Mapinduzi ya Zanzibar Januari 1964 yalikuwa ni ushindi na neema kubwa kwa Emirate of Dubai

Mapinduzi ya Zanzibar Januari 1964 yalikuwa ni ushindi na neema kubwa kwa Emirate of Dubai

Walitoka Oman, wakavamia Zanzibar, wakapinduliwa na Wazanzibar wakarudi Oman walipotokea.
Kuna swali hapo?
Siyo kweli kabisa. Huijuwi Zanzibar.

Wazanzibari wametokea sehemu nyingi, waliokimbia mapinduzi wapo waomani, wapo washirazi, wapo wachina, wapo wahindi, wapo wa Comoro, wapo wamanyema. Wapo Waajemi, wapo wazaramo, wapo wamatumbi, wapo wapakistan, wapo wasaudi, wapo wabahrain, wapo wa Kuwait, wapo wajawa. Qwapo wahabashi, wapo Wasomali, wapo wa Comoro. Wapo wabajuni, wapo wayemeni.

Wanyamwezi na wasukuma ndiyo usiseme.


Wote hao Wazanzibari.

Kumbuka, Zanzibar kilikuwa kitovu cha biashara Afrika na Asia.

Wazanzubar wsluokimbis mapinduzi wslitapasnnchi nyingu funiani.
 
Syll...
Hiyo picha hapo chini ni ya Mohamed Omari Mkwawa mwanamapinduzi wa ASP.

Mkwawa yeye ndiye alikuwa akiwavusha Wamakonde kutoka Kipumbwi wamevaa kama wavuvi na wakifika Zanzibar wanahifadhiwa tayari wakisubiri siku ifike.

Hawa Wamakonde ndiyo waliua Waarabu wengi sana mashamba.

Picha hii nimempiga ndani ya kwake katika siku zake za mwisho za maisha yake.
Hii si nyumba bali ni banda la kuku.

Alinisikitikia hali yake akasema, ''Mohamed bbada ya mimi kufanya yote yale katika mapinduzi ya Zanzibar leo mimi naishi ndani ya banda la kuku nililosaidiwa na ndugu zangu.''

Haukupita muda mrefu Mzee Mkwawa akafariki.

Sawa mzee wangu.. ila mm nilikuwa nq mbana kwenye andiko lake.... Cjapinga hayo mambo ya mapinduzi... Ila yeye aliweka mambo mengine kuusu kunyanyaswa kwa zanzbar na watu wasio waislam
 
Walitoka Oman, wakavamia Zanzibar, wakapinduliwa na Wazanzibar wakarudi Oman walipotokea.
Kuna swali hapo?
Paki....
Inabidi kwanza uisome historia ya Zanziba kwani nemeona kuwa huijui.
Zanzibar ilivamiwa na Wareno na Wazanzibar wakafunga safari hadi Oman kuomba msaada.

Womani wakaja na wakawatoa Wareno kwa silaha.
 
Siyo kweli kabisa. Huijuwi Zanzibar.

Wazanzibari wametokea sehemu nyingi, waliokimbia mapinduzi wapo waomani, wapo washirazi, wapo wachina, wapo wahindi, wapo wa Comoro, wapo wamanyema. Wapo Waajemi, wapo wazaramo, wapo wamatumbi, wapo wapakistan, wapo wasaudi, wapo wabahrain, wapo wa Kuwait, wapo wajawa. Qwapo wahabashi, wapo Wasomali, wapo wa Comoro. Wapo wabajuni, wapo wayemeni.

Wanyamwezi na wasukuma ndiyo usiseme.


Wote hao Wazanzibari.

Kumbuka, Zanzibar kilikuwa kitovu cha biashara Afrika na Asia.

Wazanzubar wsluokimbis mapinduzi wslitapasnnchi nyingu funiani.
Sehemu zote kuna kila watu, so sehemu yoyote ni ya yeyote
 
Kuandika kitabu au upload video u tube sio ndio solution ya jambo kuwa la kweli au la uongo... Hata mimi naweza ku upload video u tube,kuanza kuisema zanzibar au kuandika kitabu kinachoipond uislam, lakin naweza nikawa muongo na kupotosha
Sasa vipi uniamini zaidi ya link ya kitabu ambacho ni cha utafiti? Mimi mwenyewe ukiniuliza sana ntakwenda humo humo kukopi.


