Mapinduzi ya Zanzibar: Mchango wa John Okello (Che Guevara wa Afrika Mashariki) umefutwaje?

Ninamjua Abdul waheed Sykes kama mwanamapinduzi na mwasisi wa TANU yeye na wenzie akina Dossa Aziz kabla ya Mwalimu J.K Nyerere.

Unataka kusemaje?

Hayo ya kuwa Muasisi wa Tanu tunayapata kwenye maandiko ya Mohamed said kwa kuwa kiserikal kila kitu kafanya Nyerere na 'wenzie'

Kwa hiyo na kwa Zanzibar Mapinduzi alifanya Karume na 'wenzie' na Okelo yumo humo kwenye na 'wenzie'

Hata Africa kusini, Nyerere yupo kwenye Kundi la 'nakadhalika'
 
Ninamjua Abdul waheed Sykes kama mwanamapinduzi na mwasisi wa TANU yeye na wenzie akina Dossa Aziz kabla ya Mwalimu J.K Nyerere.

Unataka kusemaje?
Anataka kijua namna mchango wke unavyotambulika
 
Labda Okello alikuwa Mgalatia kindakindaki.
Okelo hakua na ugalatia kindakindaki historia yake amefungwa na kufukuzwa nchi zote EA alikua mkatili ndio maana aliongoza mapinduzi unless uniambie Wagalatia kindakindaki ni wauaji
 
naumbu UNASEMA OKELO ALIFUKUZWA KWA SABABU YA UKATILI NA MAPINDUZ ALYOFANYA? KWA HYO KUMBE ILIKUWA KOSA KUFANYA MAPINDUZ? MBNA MNAYAFURAHIA?
 
Nakumbuka Nilimfaham John Okello kupitia mwalm wetu wa History aliyekuwa ni mganda. Bas utapenda jinsi anavompamba mganda mwenzake.
Hakuwa anapambwa bali huo ndio ulikuwa ukweli, kwenye nyaraka za waliofanya mapinduzi anaitwa Field Marshal John Okello.
 
Mapinduzi yakifanyika Karume alikuwa dar anakunywa valuu
 
[emoji106] yaani alikuwa kama karai la kukodishwa, kazi ikiisha linatupwa kule mwenye nalo ndio aliokote
 
Kuna kitabu niliwahi kukisoma kinasema huyo jamaa alikuwa mkenya aliyeishi Uganda pia alichangia kukamilisha mapinduzi ya Zanzibar.

Baada ya hayo alirudi Uganda akawa mtu wa karibu sana na Idd Amin Dada wa Uganda ila alijiharibia baada ya kusema maneno haya 'NOW UGANDA HAS TWO FIELD MARSHALS'

usemi huo wa John Okello ulimuudhi sana dikteta Idd amin dada maana alihisi kama Okelo alikuwa na mpango wa kuja kumpindua basi Idd Amin Dada akamuua mapema tu, huo ndiyo mwisho wa John Okelo.
 
John Okello alikodishwa Kama Mpiganaji Mamluki.

Kwenye Sherehe za Uhuru wa Kidemokrasia wa Africa Kusini ushawahi kusikia Nyerere anatajwa kule?



Kwahiyo kama Nyerere hatajwi basi nasi hatupaswi kumtaja Okelo! nilidhani mnyonge mnyongeni lakini haki yake aipate
 
Mapinduzi yakifanyika Karume alikuwa dar anakunywa valuu

Wakati Mobutu seseseko anapinduliwa Hayati Laurent Kabila alikuwa Mikocheni Dar Es salaam

Wakati RPF wanakinukisha Kigali, Kagame alikuwa Kampala

Wakati wa Iran wanakinukisha Iran Ayatollah Khomein alikuwa Paris

Wakati Zimbabwe wanakinukisha Mnangagwa alikuwa Pritoria

Wakati wanajeshi wetu wanakinukisha Kampala Nyerere alikuwa Msasani Dsm
Wakati ZANU of wanakinukisha Zimbabwe Mugabe alikuwa Zambia

Viongozi wa Mapinduzi/ Mapambano huwa hawawi eneo la tukio ukiona upo eneo la tukio Wewe ni mpiganisha vita sio Kiongozi wa Vita ndio sababu Karume alikuwa Dar anakula bata Okelo akawa Eneo la tukio
 
Historia ya Zanzibar ni tata nayo.Historia tuliyo fundishwa darasani inatueleza kuwa Karume ndiye wa kwanza;lakini ukisoma vitabu vinasema Okelo baada ya kuchoshwa na uamuzi wa Karume kutokurejea Unguja alijitangaza kuwa rais na amir wa jeshi.Pia mapambano ya baada ya mapinduzi hayatajwi kabisa utadhani kazi ilikwisha usiku ule wa th 12.
 
Ukimtaja Okello utaharibu ladha nzima ya Mapinduzi kwa kuwa itaonekana ni uvamizi toka nje ya nchi badala ya Mapinduzi ya Wazanzibari!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…