Maonyesho ya Ubunifu UDSM yanafikirisha

Hatutaki cha kwenda mwezini tunataka hata cha kwenda tu hapo goba tofauti na gari na bodaboda
 
Hilo sanamu la bati linatembea au lipo tuu km la fundi maiko
Linatembea mkuu sema likikutana na mtu linatukana matusi ya nguoni linakutukania hadi bibi yako...ndo prof bado hajajua kwanini linafanya hivyo anaomba msaada kwa pm
 
Aibu sana. Na mabox yao huko uwanjani hakuna jipya. Kuna wakati mpaka madawati ya kukalia wanafunzi ni shida hadi mitihani inafanyika cafeteria. Yaani costec inawazidi. Wala sipotezi muda wangu kwenda huko.
 
Nenda kariakoo mtaa wa makamba/Swahili uone vijana watakutengenezea hadi chyup ya chuma na unaivaa hapohapo
Kwahiyo haya ndio maajabu uliyomaanisha kumbe kazi ipo.
 
Engineer anapigania kubuni mashine ya kufyatulia tofali
Nadhani umeongea kwa dharau sana. Imagine akatokea muhandisi akatengeneza mashine inayotengeneza tofali kwa mchanganyiko wa simenti kidogo na udongo wa kawaida na likawa imara kuliko la simenti na mchanga, na gharama yake ikawa ni Tsh 100 kwa tofali, unadhani linapaswa kudharauliwa kwa sababu tu "Engineer anapigania kubuni mashine ya kufyatulia tofali?"

Kuna haja ya kuwakosoa wakosoaji, maana naona kila mtu anarusha mawe alimradi amekosoa!
 
Hivi Mo aliongea nn? Maana kama Bilionea aliliona Hilo sanamu la mabati na hakushangaa itasikitisha sana
 
Prof naona jiwe limekupata kisawasawa na kitambi chako full madesa.
 
Mkuu mwache aseme ukweli. Pale Coet kweli wanashindwa kutengeneza viti na meza za chuo mpaka wampe mkandarasi wa keko alete pale. Hebu waanze kutatua matatizo yao. Hayo maungo ya aluminium wanazunguka nayo kila maonyesho hakuna jipya.
Kwani nini kinashindikana kupitia Tafiti kibao walizonazo wafanye vitu vya maana? Kuna shida ipo mahali.
 
Kuna jamaa wa Nigeria yeye anatengeza maumbo mbalimbali kwa tairi chakavu za magari...nahisi jamaa ni mbunifu kuliko hao wazee wa bati...ingawa jamaa hana elimu ya darasani
Hana elimu ya darasani hakupelekwa shule ??
 
Angekosoa kama ulivyofanya isingekuwa shida. Ukikosoa kwa kuonyesha udhaifu ni jambo jema kuwasaidia wahusika kujirekebisha. Ila ile blanket statement haifai!
 
24 May 2021
Dar es Salaam, Tanzania

MAPEMA LEO:WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA MABANDA NA KUFUNGUA MAONESHO YA 6 YA UBUNIFU NA UTAFITI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM


Source : mlimani tv UDSM
Nimesikia kama waziri kauliza kutengenezewa sanamu kama hilo litacost sh ngapi , yule mama kajibu milioni 10, watu waka cheka , au nimesikia vibaya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…