Demokrasia.Ag11
Member
- Aug 11, 2013
- 5
- 4
Mkuu Matumbo, Baba wa Taifa ni mmoja tuu, Mwalimu Nyerere, Zanzibar sio taifa, ni kitaifa!, ila Baba wa kitaifa hicho ni Abedi Amani Karume!, Okelo anabaki tuu kuwa shujaa wa Mapinduzi yale Matukufu ya Zanzibar!.JOHN Okello ndio baba wa taifa la Zanzibar..bila yeye leo waZnz wangekuwa bado utumwani chini ya mwarabu.
Masahihisho kidogo Field Marshal John Gideon Okello alizaliwa 1937,na Aliuwawa na Field Marshal mwenzake Idd Amin huko Uganda baada ya kuonekana kuwa hatari kwa utawala wake.Alikuwa ni mzanzibari mwenye asili ya Uganda.
Alijifunza siasa ya Ukomunist kutoka kwa Cuba kwa Casto
Ndiye aliyeunda Jeshi na kuliongoza hadi mapinduzi.
ALIKUWA MWANACHAMA WA ASP.
ASP haikuusika moja kwa moja na mapinduzi ila ni yeye mwenyewe binafsi na jeshi lake
Baada ya mapinduzi aliwakabidhi nchi Karume na makamu Babu na wa vyama vya siasa viwili tofauti na yeye kubakia kama kiongozi wa mapinduzi.
Ulitokea mgogoro wa kiungozi kati ya karume na Babu na nafasi ya Okelo ndani ya Zanzibar.
Karume alikubali kuingia kwenye muungano haraka ili kupata ulinzi kutoka bara wa nafasi yake ya uraisi ambayo alipewa na huyu John Okello.
Baada ya kutoelewana na Karume John Okello na alijikuta akikosa wafuasi kwani vijana wengi wa kiislamu walianza kujitoa kumsapoti kutokana na Dini yake.
1971 alifariki nchini Kenya kwa sababu zisizojulikana.
Alizaliwa 1967.
Aliamuru Sultan ateketeze familia yake
sasa nashangaa yanayowapata wakristo Zanzibar Muda huu.
mkuu akina mangi hawajawahi kudai uhuru wa taifa hili, labda unieleweshe walipigana wapi. cha zaidi ni kwamba walikuwa machifu tu wa maeneo yao. ila hao wengine naungana na wewe 100%.Kwa nini tusiwaenzi kina Chief Mkwawa, Mangi Sina, Mangi Mandara, Wakina Chief Songea Mbano na Chief Chabruma wa kule Ruvuma, au Saidi Milambo wa tabora, wakina Isike, Kinjekitile, au Chief Masanja, Chief Mataka wa kule kwa wayao? Who's Okello?
Watu wange[enda lupindisha historia kulingana na matakwa yao ya kisiasa, hasa kwa leo, muda mrefu baada ya mapinduzi ya Z'bar mwaka 1964.
Cha msingi ni kutazama standing facts na conclusions mtu atazijaza mwenyewe.
Tuelewe kimsingi kuwa WALIOPINDUA Zanzibar ni makundi ya waafrika walioungana, kuna waliotoka bara, Kenya na toka Uganda kama vile Okello.
WALIOPINDULIWA ni kundi la watawala, wakati huo chini ya vyama na uongozi wa serikali ya waarabu.
Makundi haya hasimu yamekuwa na tofauti za kimsingi na kubwa sana , na moja kati ya tofauti hizo ni UBAGUZI.Hili halisemwi na wengi sana.
Uzanzibai na Uzanzibara ulitumika kumg'oa Okello Zanzibar.Kama alivyodokeza Mwalimu suala hili la Uzanzibari na Uzanzibara ni matokeo ya ubaguzi uliokithiri katika jamii hii.Na dhambi hii imekuwepo kwa karne na karne waanzilishi wake wakiwa watawala waarabu.
Ubaguzi haukumalizika na mapinduzi ya 1964 bali yaliingia chinichini.
Nakumbuka mnamo miaka ya 1980's kule Pemba Kawawa alipotembelea kisiwa hicho kulikuwepo na maalamiko kwamba kwa nini serikali imezuia watwana toka bara kwenda kulima Pemba.
Kawawa alishangaa sana na kuwauliza kuwa bila watwana basi nyie hamli chakula?
Hivi ni moja ya vielelezo vya kwa nini watu waliokulia na kuishi katika ubaguzi wa aina fulani wanavyoweza kujisahau asili yao.
Mwaka 1964 mimi nilikuwepo Dar nikiishi Temeke karibu na Mgulani-sehemu iliyokuwa kambi kubwa ya jeshi kuanzia vita kuu ya pili.
Mwaka huo ulikuwa wa misukosuko mingi sana kwa serikali changa ya Tanganyika ,Zanzibar na hata Kenya na Uganda.
Baada ya Mapinduzi Zenj, vugu vugu la vurugu lilihamia Dar, na mimi nilisikia hata milio ya risasi katika majaribio ya maasi.
