Mapinduzi ya Zanzibar: Mchango wa John Okello (Che Guevara wa Afrika Mashariki) umefutwaje?

Mapinduzi ya Zanzibar: Mchango wa John Okello (Che Guevara wa Afrika Mashariki) umefutwaje?

I have been asking myself for quite a long time now. Why is it difficult for a simple history of about 48 years past to be proved? Why is it difficult to prove such a simple history which was witnessed by most of Zanzibaris who are present today. Is it hatred of John Okello?
I was reading an article by Ahmed Rajab on Raia Mwema of 22nd Feb 2012. The article was full of hatred rather than history. It was a misleading article. It was regarding Okello as a madman, useless, not known but branded himself with ranks. How come?
But if you peruse history of revolution, Okello was the hero of Zanzibar. No Okello, no revolution. He organized and led the revolution with the Youth League while Karume was hiding in Dar. Its he who appointed Karume as the President. And he is the founder of the Revolutionary council of Zanzibar.
A phrase in history reads:
On January 12, 1964, with popular support from the island's oppressed native African majority, Okello and his men fought their way to the capital of Zanzibar, Stone Town, where the sultan lived. Even though they were poorly armed, Okello and his men surprised the police force of Zanzibar and they took power.

During a speech on radio, Okello dubbed himself the "field marshal of Zanzibar and Pemba". He gave the sultan an order to kill his family and to kill himself afterwards; otherwise, Okello would do so himself. However, the sultan had already brought himself to safety later to be harboured in Britain. The prime minister and other ministers also managed to escape.
...
Having taken control of the island, John Okello invited Abeid Karume back to the island to assume the title of President. Other Zanzibaris in foreign territory were also invited back, most notably the Marxist politician Abdulrahman Mohammad Babu, who was appointed to the Revolutionary Council. John Okello reserved for himself the title of "Field Marshal", a position with undefined power.[SUP][5][/SUP]

...so Okello created a Revolutionary Council and named the leader of the Afro-Shirazi Party, Abeid Karume, as president and leader of the (Arabic) Umma-(Massa) Party, sheik Abdulrahman Muhammad Babu as prime minister (later: vice-president). Both Karume and Babu had not been informed of the coup. Both residing in Tanganyika, but returned to Zanzibar, where they were welcomed by Okello. However, neither Karume nor Babu wanted anything to do with him. Afterward, Okello appeared to be too unstable to play any role in government of the new country and was quietly sidelined from the political scene by Karume, who allowed him to retain his title of Field Marshal.
Then Karume used his political skills to align the leaders of neighboring African countries against Okello, and invited Tanganyikan police officers into Zanzibar to maintain order. As soon as Okello took a trip out of the country, Karume declared him an "enemy of the state" and did not allow him to return. Given the presence of Tanganyikan police and the absence of their leader, Okello's gangs of followers did not offer any resistance.

QLCoLDxTw2JsP8P174SQqtdU04AAAAASUVORK5CYII=



Ref: Bakari, Mohammed Ali (2001), The Democratisation Process in Zanzibar
 
Historia hupenda kujirudia haya mambo yamechanganya toka wakati wa mkoloni, mimi ningependa kuangalia zaidi historia ya Zanzibar kuanzia tuseme about 1960, wakati waingereza wakijitayarisha kuwaachia wazalendo kujiendesha. Kama ilivyokuwa Tanganyika kipindi hiki Znz wakafanya uchaguzi, tofauti na Tanganyika ambako Tanu walishinda kwa kura nyingi na Nyerere kuwa waziri mkuu mambo visiwani ilikuwa tofauti.

CHAGUZI ZA MWANZO

Uchaguzi wa mwanzo Januari 1961 ZNP na ASP kila kimoja kilipata viti 11 ingawa ASP walidai kuwa wameibiwa kura (Kumbuka CUF 95,00,05??), hivyo wakoloni wakatayarisha uchaguzi mwingine Juni mwaka huo na kuongeza viti kuwa 23. ZNP kwa kuungana na ZPPP wakapata viti 13 na ASP ikapata 10 ingawa walishinda kura nyingi. Fujo zikaibuka watu wakauwawa (Pemba 00??) ASP wakadai faulu ya wizi wa kura na vilevile kudai kuwa mipaka ya majimbo ya uchaguzi yalipendelea ZNP, kwamba majimbo yao ASP yalifanywa kuwa makubwa kwa makusudi.

Baada ya kutwaa madaraka ZNP/ZPPP ikapiga marufuku baadhi ya vikundi, na kujaza serikalini watu wao na kufukuza wale ambao iliona wanalalia upande wa ASP.(Kumbuka CCM Znz baada ya uchaguzi 00,05 na madai ya Kuonewa wanachama wao toka CUF??)

