Maoni yangu kuhusu gari aina ya Harrier maarufu "Tako la Nyani"

Ni gari nzuri ni comfortable ndani kama huna mapepe, if you are here next level is landcruiser, spare zipo za kutosha, mafuta kawaida, but dont overspeed! Ingawa ina matatizo ya shockups but its good car! Had two of them! Asingekuwa jiwe ningekuwa kwa v8! Dis life!
 
Nilishaliendesha Dar to Songea zaidi ya mara tano nilijikuta natumia akili nyingi sana, maana mimi napenda sana mbio, lakini lenyewe ukifika 140 unaona kabisa linataka kupaa. Nimebaki zangu na GX 110 ndo mpango mzima natembea hadi namaliza kisahani
Wewe unajua unachoongea. Sasa vijana wanaburuza hizo Harrier kama Crown Athlete au GX110 matokeo yake zinawamwaga.
 
Haukusumbui? Yani mkuu nilioinunua kwa mtu sijui iligusa maji control yake ikawa inajipiga stata yenyewe nikaona hapa kuna siku nitakuta imekanyaga vichwa watoto
Hazina shida mkuu, hukuipeleka kwa fundi kujua tatizo n nn
 
Mkuu, nimenunua hii kitu kwa mtu miezi sita iliyopita ikanishinda nikauza niliyemuuzia kapiga mzinga maeneo ya senkenke kwa mbele mwezi uliopita, nilipata mshituko sana nikahisi kama ilikuwa inanitafuta.
.....
Ila jamaa mzima



Gari zenye bonnet na bod kubwa ikipata ajali ina madhara kidogo ukilinganisha na madogo
 
Ni gari comfortable sana na iko stable sana kwa barabara, khs kupata ajali sana labda kama ulivyosema zipo nyingi na wengi wanapenda sana kuzitumia kwa safari za masafa marefu, ila ukitembea kwa speed moderate 100km/h mpk 120 , hakuna shida....kimsingi gari yyt ukileta ujuaji mwingi inakumwaga.
 
Mimi Ninayo kuluga pumbu ya nyani.

Haili kbs mafuta

Sent using Jamii Forums mobile app
Kluger inameza mkuu!! Nimeidalalia juzi,mteja katoa hela nusu! Baada ya kuitumia kidogo ananiambia nifanye mpango arudishe hata Robo tatu ya kiasi alichonipa tuli re-sell!! Hata hizo "Tako la nyani" anazozisema Mshana Jr si zote zinakula mafuta kidogo! Kuna zinazomeza kama majini!! Maana si zote ni vVti engines! Sijui mengi kuhusu hii gari ila nilimuuliza mtaalamu mmoja akaniambi kwa kifupi tu kuwa zipo ambazo ni Hybrid,na ambazo si Hybrid!! Sikumwelewa sana ila ninachoelewa ni kuwa kuna zinazokula mafuta mengi na zisizokula mengi!
 
Juzi kati imeua mtu mahali, gari haina stability ikiwa kasi, labda hayo matako yake sijui halafu zinakufa sana kwa chini sijui shoker au nini ngongongo kibao tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mshana bwanaa yaani umekoleza mwandiko kwenye tako la nyani. kuliko hapa gari yenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…