Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
ndiyo atakuwa amerogwa, siyo bure haiwezekani mtu mwenye akili timamu afanye mambo kama anayoyafanya. Aliposema pesa za kutupongeza sisi wabunge zitumike kununulia vitanda nlishtuka kidogo ila nikasema mzee ulimi uliteleza. Nikanyamaza na nikahisi kuwa inawezekana kabla ya kuja kwenye kile kijikao alikuwa amekunywa au amevuta kitu maana katika hali ya kawaida mtu asingeamua maamuzi kama yale.

Imagine tumefanya kampeni miezi hiyo, kwa shida ,mateso n.k tumekoswa koswa kuuawa na kuua pia, leo mashirika haya kwa kutambua mchango wetu wametuchangia ili watupongeze kwa kazi kubwa tuliyofanya ya kuomba kula kwa wananchi na hatimaye wananchi hawa wametupatia kula na nyingine tumejichukulia wenyewe leo tunatakiwa kujipongeza kwa sisi tuliofanikiwa kurudi tena bungeni anasema eti zikanunue vitanda muhimbili. Kweli? Hii ni akili sawa sawa? Muhimbili wagonjwa wapo miaka na miaka lakini sherehe yetu sisi ni mara moja kwa miaka mitano what was wrong with that? Huyu mzee anatumia kinywaji gani?

Miaka 10 wagonjwa wanalala chini muhimbili hakuna aliyelalamika. Ina maana yeye ndo amewaona sana kuliko sisi wabunge na rahis wetu aliyepita? Huu ni unafiki. Hawa wagonjwa hawaendi kustarehe kule mpaka kila mtu alale kitanda chake.kwani kule lodge? Tena amesababisha kwa hivi sasa wagonjwa wengi hata wakiambiwa wamepona hawataki kuondoka kurudi kwao kwa kuwa kule wakirudi wataenda tena kulala kwenye mikeka. Tumeanza kupata shida mtu hata akiumwa kichwa anakuja kuhimbili anasema sasa kuna huduma nzuri anataka alazwe hata week mbili.
Tena amesababisha hata manesi na madaktari wawe wazembe maana vitanda vingi mpaka vinabaki halafu manesi na madaktari wanalala. Na wengine wamepeleka vingine ofisin mwao.

Haya hilo likapita, leo siamini eti siku ya uhuru nipo home na wife ananambia siku ya usafi. Hajui usafi ushaanza kufanywa na mh magufuli huko bandarini na tra. Wife naye anashadadia tu leo siku ya usafi mimi roho yangu haijatulia hata nikiwaza usafi huu kwa mh magufuli asije akasafisha na kwenye hizi kamati zetu za bunge. Maana huku nako si haba kuna kauchafu kake. Wananchi hawashangai kuwa kwa nini tunagombea sana ubunge kwa hali na mali, kwa machozi ,jasho na damu..hata tukiambiwa tupeleke viu

:d:d:d😉😉
 
Asiwasahau Samwel Sitta na Harrison Mwakyembe maana hao nao walikuwa mawaziri wakati hayo madudu yanafanyika vinginevyo itakuwa ni MASINEMA TU.
 
Uhuru wa Tanganyika...safisha gereza la Tanganyika kuwarejesha masheikh wa zanzibar kwao...
Lisitumike kutia uchafu uhuru wa tanganyika...hilo ni katika majipu ya Kikwete ambayo yameiva..lipasue tuamarishe umoja....
 
Mheshimiwa Raisi na Waziri Mkuu kwa moyo wa dhati napenda kuwapongeza kwa ujasiri mliokuwa nao wa kupambana na ufisadi uliokithiri katika nchi yetu ya Tanzania. Ninafahamu kwamba mko kwenye opersesheni tumbua majipu ila naomba sana mtembelee Hifadhi ya Ngorongoro maana na kwenyewe kuna majipu yanayohitaji tiba. Sababu ya mimi kuwaomba mtembelee eneo hilo ni hizi hapa;


1. UBADHIRIFU WA KUTISHA WA KAIMU MHASIBU MKUU BW. SEZARY SEMFUKWE
Mwanzoni mwa mwaka huu niliripoti ubadhirifu wa kutisha wa Mhasibu huyu wa kiasi kinachokadiriwa cha shilingi milioni 240 iliyopelekea mwandishi wa habari wa gazeti la mtanzania kumuhoji na kukiri ni kweli alizipokea pesa hizo. Haikuishia hapo kwani kwenye ripoti ya wakaguzi wa TAC ilionyesha kuna pesa zilizochotwa huku kukiwa hakuna viambatanisho sahihi na vilevile kulikuwa na milioni hamsini iliyotafunwa bila kuwa na maelezo yeyote.Niliambatanisha viamabanisho vyote na kuwaomba TAKUKURU wafuatilie jambo hilo lakini mpaka sasa hakuna hatua yeyote iliyochukuliwa na Mhasibu huyu anaendelea kutafuna hela na kutamba kwamba hakuna mtu atakaye muweza. Nadhani wafuatiliaji wa suala hili toka TAKUKURU walipewa kidogo kidogo.
Jambo la kushangaza Mhifadhi wa Ngorongoro Dr. Manongi amekuwa mstari wa mbele kumlinda mhasibu huyu wakati ushahidi upo wazi. Sasa cha kujiuliza kama Dr Manongi na Bodi ya wakurugenzi waliweza kuwasimamisha kazi baadhi ya watumishi waliohusishwa na miamala ya shilingi milioni kumi( 10,000,000) kwanini huyu inashindikana? Waliunda Tume feki iliyokuwa inaongozwa na Mkaguzi wa wizara Mrs Flora Msami ili imsafishe mhasibu huyu lakini mwisho wa siku wafanyakazi wa Shirika hilo walimweleza ukweli kuhusu wizi unaofanywa na Bw. Semfukwe. Lakini cha ajabu ripoti haikuwekwa wazi ili wafanyakazi wafahamu nini kilichojiri.Tunafahamu Mrs Flora alikuja kwa ajili ya kupata pesa za kwenda kumtibu mwanao anayeumwa masikio huko India. Manongi nilikuhahikishia lazima hilo jipu litumbuliwe penda usipende maana waliokuwa wanakupa kiburi hawana mashiko tena katika nchi hii. Viambatanisho vya miamala iliyochukuliwa na Bw.Semfukwe nimeviweka.


2. MWENDELEZO WA AJIRA ZA UPENDELEO

Kama mtakumbuka kwenye moja ya makala yangu niliwaeleza Afisa utumishi wa Hifadhi hiyo Bw. Mackiros ni kihiyo na nilisema hivyo nikiwa na uhakika na ninachokisema. Na vilevile kwa kunukuu maneno ya bosi wa zamani wa Bw Mackiros pale chuo cha DUCE aliyesema hivi nanukuu ??uwezo wa Mackiros ni mdogo sana katika kuchambua mambo na kufanya uamuzi sahihi wenye hekima mwisho wa kunukuu.
Miezi 6 iliyopita Hifadhi hiyo ilitangaza ajira za mafundi wa gereji na waongoza mitambo waombaji wawe na sifa za elimu ya kidato cha nne. Kampuni ya PricewaterhouseCoopers (PWC) ilishinda tenda hiyo na ikafanya usaili na walioshinda wakaajiriwa.
Miezi mitatu baadae Shirika hilo hilo lilitangaza ajira kwa upande wa utawala na TEHAMA na manunuzi. Wenye sifa waliomba na kilichokuwa kinasubiriwa ni kufanyika kwa usaili. Ila cha kushangaza badala ya kufanyika kwa usaili Bw Mackiros pamoja na Mkaguzi wa ndani mwenye mbwembwe lakini fisadi Bw. Maleva waliondoka na kwenda vyuo vya uhasibu vya Arusha na Dar es salaam na kuchukua wanafunzi waliomaliza masomo ya uhasibu, manunuzi na TEHAMA kisha wakawafanyia usaili na kuleta majina yao kwenye uongozi wa shirika na kuyabariki then wakaajiriwa. Sasa swali la kujiuliza kama mlitangaza ajira kwanini hamkufanya usaili badala yake mkaenda kuchukua wanafunzi ambao ndo wamemaliza hata vyeti hawajapata na mbaya zaidi sio wale wanachuo waliokuwa waliofanya vyema katika masomo yao kuliko wengine. Ushahidi huu umepatikana kwa wahusika wenyewe na kuuliza kwenye vyuo husika. Hapa tunarudi kule kule kwenye lile suala la ajira za kujuana.

Watuambie ni vigezo gani walivyotumia kwenda kwenye vyuo hivyo viwili wakati nchi hii ina vyuo vingi vyenye sifa zinazojitosheleza? Je hamuoni mliwanyima fursa wanachuo wengine waliosoma kwenye vyuo vingine bora nchi hii kama UDSM, Mzumbe, IFM n.k? Kama mliweza kutangaza ajira za fundi wa gereji aliyemaliza kidato cha nne kwanini mlishindwa kutangaza kazi ??sensitive?? na za professional kama hizo?
Hapa ndipo ninapoona umuhimu wa kupasuliwa majipu maana baadhi ya wakubwa wa Shirika hili wameshaona taasisi hiyo ni kama mali ya mama zao.

3. PENDEKEZO LA MUUNDO MPYA WA SHIRIKA NA ?SCHEME OF SERVICE?
Taasisi hii ipo kwenye mchakato wa kuunda muundo mpya wa Shirika na kuachana na ule wa zamani lakini ukikaa chini ukapitia miundo yote miwili utagundua kabisa muundo wa zamani ulikuwa bora na ulifanywa na watu makini wenye nia njema na Shirika kwa kipindi chake kuliko huu mpya. Na sababu kubwa ni kwamba muundo mpya umeongozwa zaidi na tamaa za wadau wa uundaji. Kama miaka ishirini iliyopita wakati wasomi sio wengi nchi hii ilionekana Mkuu wa Idara awe na shahada ya uzamili( ?MASTERS DEGREE?) lakini leo hii nchi ina wasomi wa kutosha unasema haifai awe na stahada( ?Bachelor Degree?) Kwa watu wenye kufikiria mbali tunaona kabisa kuna watu wanatengenezewa mazingira ya kuzishika nyadhifa hizo. Taarifa nilizo nazo mchakato huu ulifanyiwa kazi na wajumbe wachache wa menejimenti na hao ndio waliouharibu kabisa. Mfano mdogo ni Idara ya mambo ya kale ambayo kwa sasa anayekaimu ni Injinia Joshua mwankunda ili kuhakikisha hakosi nafasi hiyo ameweka kigezo kimojawapo cha mtu kuwa Mkuu wa idara ya mambo ya kale ni awe Injinia, Hivi jamani kama mainjinia wataacha kufanya kazi zao na wakaingilia kazi za mambo ya kale wenye professional hizo wakafanye nini?
Kuonyesha namna gani Bodi ya Ngorongoro ilivyo na watu upeo mdogo na wao bila kufikiria na wakabariki muundo huo na sasa inasubiri Wizara ya maliasili pamoja na hazina wapitishe. Ombi langu kwenu Wizara na hazina msipitishe huo uchafu maana mkicheza fagio la Magufuli lazima liwapitie. Na mbaya zaidi wafanyakazi hawajashirikishwa wakati muundo huo wakati ni kwa ajili yao sasa tujiulize mbona muundo wa awali wafanyakazi wote walishirikishwa? Ni kitu gani mnachokificha? Acheni upuuzi hilo Shirika ni la umma na kila mtanzania anahitaji kulifaidi.

4. BW. MWEYUNGE (KAIMU MWANASHERIA) KUSHIKILIA NAFASI MBILI KATIKA TAASISI MBILI TOFAUTI.
Katibu Mkuu wa Wizara ya maliasili na utalii alifanya uhamisho wa watumishi wawili wa TANAPA pamoja na mmoja wa Ngorongoro kwenda TAWA (Tanzania Wildlife Authority) Morogoro. Lakini cha kushangaza watumishi wa TANAPA wamesharipoti na kuanza kazi ila wa Ngorongoro Bw.Mweyunge anaendelea kushikilia sehemu zote mbili na kulipwa posho kinyume na utaratibu. Hivi yeye ni nani? Ina maana huko Ngorongoro hakuna watu wa kuzifanya kazi zake kwa ufanisi? Au anaogopa akiondoka lile eneo aliloligawa kwa LEOPARD TOURS ambalo lipo kinyume na utaratibu litawekwa wazi? Je ina maana yeye ni mtu muhimu kwa NCAA kuliko Loibook aliyekuwa TANAPA? Hiyo jeuri anaipata wapi ya kutunushiana misuli na Katibu Mkuu wa Wizara?

Wengi wenu mlisema nimepotea ila ninawahakikishia nimerudi tena kwa nguvu mpya ya kupasua majipu na ninawasihi mjipange maana ni lazima muisome namba.

Mwisho kabisa napenda kuwatakia kila la kheri Mheshimiwa Rais, Makamu wa Raisi, Waziri Mkuu pamoja na Watanzania wote wenye kupenda mabadiliko Mungu awabariki sana.
 

Attachments

Kama Rais Dr.Magufuli anataka apate watu safi na hodari wa kumsaidia kuongoza nchi,namshauri atoe form maalam na iwekwe mtandaoni,na kwenye vyomba vingine Vya habari.
Hii fomu iwe na VIGEZO vya kuomba uwaziri na unaibu waziri.
Hapa atawapata watu hodari,wasiowaoga wala wanafiki .
Baada ya kuomba wafanyiwe intensive VETTING na TISS
Kama hili litafanikiwa basi,Tanzania ya Magufuli itapatikana.
 
Jamani kwenye hii mamlaka hakufai! Binafsi naona kwa zilizotumbuliwa tayari hii mamlaka ifuatie tu,hakufai humu ni ufisadi ufisadi ufisadi mpka aibu. Nasikia viongozi ndani ya mamlaka hiyo wanajiandaa kua tayari kutumbuliwa majipu! Yaani wanajipanga kumhadaa Magufuli kwa fake documents.
 
Ishu ya TANAPA mbona hiko wazi...jibu bado halijaiva vizuri
 
Niliweka uzi hapa nikasema sasa wataanza kujipanga ili wasiumbuke mbele ya kamera.

Tusubiri.
 
1. VIATU NA MIKANDA YA NGOZI TOKA NJE YA TZ
2. TOOTHSTICKS TOKA NJE YA TZ
3. JUICE AINA YOTE TOKA NJE
4. BIDHAA ZOTE AINA YA PLASTIC IKIWEMO NA MIFAGIO AINA YOTE PIA PIPE AINA ZOTE ZA BOMBA
5. BIDHAA AINA ZOTE ZA MBAO TOKA NJE YA TZ
6. KOKI AINA ZOTE ZA MABOMBA
7. BIDHAA AINA ZOTE ZA CHOKAA IKIWEMO NA RANGI
8. AINA ZOTE ZA BIDHAA MASHULENI
9. VYOMBO VYOTE VYA MAJUMBANI


Ukishafanya hivyo yaani Tanzania ya Magufuli ya viwanda itawezekana kabla hata haijafika 2017. Kupiga marufuku bidhaa hizo hapo juu toka nje ya TZ kutachochea ujenzi mkubwa sana wa viwanda vya kutengeneza hizo bidhaa mhimu kwa matumizi ya binadam. wawekezaji wataitumia hiyo fursa kukuza wigo wa biadhara zao na kuongeza ajira kwa Watz.

Jambo la mhimu kwako ni kuhakikisha umeme haukatiki kwakuwa tayari gass asilia ipo. Pia uongee na makampuni yanayo jishulisha na utengenezaji wa bidhaa za kielectronic mfano: computer, simu za mkononi, cd, flash, aina yote ya vyombo vya muziki, memory cards e.t.c kuja kujenga viwanda vya kuzalisha bidhaa hizo. Mungu akikupa neema zungumza pia na yale makampuni yanoyotengeneza vipuri vya magari ikiwezekana waje kujenga viwanda vya hiyo shuguli.

Mungu akikuwezesha kuyafanya haya ifikapo 2024 tutaibadilisha katiba yetu ili uendelee kutuongoza kwakuwa utakuwa umeyafanya yale amabayo si marais waliokutangulia tu bali marais wote wa Africa hawajayafanya kuwa wanapoingia madarakani kazi yao hugeuka kujilimbiza mali nying mno ambazo kiukweli hawataweza hata kuzimaliza kwa matumizi yoyote binafis. Kadhia hii imeleta kilio kikubwa mno katika bara zima la Africa, na hii ndiyo imesababisha nchi zote za Afriva kuwa tegemezi kwa weupe huku tukiwazidi kwa utajiri wa vitu vya asili. Ni aibu kubwa imetupata waafrica hata mbele zake YEYE aliyetuumba tumeleta fadhaa kumbwa ya kwamva tumeonekana watu wasiojipenda na wasio na akili hata ya kujua kuwa ni matajiri kuwazidi watu weupe.