Kwanza soma halafu utaamuwa kama yanakuingia au hayakuingii.

AlhamduliLlah bora mwamba mwenyewe kaja, mimi niulize ya wakimbizi wa Dubai. Kama ilivyo mada.
 
Sasa vioi uniamini zaidi ya link ya kitabu ambacho ni cha utafiti? Mimi mwenyewe ukiniuliza sana ntakwenda humo humo kukopi.


Kwanza soma halafu utaamuwa kama yanakuingia au hayakikuingii.

AlhamduliLlah bora mwamba mwenyewe kaja, mimi niulize ya wakimbizi wa Dubai. Mkana ilivyo mada.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].. haya bana madam
 
Sehemu zote kuna kila watu, so sehemu yoyote ni ya yeyote
Ni vyema umelielewa hilo, siyo kama kwanza ulivyofiri ni ya Waoman peke yao. Unawa/ijuwa serikali iliyopinduliwa (vamiwa) 1964?

Leo utasema Rostam Aziz mgeni Tanzania? Ana generation ya tano au zaidi Tabora na kabla ya hapo ana generation tano au zaidi Zanzibar. Mababu zake ndiyo walikuja na Waoman kuwaondoa Wareno Zanzibar. Wabulushi hao.
 
Historia ya Zanzibar inaonesha wazi kuwa Zanzibar wakati wa mapinduzi ilikuwa ni nchi iliyoendelea sana kielimu na kiuchumi kuliko nchi nyingi duniani.

Mapinduzi ya Zanzibar kisiasa yalizaa pia mapinduzi ya kiuchumi Dubai, yenye neema kubwa sana kwa Dubai. "Kufa kufaana".
Naunga mkono hoja.
Wana bodi, japo tuko kwenye harakati za kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge, kuna swali linanitatiza kuhusu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ambapo majibu yake sahihi, pia yanaweza kuwa ni kiashiria tosha cha mshindi wa urais wa Zanzibar, iwapo uchaguzi utakuwa huru na wa haki.

Swali hili lahusu ukweli haswa kuhusu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, 1964, baada ya kuibuka kwa kitabu kingine kiitwacho "Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru"
View attachment 2077603
kilichoandikwa na Mwanazouni wa Zanzibar, Dr. Harith Ghassany, kama kilivyofanyiwa mapitio na mwandishi Mohamed Said kwenye gazeti la Al-Nuur la leo.

Ghasanny anasema kumbe Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalitekelezwa na askari mamluki wa Kimakonde (Wakata Mkonge) ambao waliongozwa na Mzee Mohamed Omar Mkwawa (Tindo) chini ya Amiri Jeshi wa jeshi la mamluki hao Victor Mkello (RIP). (kumbe amiri jeshi hakuwa Mganda John Okello pekee, bali pia Mkello yumo?!.

Mamluki hao walitumia zana zao za kukatia mkonge, zile sime za makali kuwili, walizisunda kwenye nguo zao za ndani na kusafirishwa kwa mitumbiwi usiku usiku kupitia Kipumbwi. Jee wale mashuhuda wa Mapinduzi yale Matukufu ya Zanzibar, wanayakubali haya?.

Pia mwandishi anamalizia kwa kusema hata mauaji ya Karume, hayakutekelezwa na wapinga Mapinduzi, bali ni miongoni mwa hao hao wanamapinduzi, baada ya kupishana kauli fulani fulani za uendeshaji wa Zanzibar baada ya Mapinduzi.

Nimesoma kitabu cha John Okello kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar,
View attachment 2077618
yeye anasema yake, vitabu kadhaa vya waandishi wazungu wanasema yao, historia tukuka ya Mapinduzi Matukufuya ya Zanzibar nayo nayo inasema kivyake, hivi hakuna any straight line yoyote kuhusu Mapinduzi hayo, ya Zanzibar?.
Jee yalipangwa na nani? Yalitekelezwaje?.
Nini haswa kilichotokea usiku ule wa Januari 11?.
Nani alifanya nini wapi?
Na mwisho tuzungumzie wafaidika wa Mapinduzi hayo Matukufu ya Zanzibar na bila kuwasahau wahanga wa Mapinduzi hayo ambao kwako yatakuwa sio Matukufu, ni kina nani haswa?, na kama kuleta amani na utangamano wa Zanzibar kuhusu Mapinduzi hayo kutahitajika kuundwa kwa Tume ya Ukweli na Upatanisho, "Truth and Reconciliation Commission" ili waliohasimiana kutokana na Mapinduzi hayo, wapatanishwe kwa maslahi mapana ya Zanzibar?.