Kabla ya Uhuru uchaguzi mwingine ukafanyika tena 1963 na kama 1961 mambo yakawa vilevile majimbo yakaongezwa na kuwa 31, ingawa mseto wa ASP ya Karume na Umma Party cha Babu walishinda 54% ya kura walipata viti 13 na ZNP/ZPPP kuchukua vilivyobaki. ZNP chini ya Shamte wakaongeza ubaguzi wao serikalini na mashirika ya umma (CCM baada ya 95,00??) wakawafukuza kazi wanajeshi na polisi wenye asili ya bara, wakapiga marufuku Umma party na Babu akakimbilia Dar.

Uhuru kamili toka kwa waingereza ulipotangazwa mnamo 10 disemba, 1963 ZNP/ZPPP wakawa wameshika hatamu kwenye usultani wa kikatiba (constitutional monarchy) huku sultani Jamshid akiwa kiongozi wa nchi na Shamte waziri mkuu.

INGIA JOHN OKELLO

Huyu bwana hatajwi sana siku hizi kwenye siasa za Zanzibar, lakini mzaliwa huyu wa Uganda ndio alikuwa kinara wa mapinduzi ya Januari 64. Bado wasomi wa historia wanazozana kuhusu Karume na Babu kama walihusikaje kwenye mapinduzi haya...Ingawa Babu amekiri mara kadhaa kutojua kwake kwa haya mapinduzi yaliyochochewa na Okello. Inadaiwa pia kuwa Okello alimpeleka Karume Dar ili awe salama wakati huo ingawa ni wazi Karume alikuwa na shughuli nyingine tofauti Bara kipindi hicho.

Kipindi hicho kulikuwa na tetesi ya mapinduzi ambayo Babu, Hanga na kwa kushirikiana na Kambona walikuwa wanaanda kuipindua serikali , hivyo basi Okello akawawahi kwa kushirikiana na mgambo na vijana wa ASP youth league na polisi waliofukuzwa kazi waliweza kuteka vituo vikuu vyo polisi mji mkongwe na kuteka redio na uwanja wa ndege. Jamshid, Shamte na baraza la mawaziri walifanikiwa kutoroka Znz kwa kutumia meli ya sultani Seyyid Khalif kwenda Dar na baadae Sultani alienda Portsmouth, UK alipo hadi leo...sijui kwa nini hakwenda kwa babu zake Oman mi sijui sababu alikimbilia kwa wakoloni zake wa mwanzo. Anyway Okello akaanza vitisho redioni na kuamrisha vikosi vyake kuwakamata waarabu na wahindi visiwani, kukawa na umwagaji mkubwa wa damu ambao hadi leo hatujui idadi kamili, ubakaji, wizi na uharibifu mkubwa wa mali.

Angalia video hii ya kasheshe kipindi hicho

Arab Massacre in Zanzibar - YouTube

Hii video ni sehemu ya sinema ya kiitaliani inaitwa Africa Addio. Kwa kweli kuna ubishi wa idadi kamili ya vifo kuanzia 1,000 hadi wengine wanadai 20,000 SMZ haijawahi kutoa tamko wala kuunda tume huru kuchunguza mauaji haya ya mapinduzi.

Cha msingi tunajua kilichotokea baada ya mapinduzi Karume akarudi na kuwa Rais, likaundwa baraza la mapinduzi Babu akawa waziri wa mambo ya nje Hanga makamu wa rais. Muda si mrefu Okello akazuiwa kuingia Znz wakati anarudi safari toka Dar mwishowe alirudi uganda ambako inaaminika Idi Amin aliimmaliza 1972, baada ya yeye Okello kudaiwa kusema kuwa sasa Uganda ina field marshall wawili, yaani yeye na Amin.

Hata hivyo kama haya mapinduzi ambayo SMZ inadai ni matakatifu mbona nabii wake mkuu yaani Okello hawamuenzi? yaani Znz vijana wengi siku hizi hawajui Okello ni nani, na wala ushirika wake katika mapinduzi yao. Hakuna kumbukumbu (barabara au square) wala hatajwi mashuleni kwao.

Je Okello ni Shujaa (Hero) au Haramia (Villain)? only history will tell...

