Mapato sherehe ya Mavuno Jimbo Katoliki Dar ni Tsh. Bil. 4.5

Mapato sherehe ya Mavuno Jimbo Katoliki Dar ni Tsh. Bil. 4.5

Kitu hukijui unauliza.

Utaratibu wa Kanisa kuna asilimia ndogo hutolewa kupelekwa Vatican kwa ajili ya kusaidia Kanisa kwenye majimbo maskini ya nchi mbalimbali duniani kiasi kinachosalia kinabaki ndani ya jimbo kwa ajili hiyo hiyo kusaidia Parokia zisizoweza kisadaka,mf:Jimbo la dsm linasimamia Parokia za kibiti na Mafia huko waumini ni maskini ukiwaambia watoe michango kujenga Kanisa kubwa au hospital hawawezi so wanasaidiwa na Parokia zinazojiweza.

By the way,kuna 100K yangu humo ktk jumuia yangu yupo mtu alitoa 1.5mill na hawajiulizi maswali mengi.
Wanaolalamika ni njaa zinawasumbua tu.
 
daaa pesa ndefu sana hii na asilimia 50 imetoka kwenye mikono ya maskini ambao hawana uhakika wa msosi this is called new theft and robbery

hii imenikumbusha kitabu cha DEVIL ON THE CROSS by ngugi wa thiongo
Wakatoliki hawana njaa kiasi hicho
 
Kile kitendo Cha kuwatenga kuanzia kwenye jumuiya na zaidi ya bunduki. Nilishashuhudia mara kibao mnakataa kufanya ibada kwenye misiba kisa aliekufa alikuwa hotoi michango
Sasa kama mtu hakuwa mshiriki kwa nini uangaike naye? Hiyo itatoa fursa kwa waliobaki kutoshiriki shughuli za kanisa kwa imani kuwa kanisa litawazika
 
Wajinga ndio......
Na waliochanga wataendelea kuwa maskini, limbukeni, fukara na kuendelea kutapeliwa kiroho![emoji1787][emoji23][emoji28]
Tenga muda uende kanisa la katoliki jumapili kuona watu wanavyopendeza na sura zenye nuru huku parking zikiwa hazitoshi afu uje ufute kauli yako hapa
 
Mkuu kinyume chake Vatican huwa inatuma hela kila nchi bajeti ikipelea .mm nimesoma Consolata seminary nlikuwa najiuliza hivi kwa nn tunalipa laki mbili kwa mwaka wakati hara Private ya kipuuzi zinalipa 1m kwa mwaka .nkaja ona bajeti yaani 80% hela inatoka kwa wafadhil wakatoliki wa italy na ndo maana hata uende kijijini maskini vipi utakuta kanisa katoliki ni viwango vya maana
Well organized.
 
Ndio mkuu yaani kanisa ni kama shamba unakuwa unavuna tu kila siku!
Hata mimi huwa nawaza huko mbeleni biashara yangu ya majeneza ikinishinda ntaanzisha kanisa najifanya nabii niliyeshukiwa na roho mtakatifu akanambia niachane na biashara ya majeneza nieneze injili na kukusanya kondoo waliopotea
Kama unaona jambo jepesi fanya kanisa katoliki ni taasisi imara usifananishe na manabii uchwara
 
Ulipaoandika ndugu zetu upande wa pili ni kama umetupa jiwe kule kuwa hawana system nzuri ya kukusanya mapato kwa waumini wao. Anyway, nyie wakatoliki huo mtindo wenu wa kukusanya mapato na wengine wanaufanya japo wana waumini kidogo kuliko ninyi. Kuna walutheri, waanglicani, wapentekoste na wale wote wenye mfumo wa majimbo ya kanisa kama ninyi. Basi tuwape hongereni kwa kufundisha waumini wenu moyo wa utoaji
 
Tatizo linapokuja ishu ya kanisa mnabase kwenye sadaka means mema mengi yanayofanywa na kanisa katoliki hamuyaoni kabisa.
Huna cha kunidanganya, Mimi ni Mkatoliki, wala sina mpango wa kuhama lakini msimamo wangu dini zote ni Utapeli na biashara za watu.

Labda usichokijuwa tu wengi bado tupo kwenye imani za dini kwa sababu za kijamii na kifamilia tu, lakini Utapeli wa dini zote uko dhahiri ukiamuwa kutumia akili yako vizuri.
 
Back
Top Bottom