Seif al Islam
JF-Expert Member
- Nov 14, 2011
- 2,156
- 639
Kwakweli nimekaa na kutafakari kwa kina juu ya nani hasa anayeweza kufaa kuchukua nafasi ya Mbowe ya uenyekiti wa CHADEMA taifa na kujiridhisha kuwa ndugu Tundu Lissu anaweza sana kuitwaa nafasi hiyo na kukiongoza chama kwa mafanikio zaidi kuelekea 2015.
kimsingi Vigezo muhimu nilichotumia ni
1.umahiri wa ndugu Lissu awapo bungeni na hata nje ya bunge katika kujenga hoja na kuisimamia.
2. Pia Lissu sijasikia akitajwa kwenye yanayodaiwa kuwa makundi ya wanaodaiwa kuusaka urais ndani ya cdm na hata nje ya cdm.
3.ana msismamo usioyumba wala kutikiswa na nguvu ya fedha wala umaarufu wa bandia.
4.hatoki pia kanda ya kaskazini hivyo atawazima wale wachache wanaobeba hoja mufilisi ya ukanda ndani ya cdm
5.atasaidia kuiinua CHADEMA katika kanda ya kati yaani mikoa ya singida,dodoma na manyara kwa kuleta hamasa
6.sio mtu mwenye ndimi mbili katika jambo moja.
Hizi ni baadhi tuu ya sifa chache nilizoziona kwa ndugu huyu mabazo kwakweli pamoja na nyingine nyingi nimeshawishika na kuamini kuwa anaweza kuiongoza CHADEMA kwa mafanikio makubwa.
Naomba maoni yenu