Mapato sherehe ya Mavuno Jimbo Katoliki Dar ni Tsh. Bil. 4.5

Mapato sherehe ya Mavuno Jimbo Katoliki Dar ni Tsh. Bil. 4.5

Ni kweli kanisa katoliki linatumia Sadaka kujenga shule nyingi sana zenye majina makubwa

Mfano St francis mbeya

Marian bagamoyo

St joseph dar es salaam

Swali kubwa ni JE KWENYE HIZO SHULE ZA KATOLIKI WATOTO WA WAUMINI WALIOTOA SADAKA KUZIJENGA HUWA WANASOMESHWA BURE ? WANAPEWA DISCOUNT YA ADA AMA WANALIPA SAWA SAWA NA WATOTO WA DINI ZINGINE..

MFANO WAISLAM WANAOSOMA ST FRANCIS WANALIPA ADA KIASI TOFAUTI NA WAKATOLIKI WANAOSOMA ST FRANCIS AMA WOTE ADA NI SAWA ?
Hakuna kitu kama hicho, Hela lzm utoe, ingewezekana kufanya hivyo ulivyoshauri wanaochangia wangeneemeka.
 
Hongera wana Jimbo, hongera kanisa moja la mitume.

Kumbuka haya ni mapato ya sherehe ya mavuno tu, na ni kwa jimbo moja tu.

View attachment 2833300
Ukijumlisha vyanzo vingine vya mapato mfano:
1. Tegemeza jimbo
2. Miito mitakatifu
3. Sadaka za kawaida
4 mchango wa pili
5. Bahasha za Noeli/Pasaka
6.
7.
8.
9.

Kisha kadiria kwa Nchi nzima. Nadhani utakubaliana na mimi ukubwa wa hii taasisi.

Ni tofauti kabisa na "ndugu zetu wa upande wa pili". Heko kanisa, heko watoaji.

PS
Sijajua matumizi ya hizo pesa maana kama kuna ujenzi basi itaanzishwa account ya kuchangia.
🤣🤣 Tuliosoma Cuba tumeelewa hii ni SARCASM. Kiukweli bado uislamu itazidi kuwa imani bora zaidi. Ina mapungufu machache sana.... wakristo kwenye maokoto tumetekwa mno na shetani. Sasa sadaka zote hizo si ni utapeli mtupu? Hiyo bahasha ya noeli ya kazi gani?
 
MKIAMBIWA TOZO KWA AJILI YA KUJENGA SHULE MNAMTUKANA MWIGULU ILA TOZO ZA KANISANI MNASHANGILIA, HALAFU MISHULE WANAYOENDA WATOTO WENU KAMA MAGOFU YA AMBONI.
MNAJENGA MAKANISA ILA KUBORESHA SHULE ZENU HAMTAKI.
3/4 YA SHULE TZ NI MBAYA MNO, ILA JAMII HAINA MUDA WALA HAIJALI
KWELI MWAFRIKA ANA IQ YA 80.
 
Jimbo la dsm linasimamia Parokia za kibiti na Mafia huko waumini ni maskini ukiwaambia watoe michango kujenga Kanisa kubwa au hospital hawawezi so wanasaidiwa na Parokia zinazojiweza.

By the way,kuna 100K yangu humo ktk jumuia yangu yupo mtu alitoa 1.5mill na hawajiulizi maswali mengi.
Umeweka vizuri mkuu, nami kwangu kuna aliyetoa 2.5m+.
Ambayo ni sawa na mwingine akienda kunywa bia za kutosha, wengine mchango wa harusi ya saa chache ni laki 5. Acha maisha yaendelee jinsi kila mtu anavyoona inafaa.
 
Mbona mnaombea wafu, mnauhakika wanawasikia..?
Siyo tunawaombea tu,hata wao huko walipo wanatuombea sisi huku duniani,hata wewe nduguzo unaokataa kuwaombea hawachoki kukuombea,nenda kasome Luka 16:31 itafakari kwa kina uje na jibu hapa au naweka nukuu kwa wale watakaoshindwa kuifikia kwa wakati,nitaanzia mstari wa 22

