Maoni yangu Wizara ya Afya; Haya mambo yatungiwe sheria na nchi nzima kila hospitali zote zizingatie

naunga mkono hoja, kuuguza inahitaji moyo, hasa mgonjwa asiejiweza, ... vyoo vya kukaa ni muhimu
 
Wazo zuri,tatizo hivyo vyoo kama havitunzwi vizuri ni njia mojawapo ya kuambukizana magonjwa. Utakuta hosp nyingi maji ni shida sana na usafi ni haba
 
Good suggestion
 
Wazo zuri,tatizo hivyo vyoo kama havitunzwi vizuri ni njia mojawapo ya kuambukizana magonjwa. Utakuta hosp nyingi maji ni shida sana na usafi ni haba
Yaani kutilia mashaka usafi wa vyoo katika kituo cha afya ni sawa na kutilisha shaka ulinzi ulinzi katika kituo cha polisi!

Haiwezekani kikaendelea kuitwa kituo cha afya kama watakuwa wachafu
 
Hilo mbona ni Swala liko ndani ya uwezo wa Incharge wa Hospitali au halmashauri aliyopo.

Ni hali ya usafi tu na kujali afya. Lakini kwa viongozi hawa hawa naoona mimi wacha ikae hivyo hivyo.
 
Ukiuguza ndio utajua umuhimu wa hivi vyoo vya kukaa.

Ila pia katika kuboresha, wizara inaweza ku-design vitu kama removable-plastic-casing ambavyo unaweka juu ya choo kabla ya kukaa.

Ikiwa mgonjwa anakuwa na uhitaji anapewa. Ili kupunguza ile interaction ya wagonjwa wengi kukalia choo kimoja kwa wakati huo kabla ya raundi ya usafi kufika.

Hizi removable-plastic-casing zinaweza fanyiwa usafi na ndugu wa mgonjwa mpaka pale mgonjwa atakaporuhusiwa kutoka hospitali na kuzikabidhi tena kwa wahusika.
 
Wazo zuri
 
Wazo zuri sana hili.
 
Imagine mjamzito na tumbo lake kubwaaa akachuchumae mara miguu imekaza anashindwa kunyanyuka. Au mtu katoka kufanyiwa operation. Hua hosptal nyingine kuna choo cha ladies, gents na wasiojiweza i.e. walemavu. Hosptal nyingine unakuta hamna hata choo cha special needs, ni changamoto mno.
 
Jibu zuri sana, ila wakati wanajenga hizo hospitali wanapaswa kuyaangalia haya toka mwanzo na siyo kujenga ili mradi tu...
 
Kabisa ndiyo maana wajawazito hukojoa kama ng'ombe sometimes bila kuchuchumaa
 
Wazo zuri lakini kwa sasa wajenge hivyo vyoo vya kukaa inchi nzima! Hospital isipewe kibali kama vyoo bora haina!
Mkuu boy kwaajili ya PSN sio unajengajenga tu, vinahutaji design na standards zake.... ni watu wakae chini waangalie uhitaji maalum wa watu mfno wenye ulemavu Kuna design zake za vyoo... so sio swala la kukurupuka tu
 
Jibu zuri sana, ila wakati wanajenga hizo hospitali wanapaswa kuyaangalia haya toka mwanzo na siyo kujenga ili mradi tu...
Kujenga sio ishu, ishu ni ku manage, swala mfano waste water management, sanitation, na water treatment vinahitaji ufatiliaji wa karibu sana
 
Kujenga sio ishu, ishu ni ku manage, swala mfano waste water management, sanitation, na water treatment vinahitaji ufatiliaji wa karibu sana
Hayo mambo ya usafi hospitalini zizani kama wanaweza kushindwa! Cha mhimu viwepo!
 
Vyoo vya kukaa kwa hospitali zetu wala sishauri. Tutaandaa viwanda vya maradhi sugu!
Kuna hospitali moja nimetoka juzi... choo si cha kukaa lakini wameandaa mazingira kiasi kwamba mtu yeyote anaweza kukitumia bila shida yoyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…