Mapigano yanayoendelea Gaza na unafiki wa Dunia

Mapigano yanayoendelea Gaza na unafiki wa Dunia

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Duniani kote kila Bara kuna mapigano yanayoendelea huku kukiwa na ushawishi sifuri kwenye kusitisha hizo vita. Ninasema mapigano kwa sababu sehemu kubwa ya mapambano hayo yametokana na ushawishi wa makundi yanayolenga kufaidika na vita hizo. Kinachoendelea Ukraine na Urusi ni vita kamili kwa sababu pande zote wanaumizana na kila upande una uwezo wa kujibu mashambulizi ya kutoka upande hasimu. Anayelaumiwa hapo ni Urusi

pale Gaza, kinachoendelea siyo vita (kwa tafsiri yangu), bali ni mauaji ya halaiki ambayo yanadhaminiwa na Umoja wa Ulaya na Marekani kuisaidia Israel kuua watoto, wanawake na watu wa taifa la Palestina. Kwa nini nasema ni mauaji ya halaiki, ni kwamba Israel inatumia zana zote za kivita dhidi ya taifa ambalo kimsingi halijaingiza jeshi lake vitani. Hakuna zana wala kifaa chochote za kivita cha Taifa la Palestina zilizoingizwa vitani. Hakuna jeshi la Palestina lililopo mstari wa mbele kulinda mipaka yao ambayo inaingiliwa bila huruma na Israel. mauaji yanayoendelea yamejengwa kwenye dhana ya kupambana na ugaidi ambapo hata watoto na wanawake ambao kimsingi ni vulnurables kuwa wanawaficha magaidi. Ukiangalia ndani zaidi majuzi hapa Wafanyakazi wapatao 7 wa World Kitchen Centre wameuawa kwa kulengwa na vikosi vya Israel. Shirika hilo lenye makao yake makuu Marekani ndilo pekee lililosalia Gaza kutoa msaada wa kibinadamu ya chakula na maji safi. Hilo linajiri kwa sababu Israel imefunga mipaka ya kila kona kuzuia misaada ya kibinadamu kuwafikia Wapalestina waliokusanywa eneo la Kaskazini. Humu kwenye mitandao wamejaa washabiki wa kila namna bila kutafakari madhara na madhila yatokanayo na hizi tabia za kuuana kwa kujitetea kulinda utu na ustawi wa wauaji. Lakini anayelaumiwa kwenye mauaji haya ni Palestina

Afrika kuna mapigano karibia eneo kubwa la Bara hili, huku viongozi wa nchi za bara hili yaani zinazounda Umoja wa Afrika wakiendelea kujimwambafai pale Addis Ababa kwa robusta na aina kede za kahawa zinazopatikana mjini hapo. Karibia viongozi wote wapo handicapped kifikra kwa kuweka matumaini makubwa kwa nchi zilizoendelea hususan mataifa yanayotengeneza na kusambaza kwa wingi silaha na zana za mauaji duniani. Sisi Tanzania tumepeleka vikosi vya kulinda amani kwenye mataifa hayo na tunachoambulia ni kuwazika vijana wetu wanaouawa kwenye conflicts hizo zisizo na kichwa wala miguu.

Tutafakari haya

  1. DRC mapigano yanayoendelea, kwa nini hakuna juhudi za kumaliza mapambano yale? Kwa nini wanaouawa ni raia ambao siyo wahusika wa tofauti za kusaka madaraka baina ya makundi yanayopigana?
  2. Juba, mapigano yanayoendelea baina ya vikosi vya Serikali inayoongozwa na Salva Kiir na vikosi vya aliyekuwa makamu wake Riek Machari, mapigano hayo yanasababisha wakimbizi na mauaji ya kutisha kwa wananchi ambao kimsingi siyo sehemu ya ugomvi huo. Je nini kinafanyika kumaliza vita hiyo?
  3. Sudan Kaskazini, vita ni kubwa baina ya vikosi vya serikali na majenerali waliojitenga. wote wanasaka madaraka kuwaongoza watu ambao wanawaua kila kukicha kwa silaha zao... Nani wa kuzuia haya mauaji yasiendelee?
  4. Somalia bado ipo kwenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe
  5. Msumbiji imerudi kwenye kupigana vita vya msituni kutokana na vikundi vya kigaidi kujiimarisha Kaskazini mwa nchi hiyo. Eneo la Cabo Delgado siyo salama kwa raia kuishi kwa sababu wanachinjwa na kutishiwa usalama wao kila kukicha. Matukio hayo yanafanyika jirani na mpaka wa Tanzania na baadhi ya matukio yamejiri ndani ya ardhi ya Tanzania....
  6. Uganda, hakujatulia mapambano ya msituni yanaendelea
  7. Afrika Kaskazini ipo katika hekaheka ya mapambano ya msituni ndani ya nchi nyingi za mataifa ya eneo hilo.
  8. Syria, imekuwa vitani hususan dhidi ya mataifa yanayoongozwa na Marekani wakimpinga rais wa nchi hiyo, na kusababisha maafa makubwa ndani ya taifa hilo.
  9. Yemen, imekuwa katika vita inayopewa chapuo na mataifa makubwa ikiwemo Marekani
  10. Libya, ipo ndani ya Afrika lakini Mataifa makubwa chini ya kibali cha Umoja wa Mataifa yalienda kuua raia ili kumng'oa Gadaffi maradakani na hatimaye kumuua. na mpaka leo hakujatulia....
  11. Mifano ni mingi sana nsana.
Sasa tujiulize:
  1. Sisi Watanzania, tunapata wapi ujasiri wa kushabikia hizi vita zinazopiganwa duniani?
  2. Je, kwa sababu tunaishi kwa amani, tunayachukuliaje maisha ya Watoto na wanawake kwenye maeneo ya vita?
  3. Taifa letu, linapowapeleka vijana wetu kulinda amani kwenye maeneo ya vita, Ni amani ipi inayolindwa ikiwa hakuna upokonyaji wa silaha kwa mahasimu wa vita?
  4. Tunafaidika nini na ukimya ama kuchukua pande baina ya mahasimu wa kila vita?
  5. Taifa limejiandaaje ama linawaandaaje watu wake hususani kukabiliana na changamoto za Vita zinazopiganwa karibu na mipaka yetu?
  6. DO WE CARE?
 
