Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Katika wabunge wa CCM wachache waliokua wakifanya kazi zao kwa weledi wa hali ya juu basi ni Khamis Kagasheki, alikuwa ana uchungu sana na maliasili hasa majangili waliokuwa wanahatarisha usalama wa wanyama pori hasa tembo, alisimama kidete hadi kuforce operesheni tokomeza kuanza ni bahati mbaya watekelezaj vyombo vya ulinzi ndio vilivyoharibu kwa kukosa weledi wa walichotakiwa kukifanya na Kagasheki kama kanuni ya collective responsibility akajiuzulu huku wengi tukijua kosa halikuwa lake per se.

Nadhani ni muda muafaka kwa serikali iliyodhamiria kufanya kazi ya Magufuli kurudisha hili jembe mahal husika, yule bishoo Nyalandu hana lolote ndio walewale wana conflict of interest na sekta ya utalii kinyume na kanuni za utumishi wa umma.
 
Naunga mkono hoja 100% .... Kagasheki ni Kiongozi shupavu asieyumbishwa ... Watampa ? Maana watu wa Dini yake hawatakiwi ...
 
Watanzania mnanogewa sana na mbwembwe, ila unapokuwa mshabiki wa haya hakikisha hujihusishi na madili yoyote, maana am afraid Watanzania wengi wanaishi kwa wizi na wanaotegemea kipato halali ni wachache mno, shangilia iliyopo ni ya wale ambao network ziliwapita pembeni lakini wengi ni majizi.

Nitakuwa mshabiki wa Magufuri akirudisha zile nyumba zetu alizouza kwa bei ya chee mpaka na yeye moja akahonga mchepuko.

Mambo yake binafsi hayo yaache we jali kszi yake anaitekeleza
 
Watanzania mnanogewa sana na mbwembwe, ila unapokuwa mshabiki wa haya hakikisha hujihusishi na madili yoyote, maana am afraid Watanzania wengi wanaishi kwa wizi na wanaotegemea kipato halali ni wachache mno, shangilia iliyopo ni ya wale ambao network ziliwapita pembeni lakini wengi ni majizi.

Nitakuwa mshabiki wa Magufuri akirudisha zile nyumba zetu alizouza kwa bei ya chee mpaka na yeye moja akahonga mchepuko.

Hayo mambo yake binafsi we jali kazi yake
 
magu nadhan ataliona hili kuna ubadhirifu mwingi sana sekta ya utalii, kuna kombora aliwatumia siku anaongea na wafanyabishara kua mnashangilia watalii wameongezeka lakin je wameingiza sh ngap? ktk kutafuta solution ya matatizo hayo nadhan ataangalia namna ya kuweka watu sahihi pale na naamin bwana kagasheki anafaaa kurudishwa ni mtu asiyeogopa kuwajibika!!!
 
Naunga mkono hoja kwa 100%

Kagasheki alitolewa pale baada ya kuanza kuwatibulia mchwa pale Maliasili na Utalii. Nyalandu alikuwa anamzunguka ili apate uwaziri.

Ni mtu pekee kwa sasa ambaye kama atapewa Wizara hiyo, anaweza kuanza kwa speed ile ile ya Magufuli.
 
Kagasheki ni mtu wa kazi kwakweli amefanya vizuri tangu ameibua uozo wa barrick kule North Mara na hata ndani ya MALIASILI amefanya vizuri. Nasikitika kuwa nguvu ya mabadiliko na mabavu ya Lwakatare vimemnyima ubunge na uzuri hakutaka hata kuiba kura.
 
Akapumzike sasa, alipewa nafasi akaichezea, sasa abaki kusugua benchi. Kila ngoma ina mpigaji wake, hii ngoma ni mpya, ya Mkweree imerudi Msoga.
 
Magu pta hapa huu ni ujumbe toka kwa wananchi mpe huyu Kaga
 
naunga mkono 100% toka kagasheki ameondoka hakuna tena meno ya tembo yaliyokamatwa, kujiudhuru kwake ni fitina za vigogo wenye biashara hiyo haramu! MH: Dr. MAGUFURI RUDISHA KIFAA HIKI!
 
Ngoja majipu ya huko yapasuliwe ndio tutajua kuwa alikuwa na roho nzuri kwa nchi au vinginevyo.....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom