Maoni ya wajumbe 'walio wachache' katika Kamati namba Nne iliyowasilishwa na Mhe. Tundu Lissu!

Maoni ya wajumbe 'walio wachache' katika Kamati namba Nne iliyowasilishwa na Mhe. Tundu Lissu!

Tundu Lisu yuko networked kwenye hii dunia huwezi kumdanganya CHOCHOTE.. Lazima mjue alikuwa mwanaharakati kabla ya kuwa Mbunge na ni international activist...
 
HIZI SIO NONDO......
HAYA NI MAKOMBORA YA MAANGAMIZI.
Pamoja na kuunga mkono muundo wa serial I mbili, lakini nakiri kwamba hotuba Hii imenisisimua.
Nasubiri majibu dhidi ya LISSU toka CCM
 
Tbc hawajuwi kuwa kila jambo lina hasara na faida zake wamekata mawasiliano wanahisi wameweza kumbe wamebomoa !
Na vijana wa lumumba wote wamesha shituka afadhali wanafunzwa na ulimwengu tbc!
 
Ukisema aliyosema ni ya kweli tusingekushambulia hivyo ila tumefikiri kuwa wewe hutaki kusikia ukweli hata kama anayesema ni mkweli kwa wakati huo.
Huwa nnakula kiti moto na mama'ko wala si kinyemela wewe si ndio huwa unatukatia.

Nimeshasema na nnarudia tena, kila anaeponda fikra za Nyerere, mojawapo ni hii ya Serikali mbili feki, mimi nipo nae. Na Lisu yupo katika orodha ya wanaoponda fikra za Nyerere na leo kamuita muongo, mwaka 68 kaongea mengine na akaja akatenda mengine kwa kumfunga, Jumbe na wengineo. Hujamsikia Lisu alikuita Nyerere Muongo?

Leo Lissu amesema yale nnayoyasema mimi kila siku humu JF, kuwa Nyerere ni muongo, sasa mshambulieni na yeye.
 
Bado kuna mambo hujaweka hapa ambayo alisema ni ushahidi wa kutokuwepo kwa muungano na kutopelekwa kwa hati ya muungano UN. NA KATIKA HILI ALISEMA ANA USHAHIDI KWA HOJA ZISIZO PINGUWA NNE.

Ningependa mambo hayo yawekwe hapa na ningependa kusikia majibu yake kutoka kwa serikali.
Mwenye hoja zile nne aziweke hapa. mkuu 2chabruma tusaidie kuziweka hapa hata kwa audio.

cc Chabruma buchann
 
Last edited by a moderator:
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, TBC au aliyetoa amri TBC wazime mawasilisho ya Tundu Lissu hakutenda haki hata kidogo, labda iwe ni technical fault, tutapata hansard, walioko huko turushieni mawasilisho ya Lussu, alikuwa anaongea vizuri sana.

Leo mimi nipo na wote wanaomponda Nyerere kwenye huu mchakato, fikra za Nyerere siyo tu zilikuwa mbovu zimetuondolea Utaifa wetu, iweje leo nchi moja iwe na Utaifa na moja nchi nyingine Utaifa wake ufe? kwa kuwa tu Nyerere ndio kataka hivyo?

kumbe we bibi cku zingine unakuaga na akili timamu..hongera bibie..!hakuna cha technical error apo..mi nilikua live tbc taifa..lisu alipotamka khs hati ya muungano wakakata mara 1..na wakaweka matangazo yao ya kuusifu muungano
 
Inasikitisha sana,Hii ni
baada ya lissu kuja na ushahidi wa kutokuwepo hati za
muungano.Brilliant LISSU....!!

Naomba hii taarifa ya TBC kukata matangazo baada ya Lissu kuanza kuwasilisha maoni ya wachache iandikwe katika kurasa za mbele za magazeti ya kesho
 
Tuwekeeni link youtube tumchek lissu alivyoramba kisahani jamani, hawa TBC wanajulikana
 
Lisu Lisu Lisu we need your presentation here please, give us babu wewe ni zaidi ya serikali nzima ya jk and the likes
 
Bado kuna mambo hujaweka hapa ambayo alisema ni ushahidi wa kutokuwepo kwa muungano na kutopelekwa kwa hati ya muungano UN. NA KATIKA HILI ALISEMA ANA USHAHIDI KWA HOJA ZISIZO PINGUWA NNE.

Ningependa mambo hayo yawekwe hapa na ningependa kusikia majibu yake kutoka kwa serikali.
Mwenye hoja zile nne aziweke hapa. mkuu 2chabruma tusaidie kuziweka hapa hata kwa audio.

cc Chabruma buchann
Zitawekwa baadae kwani sasa cd zinaandaliwa na jua CCM wanataka kuwanyanganya waandishi zile Temu zao waizorekodi ili kufichua ukweli wa mambo ....vuta subira kidogo.
 
Tumefika pazuri sana walimfukuza tido wakahisi wanaweza jificha kumbe wanaumbuka
 
Heshima kwako kwa jitihada uliyochukua kufunua kile kilikuwa kifichwe.
 
Back
Top Bottom