidie ili watanzania tuweze kumilikishwa ardhi kwa ajili ya maendeleo yetu na taifa kwa ujumla.

Naomba kuwakilisha
 
Walimu wenzio ambao umetuacha huku katika fani hali mbaya.
Mshahara wa mwalimu siku hizi haumalizi mwezi.
Mwalimu hawezi fanya jambo lolote la maendeleo mpaka akope. Huwezi amini hata kununua sofa za sebureni mwalimi lazima akope
Mh. Kwa sasa walimu ni walala hoi kuliko watumishi wote wa serikali
Hawana hata posho moja zaidi ya mshahara wao
Najua unayajua matatizo ya walimu pengine kuliko mimi ninayeandika ujumbe huu kwa kuwa nasikia eti ulishawahi kuwa mwalimu.
Fanya jambo na roho za walimu zitapoa,
Waongezee mshahara japo kidogo walimu
Wapewe posho kama maaskari polisi
Waheshimiwe wanapotoa maoni yao kuhusu mustakabali wa elimu kwani kwa sasa madiwani ndiyo walioshikilia elimu yetu huku halmashaurini.
UKINIALIKA NITAKUELEZA MENGI SANA YA ELIMU YETU MKUU.
 
Pamoja na hayo nasikia pia katika kubadikishiwa muundo mwalimu akitoka kusoma hapandi cheo hadi akae miaka mitatu, sijui nayeye alipokua mwalimu alilikuta na kuliacha Hili?
 
Pamoja na hayo nasikia pia katika kubadikishiwa muundo mwalimu akitoka kusoma hapandi cheo hadi akae miaka mitatu, sijui nayeye alipokua mwalimu alilikuta na kuliacha Hili?

Ndiyo maana nikasema huku hali ni mbaya
 
Magufuli anayajua matatizo na shida za watanzania. Wewe tulia tu huyu mheshimiwa huwa anaibuka kama kakakuona.
 
Mkuu ofisi za halmashauri ya Bagamoyo kuna miungu watu. Kuna watu wana jeuri ya kumjibu mtu chochote kinachomjia mdomoni.
Mganga mkuu wa wilaya anakataa wauguzi wenye vyeti wanaotaka kujitolea vijijini ambako hakuna wauguzi wala huduma za afya bure bila ya sababu za msingi.
Walimu wa 2011 hawajawahi pandishwa daraja kwa mwaka wa tano wa fedha ingawa sheria ya mahusiano kazini inamtaka mwajiriwa mpya kukaa miaka minne kabla ya kupanda daraja.
Watendaji katibu wote wanaishi Dar es salaam hivyo kutumia muda mwingi kusafiri. Kuna ratiba ya huduma kuna siku unaweza kwenda unaambiwa "mhusika wa jambo hili leo siyo siku yake ya kuja kazini njoo alhamisi"
Kifupi hiyo ndiyo Bagamoyo fanya uje pia tunajenga BANDARI pale Njueni na kuna kivuko kutoka Dar es salaam fanya ukitembelee.
 
Rais wangu Dr. John, pombe Joseph Magufuri, muziki wako unaelekea kukolea naona gita la rizimu limetulia ongeza gita la solo ili muziki ukolee vizuri, tunaomba ubadirishe wafanyakazi kwenye BWAWA la pesa pale WIZARA YA FEDHA na idara zake ukianza na TRA NA HAZINA. Hili ndilo gitaa linalotengeneza muziki, pia kata safisha mitambo chakavu yote ya kurekodia kwani muziki haufiki vizuri kwa walengwa, kuna studio ndogo ndogo hapo kati kati nazo zinaongonzwa na baadhi ya watendaji wakubwa tena wengine ni wakubwa km mibuyu kuyakata unahitaji cheso mpya. mfano kuna mIbuyu pale TRA, BANDARI, DAWASCO, TANESCO, USALAMA WA TAIFA, POLISI NA NK.