Unafiki mwingine ulimwengu mzima wa kiislamu hamlaani hamas waliobaka , kuua watoto wa israel, walioteka wayahudi, walioua watanzania wawili wasio na hatia , waliorusha maroketi israel bali mliwashabikia israel imepatikana sasahivi israel inajilinda tunaona kelele kwa israel
 
Mtoa mada analeta porojo, kwamba Gaza ndiyo ionekane kuwa kuna uonevu kuliko Ukraine wala Sudan...Sema nduguzetu wa Gaza wanapenda sana kutembeza watoto mitaani badala ya kufanya mazishi, Ukraine ingeonesha mili ya watu waliouwawa barabarani kama Gaza wenda dunia wangewaonea huruma.
 
Kwani hamas wanaendelea kushikilia mateka ulitegemea nini na hamas wanaporusha maroketi yao ulitegemea uje utafute huruma huku kupitia watoto na wanawake wa gaza
Yaani Israel ingevamia Palestine kama Russia walivyoivamia Ukraine kwa msafara ule bila ata Ukraine kurusha ata jiwe Russia....ila sasa watu wanailaumu Israel waliokwenda kuokoa watu wake walioteka na wengine kuuwawa ndani ya ardhi yake.
 
Unafiki mwingine ulimwengu mzima wa kiislamu hamlaani hamas waliobaka , kuua watoto wa israel, walioteka wayahudi , walioua watanzania wawili wasio na hatia , waliorusha maroketi israel bali mliwashabikia israel imepatikana sasahivi israel inajilinda tunaona kelele kwa israel
Ukiwa kipofu ukasoma kwa upofu hautaweza kujiona kama responsible humanbeing.

Kwahiyo kama hawajalaaniwa hao magaidi kunatoa haki kwa raia zaidi ya. 30,000 kuuawa kinyama?

Waisrael waliopoteza maisha kwenye shambulio la kigaidi ni 1,200. Je unatamani wafe Wapalestina wangapi kufidia vifo vya waisraeli waliouawa na magaidi wa Hamas?
 
Yaani Israel ingevamia Palestine kama Russia walivyoivamia Ukraine kwa msafara ule bila ata Ukraine kurusha ata jiwe Russia....ila sasa watu wanailaumu Israel waliokwenda kuokoa watu wake walioteka na wengine kuuwawa ndani ya ardhi yake.
Ndugu.
Usikwazike na ujumbe niliouweka. Unaendeleza unafiki ule ule. Katika mauaji yanayoendelea wameweza kuokoa mateka wangapi?

Tusishabikie vita kama kuku wasio na vichwa
 
Unaonaje ujiunge na ukristo, ili Dunia ipige hizo kelele 🤒🤒
Kwa nini Ukristo unauonanisha na vita?

Wayahudi hawana time na hicho unachokiwaza, na sana sana ukijipeleka kule na ukristo wako unarudi kwenye jeneza
 
Kwani hapo tu ndo kuna vita? Mbona sehemu nyingine dunia imekaa kimya?
Nani ni mtu na nani siyo mtu?Je nduguyo akiuawa, ni halali nawe kuua ili kulipa kisasi?

Nani ambaye ana haki ya kuua?
 
Oktoba 7, 2023 mayahudi walitoka kwenda kuivamia Gaza! Uuwe wananchi zaidi ya elfu wasio na hatia halafu wanyamaze! Hivi huwa mnawaza kwa makalio au? Jino kwa jino ndio sera; endeleeni kujitoa ufahamu.
 
Oktoba 7, 2023 mayahudi walitoka kwenda kuivamia Gaza! Uuwe wananchi zaidi ya elfu wasio na hatia halafu wanyamaze! Hivi huwa mnawaza kwa makalio au? Jino kwa jino ndio sera; endeleeni kujitoa ufahamu.
Tatizo ni elimu
 
Ndugu.
Usikwazike na ujumbe niliouweka. Unaendeleza unafiki ule ule. Katika mauaji yanayoendelea wameweza kuokoa mateka wangapi?

Tusishabikie vita kama kuku wasio na vichwa
Mateka wasipoachiwa watazidi kuua zaidi, kwavile Hamas wamekubali kuwa wanazo bado mateka na hawataki kuwaachia hivyo Hamas ndiyo wanaocho haki ya Israel kuendelea na vita ya operation ya kuwasaka mataka wake huku wakiendelea kuua.

Hivi kwanini Hamas hawapati lawama?
 
Back
Top Bottom