Kenya nako misuko suko ya kijeshi ilikuwepo na hivyo Afrika Mashariki hakukuwa kwema sana , ikia pamoja na Uganda.
Katika mazingira haya mtu kama Okello , mtu ambaye ana asili ya bara, isingekuwa rahisi kubaki Zanzibar,Tanganyika au hata Kenya.
Leo angeitwa terrorist!
Hii ni pamoja na ukweli kuwa kuna wabara wengi walioshiriki vile vile mapinduzi hayo ya mwaka 1964.Namfahamu Jenerali mmoja mstaafu mwenye simulizi nyingi sana za matukio ya wakati huo, na ni jinsi ipi wabara walishiriki, nayeye akiwemo.
Bismillah rajaun,Mungu mlaze baba wa Taifa letu John Okello mahala pema peponi na awaadhibu wote wanamhujumu na kuteka mafanikio yake.
SOURCE PLEASE maana usituletee mambo yako ya UPENZITafuteni kitabu chake alicho andika mtajua katumwa na nani. Yeye ndio jawabu.kwa uchache amesema ametumwa na yesu kuupindua uislam zanzibar lakini wakristo wenzie walim betray . Kwa mujibu wa okelo mapinduzi yalikua ni crusade na miaka ya mwanzo ya mapinduzi masheikh wengi waliuliwa na kufungwa . Elimu ya dini ya kiislam ilipigwa marufuku . Viongozi wakidhihaki Quran hadharani.
Ilikua pindua zanzibar na dini yao.
SOURCE PLEASE maana usituletee mambo yako ya UPENZI
YAITWAYO "MAPINDUZI"
John Okello alitoka kwao Uganda, Injin aliyetoka kwao Kenya na Mfaranyaki aliyetoka Tanganyika, na kuivamia nchi huru usiku wa manane wa kuamkia tarehe12 Januari 1964. Wananchi, mafisadi kwa sababu ya maslahi ya nafsi zao hawakuhisi uchungu kuipoteza nchi yao, wala kuzipoteza roho za wazee wao, za ndugu zao na za marafiki zao. Kwa mujibu wa kitabu cha huyo aliyejipa ujamadari wa hayo 'mavamizi' ya Januari 12, 1964, John Okello, amesema kuwa watu waliyokufa katika 'mavamizi' hayo ni 13,000. Hii ni idadi ndogo kabisa aliyopenda kuitaja.
Ukatili, ushenzi na unyama uliofanywa katika visiwa hivi vilivyokuwa na ustaarabu wa kupigiwa mfano, hauwezi hata kuhadithika. Wengi waliokuwa wanaijua Zanzibar, waliona taabu kuyaamini waliyokuwa wameyasikia yametokea Zanzibar kutokana na hayo yenye kuitwa 'mapinduzi'. Ilifika hadi, siku hiyo ya 'mavamizi' washenzi na makatili hao kuwanajisi maiti wa kike. Kitendo hicho hakijawai kufanyika katika nchi nyingi ulimwenguni zenye ubinaadamu na ustaarabu wake. Lenye kuzidi kushangaza na kusikitisha ni kumsikia mwananchi mwenye kujulikana kuwa yeye ndiye mwongozi wa hao wenye kujiita "progressives" akasema kuwa, watu waliyouliwa katika hayo yenye kuitwa 'mapinduzi' ni 491! Duh!
Mwenyewe Okello alieongoza hayo mauwaji amesema kuwa wamekufa wananchi 13,000. Hata wangekuwa watano tu, bali ni binaadamu, ni wananchi, jee, ndio wawe wamestahiki kuuliwa kwa kuvamiwa nchi yao na wageni ambao wewe na wenzio kama wewe mmechanganyika na hao wageni katika kuifisidi nchi na wananchi wake? La kustaajabisha zaidi - ni pale ilipojulikana kuwa haya yote yalipangwa kabla - kwa siku 30 tu yaaani Desemba 10 mpaka Januari 11 ilitosha kujuwa uovu wa Serikali hata ikastahiki kupinduliwa? Hata ingelikuwa ni ovu hivyo, bali njia za kuiondowa za kikatiba zilikuwepo ambazo zingaliweza kutumika, khasa na hao Wapinzani. Haikuhitaji hata kidogo kutumia nguvu. Lakini hakika khasa ni kuwa mambo yalikwisha pangwa zamani, hayo yalikuwa ni matekelezo tu!!
Yule uliyemuuliza alitaka kukupotosha. Tafuta kitabu Revolution in Zanzbar,1967,(Nairobi: African Publishing House). Ni autobiography ya John Okello mwenyewe.SOURCE PLEASE maana usituletee mambo yako ya UPENZI
Unakubaliana kuwa Okello alisoma CUBA?Masahihisho kidogo Field Marshal John Gideon Okello alizaliwa 1937,na Aliuwawa na Field Marshal mwenzake Idd Amin huko Uganda baada ya kuonekana kuwa hatari kwa utawala wake.