Unaota ndoto za mchana wewe. Huyo magufuli wako anawezaje kukata tawi LA mti alilolikalia,BOT, hazina wamejaa watoto na ndugu wa mabosi wake kwenye chama, waliomuweka hapo, adhubutu awaguse tuone kama atamaliza miezi 6 tu,
 
Itakuwa jambo jema sana kama atafanya hivyo, kwa sababu pale pamegubikwa na rushwa ndogondogo kwa wauguzi, kadhalika huduma mbovu nadhani kuliko hospitali zoote za mkoa wa Dar es salaam. Nadhani kwa hapo atafukuza wengii
 
Ushauri wangu kwa Rais,

1. Fufua TAZARA haraka iwezekanavyo ili kunusuru barabara zetu
2. Anzisha mfumo wa bandari kavu -moja Kibaha(Soga au Ruvu), na nyingine kubwa tu Morogoro-magari makubwa mengi yataishia Morogoro na Kibaha-hayataingia jijini. Pia mfumo wetu wa reli zote 2 ya kati na Tazara utatumika vizuri kwa short hauls.
3.Panua wigo wa Bima ya Afya ili iweze kucover kada nyingi zaidi-wafanyabiashara wadogo wazalendo wenye anuani, wakulima, wavuvi, wafanyakazi katika sekta binafsi -na kila Mtanzania ambaye anaweza kuchangia. Jinsi ilivyo hivi sasa Bima ya Afya ni discriminative na inafanya kazi chini ya kiwango.
4. Tunisha mfuko wa Mikopo ya Elimu ya JUU ili vijana wengi wanufaike-wengi waliosoma kwa mkopo huo wameajiriwa lakini bado hawajaanza kurejesha -japo kidogo kidogo. Vile vile anzisha kodi ya elimu ya juu kwa waajiriwa wote waliosomeshwa na serikali bure. Tupo wengi na wengi wetu ni senior, middle or high level managers-wengine wabunge. Pia imarisha usimamizi wa utoaji mikopo -sehemu kubwa inakwenda kwa wasiostahili.
5. Rekebisha utumishi polisi-kuna maskari polisi hasa trafiki na CID wamekaa kituo kimoja kwa zaidi ya miaka 10. Utendaji wao umeshuka sana sana na jeshi la polisi wanaliona biashara yao binafsi .
6. Tengeneza Southern Economic zone around Mtwara na Lindi ili ukanda huo uweze kushindana na kanda zingine na kukuza uchumi. There is every thing that in necessary in that zone for sustained growth-hivi sasa ni sleeping giant.

Haya kwa sasa yanatosha. Nitarudi tena.
 
By: Visionary Leader Zitto Zuber Kabwe.

"Thomas Sankara once said ?You cannot carry out fundamental change without a certain amount of madness? (Uwendawazimu).

1. weka mikataba yote ya Rasilimali za Nchi wazi - PSAs and MDAs.

2. Futa posho za makalio katika mfumo mzima wa Serikali kama Mpango wa Maendeleo unavyotaka.

3. Futa business class air tickets Kwa watendaji wa Serikali na wanasiasa isipokuwa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu.

4. Futa matumizi ya mashangingi ( BoT wameonyesha mfano kwenye hili).

5. Futa uagizaji wa sukari kutoka Nje na anzisha miradi ya miwa tuuze sukari Nje.

6. Weka wazi taarifa ya Serikali kuhusu utoroshaji wa fedha na fungua mashtaka Kwa wahusika mara moja.

7. Wape takukuru mamlaka ya kukamata na kushtaki na kila mwenye Mali athibitishe yeye kaipataje (reverse burden of proof).

8. Mali na Madeni ya Viongozi yawe wazi Kwa umma na wananchi waruhusiwe kuhoji.

9. Ruhusu mshindi wa uchaguzi Zanzibar atangazwe na ufanye naye kazi.

10. Acha mchakato wa Katiba Kwa kuanzia alipoishia Warioba, achana na Katiba Pendekezwa".
 
Muhimbili was a sample...surely it reflect the general population of the hospitals in Tz......

No need
 
Unaota ndoto za mchana wewe. Huyo magufuli wako anawezaje kukata tawi LA mti alilolikalia,BOT, hazina wamejaa watoto na ndugu wa mabosi wake kwenye chama, waliomuweka hapo, adhubutu awaguse tuone kama atamaliza miezi 6 tu,

umenena
 
Zitto ana madini kichwani yanayoendelea kupanda thamani.....
 
Yaani hospital za government zimejaa rushwa na mataputapu yote. Kuna siku nimeenda hospital kupima bp. Eti nesi hajui bp kubwa inaanzia ngapi.
 
Huyu jamaa anamiakili mingi, anajua kujenga hoja na kuitetea ila wabunge wetu wengi wanajua siasa ni kujua kuongea tu, hawatambui kuwa kuna muda wa kuumiza ndonga.
 
hapo mimi naunga mkono hoja mbili tu,
1. kuweka mikataba yote wazi
2. aliyeshida Zanzibar atangazwe hata kama kuna wizi umefanyika maana kule waliiba zote wakaacha za rais wa muungano
 
mbona kaandika mambo ya kawaida sana lakini misifa kibao isiyokuwa na maana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom