-Njia ambazo zinatumika kuwakabili wanaokujaribu, zinakuingiza zaidi majaribuni. Hii tabia ya kukamatakamata watu hovyo, ndiyo inakufanya ujaribiwe zaidi na zaidi.
-Mimi kama raia mtiifu, lazima niishauri serikali ; Tabia ya kuwakamata akina Lissu, Zitto, Mbowe na wapinzani wengine, haiwafanyi wakuogope, bali unawajenga kitofauti.
-Na wewe si umesema ni wa tofauti? Basi na wenyewe unawafanya wawe wa tofauti. Unawakamata na kuwaweka mahabusu, wakiachiwa wanaongea yaleyale yasiyokupendeza. Unawakamata tena, mwisho wanazoea, wanaona ni sehemu ya maisha yao.UNAJARIBIWA NA UNASHINDWA ZAIDI
-Ogopa sana wapinzani, wakiona jela ni sehemu ya maisha yao watakusumbua mpaka maisha ya Ikulu utayaona yamejaa presha. Si presha za kazi ya kuwahudumia wananchi, ni presha ya usalama.UTAJARIBIWA KAMA HUTOBADILIKA
-Wapinzani wamezowea vurugu mechi za dola. Wakiona virungu hawaogopi, ukiwaonesha bunduki wanasogea kidogo tu. Ukiwapiga mabomu ya machozi, utapita muda yatakauka, ukiwamwagia maji ya kuwasha, wanawashwa, baadaye muwasho unaisha, maisha yanaendelea.
-Wapinzani wanapokuwa sugu baada ya kusumbuliwa muda mrefu na serikali, wanakuwa hawana tofauti na magaidi wanaodai haki zao bila kuogopa kifo. Wanaweza kufanya chochote bila kuhofia dola, maana kwao dola huona ni adui yao. Hiyo ni hatua mbaya sana.
-Naomba nikuulize swali MAGUFULI, ni wapi wapinzani wamewahi kunyamazishwa kwa nguvu za dola hadi wakatulia ? UMESHARUSHUSU KUJARIBIWA
-Binadamu ameumbwa kuzoea mazingira. Akiwa anasikia sana milio ya risasi, inafikia wakati anazoea. Akizoea mabomu, akisikia tu, anakimbilia kulala chini. Hata mfungwa wa muda mrefu, wakati mwingine hushangaa uraiani watu wanaishije.
-Ingekuwa matumizi makubwa ya dola yanasaidia watawala kuwanyamazisha wapinzani, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere angekata tamaa na kwenda Butiama, akawe Chifu wa Wazanaki na habari za kudai uhuru wa Tanganyika angeachana nazo.
-Hata hivyo, kadiri walivyokuwa wakimwandama ndivyo naye alivyozidisha harakati. Utawala wa Kiingereza, ulimfanya Mwalimu Nyerere awe sugu, akaendelea kupambana mpaka uhuru ulipopatikana.Vyama vya upinzani navyo havitonyamaza hadi wapate kile kinachotakiwa.
-Nguvu kubwa ya dola ingekuwa inasaidia kunyamazisha upinzani, Nelson Mandela ‘Madiba’, angenywea tangu miaka ya 1960. Akina Jacob Zuma, wasingeukwaa urais. Makaburu wangeendelea kutawala na ubaguzi wa rangi ungetamalaki hadi leo.
-Ni kwa sababu nguvu kubwa ya dola huwa hainyamazishi upinzani, ndiyo maana Sani Abacha hakuwahi kuifanya Nigeria itulie. Joseph Kabila, hajamudu kuiweka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) katika utulivu, vilevile Paul Kagame na utulivu wa Rwanda ni magirini tu.
-Unadhani miaka 27 ambayo Mandela aliishi jela, siku zote hizo zilikuwa za mateso? Ukifikiria hivyo utajidanganya kabisa, vipo vipindi ambavyo alifurahia maisha hata kama alinyimwa uhuru kwa kukaa gerezani.Lakini alijua kuna siku atapata ushindi na alipata.
-Tazama sasa, wakati Mandela akizoea maisha ya jela na kuona ni sehemu ya kawaida katika maisha yake, nje, Serikali ya Kikaburu ikawa kwenye mateso makubwa kutokana na presha ya kumfunga jela Mandela pamoja na wanaharakati wengine.
-Chukua hii; Matumizi makubwa ya nguvu ya dola dhidi ya wapinzani, kwa kawaida huifanya serikali yenyewe iteseke kuliko hata wapinzani wenye kukamatwa na kufungwa.
-Kwa maana kwamba serikali hukosa utulivu kwa sababu wapinzani ni viongozi, kwa hiyo wanakuwa na kundi kubwa la wafuasi, ukiwakamata inabidi shughuli nyingi zisimame na gharama za kukamata ni kubwa mno. Hayo ni mateso makubwa.
-Fikiria kumsafirisha Lissu kutoka Singida mpaka Dar es Salaam, kumsaka Zitto usiku na mchana ikiwa ni pamoja na kuizingira nyumba yake kwa siku tatu. Kisha Lissu anapewa dhamana anaondoka akiwa anatabasamu, Zitto anajitokeza mwenyewe halafu anasema “siogopi.” MAJARIBU GANI UNAYOYATAKA ZAIDI YA HAYA
-Tuachane na mateso kwa serikali, akina Lissu wakizoea jela, watakuwa wanaona kama vile wako ofisini kwako pale UFIPA. Kule kuna watu, siasa zinaweza kuendelea hukohuko ndani.
Ninakukumbusha kuwa kuna kipindi Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, alikataa kutoka jela, alitaka aishi hukohuko baada ya kuona anaonewa sana polisi uraiani.
Ujumbe wangu ni kwamba MAGUFULI afanye kazi zake inavyotakiwa. Awaache akina Lissu, Zitto, Mbowe na wapinzani wengine wafanye siasa zao, yeye ajikite kujenga nchi.
Ikiwa anaona wapinzani wanataka kulifanya suala la Bunge Live kuwa ni ajenda yao, yeye anamwambia Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye aruhusu bunge lionekane moja kwa moja.BILA HIYO TUNAKUJARIBU NA TUTAKUSHINDA
Kama ni bajeti ipangwe vizuri na iwe kweli, sio yenye chumvi kibao na majigambo mengi wakati ni hewa tupu.HAPA LAZIMA UJARIBIWE
Kuwafukuza bungeni wabunge haisaidii, mwisho wataona ni sehemu ya maisha yao. Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kuwakomoa wapinzani, haisaidii, watajenga chuki tu. HAPA LAZIMA TUTAKUSHINDA Umejenga majaribu mwenyewe
Dawa ya kuwanyamazisha wapinzani sio kuzuia mikutano ya kisiasa,bunge live,kupitisha bajeti kwa nguvu na kejeli kibao,kuwatukana wapinzani majukwaani,kutumia polisi kila siku,kuwafukuza bungeni, HAPA LAZIMA TUKUJARIBU NA TUTASHINDA.
Nimkumbushe Rais Magufuli kuwa enzi ya utawala wa Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Rais Benjamin Mkapa, Chama cha Wananchi (Cuf), kama chama kikuu cha upinzani wakati huo, kilitangaza siasa za kimapambano kwa kauli mbiu ya jino kwa jino.
Mapambano yalikuwepo makali kweli na wapinzani hawakunyamza. Ni kipindi ambacho Cuf walijitangaza kuwa wao wapo Ngangari, aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Omar Mahita, akasema polisi nao ni Ngunguri. Ikawa mapambano ya Ngangari na Ngunguri.
Kipindi cha utawala wa Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Dk Jakaya Kikwete, mambo ya Ngangari na Ngunguri hayakusikika, mapambano ya jino kwa jino, hayakuwepo. Ni kwa sababu kulikuwa na uhuru wa wanasiasa wa upinzani kufanya siasa zao.
Pamoja na uhuru uliokuwepo, matukio machache yalipotokea kati ya upinzani na dola, athari yake ilionekana. Rejea mauaji ya Arusha kama somo la karibu zaidi katika nyakati za machafuko wakati wa JK.
Vitisho vya “sijaribiwi” na “mimi nipo tofauti”, vinaweza kurejesha jino kwa jino na Ngangari, matokeo yake yakakutesa wewe MAGUFULI zaidi kuliko kujenga utulivu wa kitaifa.
#UKUTA NI LAZIMA September 1