Kuna so many Untold story Kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar ambazo zinafichwa Na kuchakachuliwa ili kuficha ukweli. Mapinduzi hayo yaliyomng'oa Sultan Jamshid bin Abdullah yalibuniwa, kuasisiwa Na kutekelezwa Na John Gideon Okello Kama Kijana aliyejinatisha Kwenye vuguvugu la Afro Shirazi akiwa Na Umri wa Miaka 27 tu wakati huo. Okelo ambaye alizaliwa 1937 mwaka ule wa Mapinduzi 1964 alipata miaka 27tu imargine.
Okelo ambaye Alikuwa Polisi huko Pemba aliingia Unguja 1963 akaunda kikosi Chake Kwa kutumia Silaha Za jadi wakaisambaratisha ngome ya Sultani kimchezomcheZo huku zaidi ya waarabu 18,000 wakichinjwa Kama kuku.
Okelo ambaye hakujali Dini Yake au Imani Yake aliwaunganisha wazanzibar wote na wakati huo Waasisi wa Afro Shirazi Sheick Karume na Abrahaman Babu wako Darisalama wanakula mishikaki hawajui kinachoendelea Zanzibar.
Okelo Baada ya Mapinduzi akaunda Baraza la uongozi wa Nchi likiongozwa na Karume Kama Mwenyekiti na Abrahaman Babu kama Waziri mkuu. Wakatafutwa Mabwana Hawa tokea Darisalama Kama Ndoto wakaitiwa urais. Okelo ambaye Kwa kukubalika angejiweka Kuwa Raisi nani angemtoa? Zanzibar ya Leo Ingekuwaje.?!,.
Lakini mambo haya yanasahaulika faster, mwarabu aliyeleta Dini, akaidhoofisha sana Zanzibar Leo kuna watu wanajitokeza kutaka kuturudisha tulikotoka Kwa kuenzi DINI NA UDINI. Mtu Mwenye Akili timamu anatoa pofu Mbele ya jamii akidai Sheria Za Dini yake yeye zitumike Kwenye Jamhuri ya Muungano, Mtu mzima kabisa anadai kuwe na Mahakama Za UDINI zinazotambulika na kufadhiliwa na Nchi.
Kama John Gideon Okelo angekuwa Mdini au angeendekeza UDINI angeunda Baraza lake la Ukristo na Hakuna ambaye angepinga. Lakini mwanamapinduzi huyu Ni mwafrica, anapigania Haki Za wengi Kwenye Nchi Yao na sio UDINI.
Tukiendekeza Ukristu Wetu, Uislam Wetu au Uhindi Wetu, tukaanza kutoa pofu kulazimisha Sheria Za Dini Zetu zitambuliwe na kuenziwa na Nchi, Ni UHAINI, Ni kuliuza na kulihamisha Taifa liwe Mali ya Taifa Jingine.
Taifa ni letu Sote, kila Mtu ana uhuru wa kuabudu atakacho na ajuacho pasipo kuvunja misingi ya Nchi. Wanaojaribu kulipasua Taifa Kwa kuendeleza uzezeta Wao wa UDINI hawapaswi kuchekewa. Lazima wakaripiwe na kuonywa na kuchukuliwa hatua kali Za kisheria Kama wahaini.
Taifa hili ambalo kila kukicha waislam wanaoa wakristu, wakristu wanaoa waislam, maelfu Kwa maelfu, haitoshi utasikia Kule wakristu mamia wanasilimu Kuwa waislam na waislam maelfu wanaokoka ha Kuwa wakristo. Bado haitoshi kuna maelfu ya familia ambazo Wazazi wawili kila mmoja ana Dini Yake na wanaishi Kwa Amani kabisa. Na tumeishi hivi vizazi Kwa vizazi Nani Leo Hii anataka kutibua mustakabali wa ustaarabu wa Nchi hii.
Waacheni waislam wafanye mihadhara Yao HATA wakiconvice Taifa zima likawa waislam lakini Bado Hii Ni Nchi ya kijamhuri. HATA Kama wakristo wakihubiri Na ku convince waislam wote tukawa wakristo lakini Bado Hii Ni Jamhuri.
Tufanye mistaarafu Za Dini zetu pasipo kuchokonoa misingi ya utawala wa Kijamhuri.