Maoni yangu ya kisomi kuhusu mabango ya Yanga

Maoni yangu ya kisomi kuhusu mabango ya Yanga

Simba kinachowauma ni logo Yao kutumika au 5 Yao kutumika??

Maana mshaambiwa vyote hivyo ni vyenu
Matokeo ni ya simba na nembo inayoliliwa ni ya simba sasa shida iko wapi,au uchungu wa kolo kushindiliwa tano🤪
 
Mkuu wewe ulitakaje kwani yanga hawajawafunga simba sc goli 5????

Ila 5 kwa Thiiimbaaaa Sim5a zinauma sana.

kwani kinakuuma nin?

zile 5-1 ni kweli mlipigwa au Yanga wanatangaza uongo?? TUANZIE HAPO KWANZA

Matokeo ni ya simba na nembo inayoliliwa ni ya simba sasa shida iko wapi,au uchungu wa kolo kushindiliwa tano🤪
Hauwezi kutumia nembo ya brand ya watu kutaka kuwadhalilisha. Mnatumia kichaka cha "kwani matokeo yaliyowekwa siyo sahihi?", Pilato atawauliza tangu lini mmekuwa na utaratibu wa kutangaza matokeo kwa mabango? Suala hili itaangaliwa "motive" au "nia" nyuma ya tendo husika. Nia ipo wazi kabisa hata jinsi mnavyoongelea suala hili inaonekana.

Tungewafilisi kuku nyie, mshukuru tu mamluki na vikondoo vimejaa kwenye safu ya uongozi pale Simba
 
Nitaelezea kwa ufupi sana maoni yangu ya kisomi kuhusiana na ishu ya mabango ya Yanga yanayoonyesha matokeo ya mechi yake na Simba yaliyopachikwa maeneo mabalimbali Dar es Salaam.

Upande mmoja wamekuja na hoja kuwa walichofanya Yanga ni kuchukua maudhui kutoka Azam TV na walichofanya ni kuyasambaza tu kama yalivyo. Tukumbuke kuwa AzamTV hawawezi kusambaza maudhui ambayo katika graphics wanaorodhesha wadhamini wote wa Yanga. Ile ni graphics iliyotengenezwa na Yanga kwa madhumuni yao wenyewe. Unataka kuniambia Azam waliweka 1 ndogo na 5 kubwaaa kama lile bango linavyoonyesha? Ukiwaambia Yanga watoe uthibitisho wa video ya Azam waliyotoa kile kinachoonekana katika lile bango hawawezi kukuonyesha.

Ukitumia hoja ya haki ya timu kusambaza habari na matokeo yake kama ambavyo timu zimekuwa zinafanya kwenye mitandao ya kijamii, swali linaweza kuja, ni lini Yanga wamekuwa na utaratibu wa kutangaza matokeo ya mechi zao kwa njia ya mabango? Tukipata mifano mingine sawa, kama hakuna kesi inaendelea. Nina uhakika mikataba ya Azam na vilabu vyote inaonyesha ni maeneo na jinsi gani timu zote zinaweza kutumia maudhui ya ligi bila kuathiri haki za timu pinzani.

Hili suala linarudi hadi katika ile makala ya mwisho wa msimu uliopita, sidhani kama Yanga walifuata taratibu zote stahiki kutumia maudhui yote kutoka kwa wahusika wote ikiwemo Simba. Tukiamua kufukua makaburi, hata kwenye ile makala ambayo mpaka leo inaingiza pesa AZAM TV, Simba wanaweza kulipwa fidia.

Kama tumetoka kupiga kelele wale wanaotengeneza jezi feki bila idhini ya wahusika, hili tukiliacha lipite, kesho au keshokutwa kuna watu watatengeneza vyupi wataweka nembo ya mpinzani wake na matokeo yao halafu watasema wametoa Azam TV.
Unajiumiza bure hili ungeliacha tu lipite.
 
Adui yako mkubwa unapomshinda utasheherekea. Duniani hapa yanga hana adui yeyote isipokuwa tu simba. Simba ni adui namba moja wa yanga, na anapomtesa hufurahi.

Ulitaka yanga afurahi kumfunga al Ahly au Mamelodi kuliko kumfumua simba?

Simba ni adui no moja wa yanga, na itakua hivyo milele.
 
Yanga siku zote nawaambia huwa mna mitazamo ya muda mfupi inayoendeshwa na mihemko. Hamfikirii lile mnalolitetea au kilipinga leo kesho linaweza kuwadhuru hata nyie wenyewe. Mnaendeshwa kama hamnazo.
Mkuu nadhani ingekua busara zaidi ungetumia maono yako makini kwa ajili ya maslahi yako binafsi na kama itawezekana kwa ajili ya chama lako pendwa la msimbazi. Naamini wewe na familia yako mtafaidika pamoja na chama lako
 
Ila kweli yanga tumebugi

Maana wao ndo walikuwa wenyeji wetu mchezo ulikuwa wa kwao wakalipwa wao, wakala 5 zao

Tulipaswa kuwaomba kutundika hayo mabango ila tunafanya kuwakera tu wakereke weeeee wapigane

Maana wamefarakana hakuna yeyote wa kwenda Mahakamani akienda watambana fedha badala ya kusajiri uanze kusumbuka na kesi , unaanza kesi mara puuu asec hawahapa wanakuchapa 5 mzuka [emoji2][emoji2][emoji2]
 
Yanga ni timu fulani ya kiswahili sana, yani malengo yao makubwa ni kuifunga Simba.
Yani kuifunga Simba ( Club kubwa) imekua nongwa ivo? Hawa jamaa ni amateur
 
Fungueni mashtaka wanaouza cover za simu zenye nembo ya Simba bila makubaliano.
Na huyu wa vikombe faini 100M
FB_IMG_1700151135726.jpg
 
Yanga siku zote nawaambia huwa mna mitazamo ya muda mfupi inayoendeshwa na mihemko. Hamfikirii lile mnalolitetea au kilipinga leo kesho linaweza kuwadhuru hata nyie wenyewe. Mnaendeshwa kama hamnazo.
Ninyi mulionazo mangungu akawaletea manzoki kwenye uchaguzi na kwa usmart wenu mukampigia kura kwa ajili hiyo
 
Hauwezi kutumia nembo ya brand ya watu kutaka kuwadhalilisha. Mnatumia kichaka cha "kwani matokeo yaliyowekwa siyo sahihi?", Pilato atawauliza tangu lini mmekuwa na utaratibu wa kutangaza matokeo kwa mabango? Suala hili itaangaliwa "motive" au "nia" nyuma ya tendo husika. Nia ipo wazi kabisa hata jinsi mnavyoongelea suala hili inaonekana.

Tungewafilisi kuku nyie, mshukuru tu mamluki na vikondoo vimejaa kwenye safu ya uongozi pale Simba
Dunia haiishi vituko eti wewe nawe uifilisi yanga
 
Back
Top Bottom