Uwepo wa viwanda ktk taifa ni injini ya maendeleo; chonde chonde baba yangu Magufuli wingu la tamaa ya kujilimbikiza mitrilion huk wengi wakifa maskini lisikufunike kabisa bali wewe Rais Magufuli uwe hodari ukafanye yaliyo mema mbele zake aliyekuumba na mbele za watu wako watanzania

Basi, Neema na Amani itokayo kwa Mungu wetu, yaani BABA yetu wa Mbinguni iwe juu yako katika utumishi huu uliokupa Yeye aliyejuu kupita vyote; uwe hodari, ufanye kiume jitie nguvu na wala usiwaonee haya wote wapendao dhuruma na kuhujumu nchi yetu; watu kama ni wabaya si kwa watanzania tu bali hata mbinguni walishakataliwa;

Wewe uwe na moyo wa kuijenga Nchi yetu kwa moyo wa upendo kwa Tanzania na kwa Mungu: Sasa na atukuzwe MUNGU muumba mbingu na nchi yeye aliyetupa kukaa kwenye kiti cha enzi cha Tanzania ili ufanye yaliyo ya akili. Amina na Amina.
 
Nguo za aina zote pia zipigwe marufuku ila vitambaa vya aina zote viruhusiwe
na vipunguzwe kodi
 
Apige marafuku nguo za wanawake za uch eg; skin tite wanazotoka nazo wanawake bila kujali zinaonyesha uchi
 
IRINGA biashara ya NOTI BANDIA imeshamiri kila kona...Na inafanyika kwa uwazi mno na inalipa kweli kweli..
Watu wanajenga majengo makubwa ya hatari, wanasomesha watoto shule za maana na wanamiliki magari ya kifahari balaa
Cha ajabu askari wa jeshi la POLISI wanahusika moja kwa moja na hii kitu na wanaifanya kama "part-time bussiness"...

Kuna viwanda vya kutengeneza hizi noti feki kila kona kuanzia KIHESA, MSHINDO, IPOGOLO,ILALA, MTWIVILA, maeneo ya nyuma kabisa ya Ikulu ya mkoa ya Gangilonga na kila kona ya mji na na vingine viko nyuma tu ya vituo vya polisi na vinajulikana kwa kila mtu hata kwa polisi wakuu...
Noti moja FEKI moja huuzwa kati ya shilingi elfu sita(6,000) mpaka elfu nane(8,000) na ni biashara inalipa kwa watoto wa mjini kwa kushirikiana na baadhi ya askari polisi...

Juzi kati kuna dogo hapa kitaa alikamatwa na "MZIGO" wa kutosha na askari polisi...cha ajabu akanyang'anywa mzigo na wakamkamua kama ELFU 80 hivi ya kutuliza soo mambo yakaisha "KI-UTU UZIMA"...Jioni karudi nyumbani mdingi wake kam-maindi ni kwa nini amekwapua mzigo wake na anamuharibia kazi inayomuweka mjini tangu miaka ya 90, akamuonya sana na akampa namba za simu za baadhi ya "WAKUBWA WAPOLISI" ili siku akiwa na mzigo na mambo yakaharibika awatafute wata solve issue...
Baada ya muda jamaa akawasiliana na "WAKUU" jamaa akarudishiwa mzigo wake kwa "FAINI" waliyoelewana

TISS MKO WAPI??
TISS MNAFANYA NINI??

Minadani ndiko wanakoziingizia kwenye mzunguko hizi noti feki...wakulima kwa sababu ya njaa zao na ujinga wao hawajui kutofautisha FEKI na ORIGINAL...wakija kustuka washaliwa.

Fedha hizi kuna tetesi kuwa pia zinaingizwa kwenye mzunguko kupitia benki yetu pendwa "ya sirikali"

Haiitaji intelijensia kama ya KOVA au kuundwa TUME MALUMU kutafuta HIVI VIWANDA au HAWA WAPIGA DELS..we njoo tu stendi ya mabasi pale MIYOMBONI ulizia kijana yeyote wa mjini "WAPI NAPATA FEKI"...utapelekwa moja kwa moja mpaka jikoni....

Magufuli okoa hii nchi...Au kama umehalalisha hii biashara tuambie na sisi tufanye maana maisha mitaaani magumu mnoo kwa kuwa inalipa...TENA INALIPA SANA TU.....

Hata sie tunapenda kujenga majengo mazuri ya kifahari na kuendesha magari mazuri
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom