Nimejaribu kusoma na kuisikiliza mijadala juu ya hili sakata la DP World. Kwa kweli mpaka Sasa kama taifa bado tunarumbana juu ya sisi Kwa sisi Cha kushangaza zaidi hata hao wasomi wa Sheria katika nchi hii wameshindwa kuwa na tafsiri ya pamoja katika mkaba huu.
Tofauti na ilivyotarajiwa sasa suala hili limetoka katika nyanja mjadala wa kitaifa katika uchumi likaingia katika nyanja za kisiasa na sasa limeingia kwenye udini.
Suala hili lipo mahali pabaya sana. Mimi binafsi sina shaka kabisa na kubinafisisha bandari kwa miradi kama vile Bwawa la Nyerere - Misiri na SGR - waturuki, Wala haijawahi kuwa mjadala. Ili kufunga mjadala wa DP World nashauri mambo yafuatayo:
1. Kufungua kesi kwenye mahakama kuu ya Tanzania ili itoe tafsiri katika vipengele vinavyobishaniwa kwy mkataba, ili tuwe na tafsiri Moja.
2. DP World apewe bandari nje ya Dar mfano Mtwara, Mafia au Tanga ajenge bandari Mpya Kwa gharama zake.
3. Serikali isimamishe mchakato na ipige marufuku mjadala huu hadi hapo itakapotangazwa.
MWISHO:
Amani ni tamu sana tusiichezee kisa umasikini wetu.