Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,428
- 3,937
Hii mada ni ya kiutu uzima kwa hiyo tuweke mzaha pembeni kidogo.
Miaka ile ikitokea kuna mapinduzi ya kijeshi, moja ya sehemu ya kwanza ambapo wafanya mapinduzi walikuwa wanachukua ni radio au television ya taifa. Tukumbuke kuwa kipindi hicho kulikuwa hakuna media binafsi.
Hivi katika dunia ya sasa, ya vyombo vya habari binafsi ambavyo vinafika nchi nzima na hata mitandao ya kijamii ambayo inaonekana dunia nzima, mapinduzi ya kijeshi yamebadilikaje au kuna uwezekano siku za mbele kuona mabadiliko ya jinsi mapinduzi yanavyofanyika?
Kwenye 'Arab Spring' nakumbuka mitandao ilitumika sana kuangusha serikali lakini hili ni jambo tofauti kidogo na ninaloliongelea lakini lina muelekeo huo huo.
Tukumbuke pia kuwa hata uvamizi wa kijeshi umebadilika. Marekani alipovamia Iraq alikuta adui amejipanga tofauti na yeye akasumbuka sana kupigana tofauti na alivyozoea.
Hili mnalionaje? Tulijadili kiutu uzima.