Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Mheshimiwa rais Magufuli naomba uanze na chama cha walimu (CWT). Chama hiki kifutiwe usajili kwa kuwa hakinufaishi walimu bali ni kwa manufaa yao. Vitega uchumi vya CWT vibinafsishwe.

HERI WALIMU TUKOSE CHAMA KULIKO KUWA NA CWT!
 
atawagusaje wakati ilisadikika ccm walipewa 35 bilion? kazi tu hapa hakuna, akiinua pua atadaiwa ata malimbikizo yote
 
Cwt ni mdudu anayekula pesa ya walimu bila faida yeyote.cwt wanajifanya wema kumbe wanadidimiza walimu.Futa kabisa huyu mdudu.
 
mbona mnataka kutia aibu,magufuli aanze na wapi aache wapi.mwishowe mtataka aingilie mambo ya ndoa zenu
 
Vyama vyote vinavyotetea maslahi ya watumishi wa umma vifutwe. Kama CWT, TALIGWA na TUGHE vinazidi kutupunguzia mishahara yetu watumishi wa umma na ukiangalia hawana kazi yoyote .
 
Hatua kwa hatua kilio chenu kitasikilizwa.

Mpeni muda Jembe letu, kwa kweli bado ana mambo mengi sana kuyafanyia kazi
 
Hongera Mh Rais lkn swala la kupona mashine hizi kwa haraka kuliko ilivyotarajiwa tunaomba iwe chachu ya wewe kuzifuatilia sasa zile mashine za mitaani zilizokus nzima wakati wote uweze kuwabaini wamiliki wake ni nani,ikiwa zitakuwapo zinazomilikiwa na ma daktsri wa kutoka serikalini ni bora mwanzo kuzitaifisha then kesi ifuate sababu kwa miezi hiyo 2 kuna roho za watu zimepotea pengine kwa uzembe tu.mwisho endelea kuvamia taasisi nyeti na hata mashirika ya umma kujionea uozo watu hawafanyi kazi!
 
Katika Sekta ya Maji namshauri Mhe. Rais aunde TANWATER na kuunda MAJI FUND kama ilivyo kwenye Sekta ya Miundombinu ambapo kuna TANROADS na ROAD FUND. Wabunge wengi katika bunge lililopita walipiga kelele juu ya umuhimu wa serikali kuanzisha vyombo hivi muhimu ili kuongeza kasi ya serikali katika kutatua kero ya maji kwa wananchi. TANWATEE ikiundwa, hakutakuwa na haja ya kuwa na wakurugenzi wengi kwenye ngazi ya Wizara ya Maji na ateuliwe Mtendaji Mkuu mahiri wa TANWATER mwenye rekodi nzuri ya utendaji na uadirifu. Mtendaji Mkuu huyo apewe uhuru wa kuunda Timu mahiri inayofanana na yeye. Nina imani kubwa sana kuwa ndani ya miaka 5 ya Tanzania ya Magufuli, wananchi wengi sana kama si wote watapata huduma ya uhakika ya maji.
 
Ninaposema siasa ni mchezo mchafu na wanasiasa ni wajuzi wa kuteka akili za watu huku wakifukia mambo muhimu mnasema naponda na siupendi utendaji viongozi hasa huyu mh Pombe!

Sasa nawauliza hivi karibuni tu wote tumepata taarifa kuwa Mh JK amekomba hazina yote, lkn pia kama watanzania tunahaki ya kuzijua mali za waheshimiwa wetu Mkapa na Jk ambao wameliongoza taifa letu,

Je Mh Pombe atatusaidia kuwahoji walivyozipata ili tujue kweli yeye ni kiongozi wetu na hayuko kulinda masilahi ya watu flani?
 
Badala yake utayaona yanahangaika na chadema tu mara chadema hivi chadema vile. Utadhania ndicho chama tawala
 
wala hataishia hapo atamuhoji mbowe, hatamuhoji,lowassa, sumaye, kingunge na watu wengine
 
Siku akifanya hivyo nami ntajiunga na wanaomsifia...akishindwa basi mo sio bendera fwata upepo
 
Viongozi kuchota mali ya umma ulianza rasmi enzi za mzee ruksa, ndipo ukawa ni mfumo. Hakuna wa kudhibiti hali hiyo kwani mihimili 3 ya dola iliotegemewa kukaguana, bunge na mahakama haviko huru, uraisi ndio mambo yote.
 
Viongozi kuchota mali ya umma ulianza rasmi enzi za mzee ruksa, ndipo ukawa ni mfumo. Hakuna wa kudhibiti hali hiyo kwani mihimili 3 ya dola iliotegemewa kukaguana, bunge na mahakama haviko huru, uraisi ndio mambo yote.

ndo maana nikasema kwasababu yeye ndo kila kitu atatusaidia kuwahoji?
 
Ninaposema siasa ni mchezo mchafu na wanasiasa ni wajuzi wa kuteka akili za watu huku wakifukia mambo muhimu, baadhi husema sipendi maendeleo ya viongozi hasa Mh Pombe..

Sasa nawauliza ni juzi tu tumesikia Mh Jk kakomba hazina yote, lakini pia sisi kama wadau tunaowaweka viongozi madarakani tuna haki ya kujua JK na Mkapa walivyopata mali zao,,

sasa je Mh Pombe atatusaidia kuwahoji jinsi walivyozipata ili tujue kua yeye ni kiongozi wetu na hayuko kwa ajili kulinda masilahi ya watu fulani?

Jf hii haifanani na kumteua mama Anna Mngwira kwenye serikali ya raisi Magufuli...acheni kuchomekea
 
Mi nataman maufisadi yote makubwa makubwa yaundiwe tume huru na ya wazi kama ile iliyoundwa Africa kusini Mandela alipopata urais. Ile tume ya akina Desmond tutu.

Tuwekane wazi nani alifanya nini kwenye zile kadhia

Ikiwezekana hela zetu zirud

Tuangalie baadae kifanyike nini ili maufisadi Yale kamwe yasijitokeze tena na yakijitokeza ijulikane yatashughulikiwa vipi maana utakuta mpaka rais au waziri mkuu anahusika
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom