Maoni yangu ya kisomi kuhusu mabango ya Yanga

Maoni yangu ya kisomi kuhusu mabango ya Yanga

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Nitaelezea kwa ufupi sana maoni yangu ya kisomi kuhusiana na ishu ya mabango ya Yanga yanayoonyesha matokeo ya mechi yake na Simba yaliyopachikwa maeneo mabalimbali Dar es Salaam.

Upande mmoja wamekuja na hoja kuwa walichofanya Yanga ni kuchukua maudhui kutoka Azam TV na walichofanya ni kuyasambaza tu kama yalivyo. Tukumbuke kuwa AzamTV hawawezi kusambaza maudhui ambayo katika graphics wanaorodhesha wadhamini wote wa Yanga. Ile ni graphics iliyotengenezwa na Yanga kwa madhumuni yao wenyewe. Unataka kuniambia Azam waliweka 1 ndogo na 5 kubwaaa kama lile bango linavyoonyesha? Ukiwaambia Yanga watoe uthibitisho wa video ya Azam waliyotoa kile kinachoonekana katika lile bango hawawezi kukuonyesha.

Ukitumia hoja ya haki ya timu kusambaza habari na matokeo yake kama ambavyo timu zimekuwa zinafanya kwenye mitandao ya kijamii, swali linaweza kuja, ni lini Yanga wamekuwa na utaratibu wa kutangaza matokeo ya mechi zao kwa njia ya mabango? Tukipata mifano mingine sawa, kama hakuna kesi inaendelea. Nina uhakika mikataba ya Azam na vilabu vyote inaonyesha ni maeneo na jinsi gani timu zote zinaweza kutumia maudhui ya ligi bila kuathiri haki za timu pinzani.

Hili suala linarudi hadi katika ile makala ya mwisho wa msimu uliopita, sidhani kama Yanga walifuata taratibu zote stahiki kutumia maudhui yote kutoka kwa wahusika wote ikiwemo Simba. Tukiamua kufukua makaburi, hata kwenye ile makala ambayo mpaka leo inaingiza pesa AZAM TV, Simba wanaweza kulipwa fidia.

Kama tumetoka kupiga kelele wale wanaotengeneza jezi feki bila idhini ya wahusika, hili tukiliacha lipite, kesho au keshokutwa kuna watu watatengeneza vyupi wataweka nembo ya mpinzani wake na matokeo yao halafu watasema wametoa Azam TV.
 
Simba kinachowauma ni logo Yao kutumika au 5 Yao kutumika??

Maana mshaambiwa vyote hivyo ni vyenu

Ndo akil zko zilipoishia

Nenda kawe mwanasheria wa Simba mchukue toyo na Mangungo muende kisutu, kwani pamefungwa?
Yanga siku zote nawaambia huwa mna mitazamo ya muda mfupi inayoendeshwa na mihemko. Hamfikirii lile mnalolitetea au kilipinga leo kesho linaweza kuwadhuru hata nyie wenyewe. Mnaendeshwa kama hamnazo.
 
Yanga siku zote nawaambia huwa mna mitazamo ya muda mfupi inayoendeshwa na mihemko. Hamfikirii lile mnalolitetea au kilipinga leo kesho linaweza kuwadhuru hata nyie wenyewe. Mnaendeshwa kama hamnazo.

Kwamba unatushauri unatupenda? Sisi tuna enjoy lile bado hata ikipaswa tulipe fidia hakuna shida, yale matokeo yapo kila mahali, hata kwenye simu yako yapo, ni public results. Uache u bush lawyer wako
 
Hauzuiwi kusambaza maudhui ila unaambiwa fuata taratibu. Ndiyo maana hata watu wa online TV wanaweza kuhoji mashabiki baada ya mechi ila hauoni wakitumia video za Azam katika maudhui yao. Unadhani Yanga wanaweza kuchukua maudhui ya mechi ya Mtibwa vs Namungo na kuyasambaza kisa tu yapo kila mahali?
 
Yanga siku zote nawaambia huwa mna mitazamo ya muda mfupi inayoendeshwa na mihemko. Hamfikirii lile mnalolitetea au kilipinga leo kesho linaweza kuwadhuru hata nyie wenyewe. Mnaendeshwa kama hamnazo.
Kwani kinakuuma nin?
 
Nitaelezea kwa ufupi sana maoni yangu ya kisomi kuhusiana na ishu ya mabango ya Yanga yanayoonyesha matokeo ya mechi yake na Simba yaliyopachikwa maeneo mabalimbali Dar es Salaam.
yupi wataweka nembo ya mpinzani wake na matokeo yao halafu watasema wametoa Azam TV.
Poleni sana kwa maumivu makali mnayopitia mpaka sasa.
 
Back
Top Bottom