Majibu ya maswali haya yatasaidia kujua mustakabali wa matokea ya uchaguzi wa Zanzibar kudhirihisha kuwa Wazanzibari ni wamoja, hakuna kundi la walishiriki Mapinduzi ndio wenye uhalali zaidi kuitawala Zanzibar kuliko wasioshiriki, after all kumbe Mapinduzi yenyewe, yametekelezwa na askari mamluki wa Kimakonde, toka mashamba ya mkonge Tanga!.

Pasco
Rejea za Mwandishi huyu kuhusu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
  1. Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Bado Kuna Maswali Bila Majibu -1
  2. Neno "Matukufu" Katika Mapinduzi ya Zanzibar, Lilitoka Wapi, na Yana Utukufu Gani?!,
  3. Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa! Walikimbia Wenyewe - Mzee Sukari
Tarehe kama ya leo 11/01/1964 miaka 60 iliyopita, ndio Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalifanyika!. Alfajiri ya Tarehe 12 Januari, 1964 ilikuwa ni kutangazwa tuu!.

Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Paskali
 
Naunga mkono hoja.


Tarehe kama ya leo 11/01/1964 miaka 60 iliyopita, ndio Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalifanyika!. Alfajiri ya Tarehe 12 Januari, 1964 ilikuwa ni kutangazwa tuu!.

Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Paskali
Sijauona huo utukufu.

au kuporomoka kwa maadili ndiyo utukufu?
 
Ndiyo nikasema "sijauona huo utukufu" na kuuliza "au kuporomoka kwa maadili ndiyo utukufu?"

Kwa mtazamo wangu, anaeyaita hivyo ni poyoyo tu au haelewi maana ya utukufu.

Ulitakaje labda,yani waarabu waendelee kukikalia kisiwa chetu pendwa
 
[emoji2][emoji2][emoji2].. ila toka zaman zanzbar inaziadi ya aslimia 90 ni wa islam, inakuaje waweze kunyanyapaliwa na asilimia ndogo sana ambao sio waislam....
Mkuu hapo sasa unapiga kwenye mshono?😂 Maana hawa mafarisayo huwa wanaamini wao wanachukiwa tu na kunyanyapaliwa bila hata sababu, hata kama wapo 99 katika 100 bado watajiliza yule mmoja anawaonea😂
 
Siyo kweli kabisa. Huijuwi Zanzibar.

Wazanzibari wametokea sehemu nyingi, waliokimbia mapinduzi wapo waomani, wapo washirazi, wapo wachina, wapo wahindi, wapo wa Comoro, wapo wamanyema. Wapo Waajemi, wapo wazaramo, wapo wamatumbi, wapo wapakistan, wapo wasaudi, wapo wabahrain, wapo wa Kuwait, wapo wajawa. Qwapo wahabashi, wapo Wasomali, wapo wa Comoro. Wapo wabajuni, wapo wayemeni.

Wanyamwezi na wasukuma ndiyo usiseme.


Wote hao Wazanzibari.

Kumbuka, Zanzibar kilikuwa kitovu cha biashara Afrika na Asia.

Wazanzubar wsluokimbis mapinduzi wslitapasnnchi nyingu funiani.
Sielewi watu weusi wanakimbiaje mapinduzi ilhali walikataa kurudishwa ndani ya utumwa wa mwarabu, na ndio maana watu weusi walishiriki mapinduzi hayo na waarabu hakuna alieshiriki (historia yote sijaona mahali Mwarabu alishiriki)

Ule ulikuwa ukombozi uliomweka mtu mweusi katika nafasi ya walau kuonekana binadamu maana kabla ya hapo alikuwa daraja la mwisho katika nchi yake ya asili akitanguliwa na mzungu, mhindi, mwarabu kisha yeye
 
Tukiitazama historia ya Dubai au UAE kwa ujumla, Oman, mwambao wote wa Zanzibar na bandari takriban zote za nchi za mashariki ya kati mpaka India na Asia ya mbali,utakuta kulijuwa na mwingiliano mkubwa wa kibiashara kati yao.

Bila shaka ni historia ndefu sana na ya zamani sana, kwa ufupi, leo tutazame mafanikio na neema kubwa iliyowadondokea Dubai na yalipotokea mapinduzi ya Zanzibar 1964.

Wimbi la awali la wakimbizi wa Zanzibar walianza kumiminika Dubai kati ya mwaka 1964 na 1968, Wazanzibari wengine, kwa mujibu wa data za UNHCR qazanzibari waliendelea kwenda kama wakimbizi baina ya mwaka 1967 mpaka 2013.

Katika miaka hiyo wengi wa watu kutoka Afrika Mashariki nzima wakaanza kumiminika kama wakimbizi Wazanzibari. Sheikh Rashid akaunda kamati ya Wazanzibari, katika wale waliofika mwanzo, waamuwe katika "wakimbizi" wanaokuja Dubai ni wepi Wazanzibari wa kweli wanaostahiki ukimbizi wa Zanzibari. AlhamduliLlah kwa kuwa kulikuwa na mwingiliano mkubwa wa watu wa Afrika mashariki wengi wanzangu na mie wasio na asili ya Zanzibari wskajipatia "status ya ukimbizi". Fsmilis. Nyingu za Dar. Tunafahamiana nao ambao wsliibgianjwente mkumbi huo na siku hizi wameshakuwa raia wa UAE kiuhalali kabisa. (kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani.


Kwanini ikawa ni ushindi na neema kwa Dubai? Historia ya Zanzibar inaonesha wazi kuwa Zanzibar wakati wa mapinduzi ilikuwa ni nchi iliyoendelea sana kielimu na kiuchumi kuliko nchi nyingi duniani.

Sheikh Rashid bin Saeed Al Maktoum, ambae ni babu wa Mfalme wa sasa wa Dubai, aliposhauriwa na mshauri wake wa Kiingereza (Duff) kuhusu wakimbizi wa Zanzibar, hakusita kuwakaribisha na kuwapokea kwa nia njema kabisa.

Kwa bahati nzuri kabisa, wakimbizi wengi wa Zanzibar wa wakati huo walikuwa ni wasomi na wataalam wa biashara na siasa za kidunia.

Wasomi na wataalam hao ikawa ni neema kubwa kwa Ufalme wa Dubai. Ufalme wa Dubai ukajipatia washauri, wafanyakazi na wataalaam mbali mbali wenye utamaduni unaofanana kabisa na wao.

Wazanzibari hao hawakuliangusha jina la Zanzibar, walifanya kazi na biashara zao na. walishauri serikali ya Dubai kwa uaminifu kabisa.


Mapinduzi ya Zanzibar kisiasa yalizaa pia mapinduzi ya kiuchumi Dubai, yenye neema kubwa sana kwa Dubai. "Kufa kufaana".

Itaendelea kidogo kidogo kwa mtindo wa maswali na majibu.

Yeyote anaweza kuongezea nyama kwenye upungufu. Yeyote anaweza kuuliza yanayohusiana na hii mada.
Nimecheka sana wewe zuzu kufurahia mapinduzi ya zanzibar wakati ndiyo yanayo mtia uchungu samia na genge lake la raia feki ...maana hayo mapinduzi yaliua wajomba wa samia na baadhi yao kufanikiwa kukimbilia oman na arabuni huko[emoji16][emoji16][emoji16] ndiyo siri kubwa kwanini SAMIA ana wachukia Nyerere na Karume kuliko Magufuli.
 
Ulitakaje labda,yani waarabu waendelee kukikalia kisiwa chetu pendwa
Hakupinduliwa Mwarabu Zanzibar. Waarabu waliuliwa tu na wengine wakajiondokea.


Iliyopinduliwa ni serikali iliyochaguliwa kwa kura za Wazanzibari.

Kafanye homework yako vizuri.
 
Back
Top Bottom