Maoni ya wajumbe 'walio wachache' katika Kamati namba Nne iliyowasilishwa na Mhe. Tundu Lissu!

Maoni ya wajumbe 'walio wachache' katika Kamati namba Nne iliyowasilishwa na Mhe. Tundu Lissu!

Sisi Wazanzibar hatutaki TBC iturushie matangazo ya Bunge maalum,tupeleke ZBC wauturushie,TBC ya bara wanatunyima haki yetu
 
Ni kweli kaka hapo tulipofika ni pazuri sana. Ni suala la wakati tu Watanzania wategemee mabadiliko makubwa sio muda mrefu. maana ukiona hivyo ujue maji yamefika shingo. Mfa maji huyashika hata maji yenyewe ingawa hayashikiki
Tumefika pazuri sana walimfukuza tido wakahisi wanaweza jificha kumbe wanaumbuka
 
Hakika Lissu ni jembe book kumi yangu niliyotoa kusuport uchaguzi Singida kwa Lissu haikwenda bure. Asante wananhci tumewaelewa bado CCM tu ingawa nao upande wa Zanzibar wanaelewa.
 
Hayo maoni ya wachache ndio yale yaliyosomwa na Kigwangala pamoja na maoni ya wengi. Alichokatizwa Lissu ni ule ufafanuzi wa dakika 30. Hapo imekula kwenu, chama kubwa limeamua.
 
Name:
Number: by salma........................... mjumbe wa bunge la katiba
Content:
Matangazo yamekatika ghafla wanasema kuwa kuna tatizo la kiufundi kutokana na hali ya hewa lakini na huku tumekataa kuendelea mpaka tbc irudi kwa hivyo tumeakhirisha hadi j3 na ataendelea huyo Tundu Lisu na. Mwenyekiti amekubaki kuwa tunaakhirisha bunge hadi J3 msiwe na wasiwasi
Time: 4/12/2014 1:40:19 PM
 
Bado kuna mambo hujaweka hapa ambayo alisema ni ushahidi wa kutokuwepo kwa muungano na kutopelekwa kwa hati ya muungano UN. NA KATIKA HILI ALISEMA ANA USHAHIDI KWA HOJA ZISIZO PINGUWA NNE.

Ningependa mambo hayo yawekwe hapa na ningependa kusikia majibu yake kutoka kwa serikali.
Mwenye hoja zile nne aziweke hapa. mkuu 2chabruma tusaidie kuziweka hapa hata kwa audio.

cc Chabruma buchann
kuhusu ushahidi wa hati kutokuwepo UN anasema hivi
27/04/1964 walitakiwa na mwanasheria Mkuu (Costantine Paul) kupeleka hati ya muungano
06/05/1964 wakapeleka barua kwamba kweli wameungana na kusema wameambatanisha nakala ya Hati
14/05/ mwanasheria mkuu (Costantine Paulo) alitaka atumiwe hati mbili kwa ajili ya kusajili
sasa ushahidi kwamba haipo UN
2009-Andrey Golomoye alimwandikia mwandishi mmoja wa kitabu kwmba hakuna ushahidi kama hati ilipokelewa umoja wa Mataifa
Hati hii haipo UN wala Haipo Tanzania na ushahidi ni kama ifuatavyo (TBC wamepotea ghafla hewani)
 
Hakika Lissu ni jembe book kumi yangu niliyotoa kusuport uchaguzi Singida kwa Lissu haikwenda bure. Asante wananhci tumewaelewa bado CCM tu ingawa nao upande wa Zanzibar wanaelewa.

Kweli umaskini wa akili ni kazi sana.wewe ubongo wa kuku unafaham maana ya network? Na unafaham Leo bunge mwisho wake ulikuwa SAA ngapi? Ubongowa kuku
 
Tangu saa tatu nasikiliza bunge wameongea wakina kingwangala na wengine lakini alivyoanza Tundu Lissu tu(mwanasheria aliyebobea wa Chadema) baada ya dakika chache matangazo ya Live yakakatika nchi nzima. ameongea kwa ushahidi na data kutoka kwa wanaojiita wasomi,wabunge na mwalim Nyerere. CCM wanatuchezea sana lakini wajue kuwa ukweli hauwezi kuchanganywa na uwongo hata siku moja na Tundu amewaambia kuwa aliyezoea uongo hawezi kusurvive kwenye kweli.
 
Kama asemavyo mwenyewe haogopi kitu aliisha kufa akafufuka'come what may'
Mwakyembe kabla hajawa kiongozi wa ccm alikubaliana na anachounga mkono kukipinga leo, serkali tatu alizopendekeza wakati wa research yake ya udhamili leo hataki.
 
Utumbo mtupu, no intelligency
Wewe ni mfano mzuri wa mtu ambaye hajasoma,hana hoja, hajui lolote, anayesubiri fikra za mwenyekiti kumuongoza, kifupi MBUMBUMBU. Bravo kwa kutuonyesha uwezo wako wa kufikiri
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, TBC au aliyetoa amri TBC wazime mawasilisho ya Tundu Lissu hakutenda haki hata kidogo, labda iwe ni technical fault, tutapata hansard, walioko huko turushieni mawasilisho ya Lussu, alikuwa anaongea vizuri sana.

Leo mimi nipo na wote wanaomponda Nyerere kwenye huu mchakato, fikra za Nyerere siyo tu zilikuwa mbovu zimetuondolea Utaifa wetu, iweje leo nchi moja iwe na Utaifa na moja nchi nyingine Utaifa wake ufe? kwa kuwa tu Nyerere ndio kataka hivyo?

Kumbe wewe furaha yako hapa ni kuona tu Mwal. Nyerere anakandiwa eti eeh, udini mpaka kwenye damu we nguchiro, hopeless kabisa wewe!!
 
Wananchi tukatae na tupige kelele hotuba ya Lissu irudiwe jmatatu kwanza kabla ya kuendelea na mengine.Watanzania tuna haki ya kujua alichokisema Lissu!!
 
Ukwel ulipotoshwa tangu asil ya mwanadamu mf ni wakuu wa serikali ya kilumi wakati ule yesu anafufuka waliwapa walinzi rushwa ili wapotoshe ukweli kwa kusema yesu hajafufuka bali wanafunzi wake walimuiba wakati wao wamelala. Tangu lini mlinzi analala
 
Swala la kwamba Nyerere ni Muongo lipo wazi tumelisema sana Hapa lakini tukaonekana wadini....
Haya Leo Tundu Lisu kasema Nyerere ni Mzushi na muongo PRO CHADEMA mmesikia ?
 
Back
Top Bottom