22 “Hatimaye,yule maskini alikufa.Malaika wakamchukua akakae pamoja na Ibrahimu mbinguni.Yule tajiri naye pia akafa, akazikwa.23
Alipokuwa kuzimuni ambapo alikuwa akiteseka,alita zama juu, akamwona Ibrahimu kwa mbali na Lazaro karibu yake.24 Akaita,‘Baba Ibrahimu, nionee huruma umtume Lazaro achovye japo ncha ya kidole chake katika maji aupoze ulimi wangu maana ninateseka kwenye moto huu.25 Lakini Ibrahimu akamjibu,‘Mwanangu,kumbuka kwamba ulipokuwa hai ulipata kila kitu kizuri uli chotaka,ambapo Lazaro alipokea mabaya. Lakini sasa anafarijika hapa na wewe unateseka.26 Isitoshe, kati yetu na ninyi huko, kumewekwa bonde kubwa lisilopitika ili wale wanaotaka kutoka huku kuja huko au kutoka huko kuja huku wasiweze.’ 27 Akasema, ‘Basi, baba, tafadhali umtume Lazaro aende nyumbani kwa baba yangu, 28 awaonye ndugu zangu, wasije wao pia wakaletwa mahali hapa pa mateso watakapokufa.’ 29 Ibrahimu akamjibu, ‘Ndugu zako wanazo sheria za Musa na maandiko ya Manabii. Itawapasa watii hayo.’ Lakini yule tajiri akazidi kumsihi, 30 ‘Hapana baba Ibrahimu, ndugu zangu hawatashawishiwa na hayo. Lakini mtu kutoka kuzimu akitumwa kwao watatubu na kuziacha dhambi zao.’

31 “Ibrahimu akamwambia, ‘Wasiposikiliza na kutii sheria za Musa na Maandiko ya manabii, hawatashawishika kutubu hata kama mtu akifufuka kutoka kuzimu.”’


Soma kwa tafakuri humo nilimo-bold maandishi makubwa hasa mstari wa 30 utajua kwamba kwanini wewe lazima uwaombee ndugu zako waliokutangulia,assume leo ufe ufike huko ukute mazingira mabaya utataka mkeo au mama yako uliyempenda sana nae afike huko?utakapopata nafasi ya kusema kitu unadhani utaacha kuomba juu yao?Kanisa Katoliki halifanyi kitu nje ya maandiko matakatifu tambua hilo.
 
Hapo zinapelekwa vatican wazungu wakajengee ma fly over na maendeleo mengine kwenye nchi zao.

Dini walizotuletea ni biashara nzuri sana ambayo wazungu wanaifanya. .
Mkuu kinyume chake Vatican huwa inatuma hela kila nchi bajeti ikipelea .mm nimesoma Consolata seminary nlikuwa najiuliza hivi kwa nn tunalipa laki mbili kwa mwaka wakati hara Private ya kipuuzi zinalipa 1m kwa mwaka .nkaja ona bajeti yaani 80% hela inatoka kwa wafadhil wakatoliki wa italy na ndo maana hata uende kijijini maskini vipi utakuta kanisa katoliki ni viwango vya maana
 
Hongera wana Jimbo, hongera kanisa moja la mitume.

Kumbuka haya ni mapato ya sherehe ya mavuno tu, na ni kwa jimbo moja tu.

View attachment 2833300
Ukijumlisha vyanzo vingine vya mapato mfano:
1. Tegemeza jimbo
2. Miito mitakatifu
3. Sadaka za kawaida
4 mchango wa pili
5. Bahasha za Noeli/Pasaka
6.
7.
8.
9.

Kisha kadiria kwa Nchi nzima. Nadhani utakubaliana na mimi ukubwa wa hii taasisi.

Ni tofauti kabisa na "ndugu zetu wa upande wa pili". Heko kanisa, heko watoaji.

PS
Sijajua matumizi ya hizo pesa maana kama kuna ujenzi basi itaanzishwa account ya kuchangia.
Duh.!
Kwa hali hii acha watu waanzishe makanisa tu
 
Mavuno neno tamu sana hili yaani wamevuna
Ndio mkuu yaani kanisa ni kama shamba unakuwa unavuna tu kila siku!
Hata mimi huwa nawaza huko mbeleni biashara yangu ya majeneza ikinishinda ntaanzisha kanisa najifanya nabii niliyeshukiwa na roho mtakatifu akanambia niachane na biashara ya majeneza nieneze injili na kukusanya kondoo waliopotea
 
Back
Top Bottom