MUUNGANO BAADA YA MAPINDUZI

Ingawa wengi naona humu wanadai kuwa muungano uliletwa kuzuia ujio tena wa Sultani, historia inaonyesha tofauti. Mapinduzi kwa kiasi kikubwa yaliungwa mkono na weusi wengi Znz hasa unguja ikumbukwe wakati huo idadi ya watu znz ilikuwa kama 300,000 huku weusi na washirazi kama 230,000 waarabu 50,000 na wahindi/waasia 20,000. Ingawa idadi kubwa tu ya watu walikuwa ni mchanganyiko, lakini weusi walikuwa wanatengwa ZNP hawakuwa na waziri mweusi kwenye baraza lao na vilevile kazi nyingi za juu serikalini walipewa waarabu na wahindi. Weusi kwenye sekondari hawakuzidi 12%...Hivyo basi sera za mwanzo za ASP na Umma za kuongeza nafasi za kazi, shule pamoja na kujengea weusi makazi bora pamoja na kuwaongezea huduma za afya ziliwapa wapenzi wengi.

Tatizo likawa kama kwenye serikali nyingine za kiafrika upinzani ukapigwa marufuku, uhuru binafsi na wa kujichanganya ukawa duni, uhuru wa vyombo vya habari nao vilevile ikawa hakuna.

Ingawa Karume alikuwa popular lakini bado alikuwa na wasiwasi na vuguvugu la Umma party na sera zao za mlengo wa shoto(ukomunisti), na hii ndio inaaminika kuwa sababu kubwa ya kuungana na Tanganyika na si tishio la kurudi sultani. Wengine wanasema baada ya mkutano kati ya Obote, Kenyatta, Karume na Nyerere kuhusu kuunda Shirikisho la afrika mashariki kuvunjika, basi Nyerere na Karume wakaamua kuunda muungano wao bila kujali Kenya na Uganda.

Ukweli halisi hatuwezi kujua maana wote ni marehemu.

UAMSHO NA HARAKATI ZA SASA??

Tatizo kwenye vuguvugu la sasa ni jee hawa wanaitaka Zanzibar ipi? ile baada ya Uhuru chini ya sultani na ya kibwanyenye au ya Karume kabla ya muungano ya mrengo wa kushoto na ukandamizwaji au kuachana na hizo na kujaribu mpya kabisa. Kwa wafuatiliaji wa siasa za Zanzibar tangu awali utaona kuanzia wakati wa ZNP na ASP hadi sasa kati ya CUF na CCM siku zote visiwa hivi vina siasa kali za mfarakano mkubwa...kwamba CUF ndio ZPPP ya leo ni suala la kuwaachia wenyewe wajadili, lakini ni wazi kuwa Pemba ndio ngome kuu ya CUF kama ilivyokuwa kwa ZPPP. Na CUF vilevile inadai Zanzibar huru ingawa inaendelea kufaidi matunda ya muungano.

Uamsho wanapiga tu makelele na ni wazi wanafadhiliwa na wazito toka Oman, ila ni vyema wajue kuwa waarabu si wafadhili wazuri siku zote, angalia kama wangekuwa wafadhili wazuri wasingeruhusu waarabu/waislamu wenzao ambao hawana mafuta kuwa maskini wa kutupwa na kuteswa (i.e Yemen, Palestine, Somalia)

Vilevile serikali zao hivi sasa haziko imara, pili ujuzi wao wa kuendesha NGO/ asasi binafsi si mzuri na sera za wazi hawana zaidi ya kufadhili makundi ya kigaidi. Mi nafikiri mwisho Uamsho itabadilika na kuwa chama kipya cha siasa Znz na kuwa chama cha upinzani, ambacho kitakuwa kitu kizuri maana hivi sasa Znz hawana upinzani rasmi baada ya CUF kuungana na CCM kwenye SMZ, ingawa muungano huo wa CUF/CCM utadumu muda gani hatujui.

Tusubiri hiyo kura ya maoni na baada ya hapo tuone kama Znz itaweza kukwepa siasa za kuumizana na kupigana bakora, ambazo hazijalishi status ya Serikali kuanzia wakati wapo huru (61,63,64) au ndani ya muungano (72 mauaji ya karume, 95,00 mauaji pemba)...Kumbuka historia hupenda kujirudia. Tuombe liwalo lolote liwe la kheri maana Znz na Tanganyika ni ndugu na kheri visiwani ni kheri bara, aidha kwenye muungano au nje ukweli huu wa udugu utakuwepo tu siku zote.

Karl Marx alisema "History repeats itself, first as tragedy, second as farce"


Yetu macho

Nawakilisha
 
John Okello inapaswa atambuliwe kwenye mapinduzi ya Zanzibar, sababu alivyo plan na kuwahamasisha watu kwa kuwaambia eti ameoteshwa usiku na watu wakakubali nakufanya kweli, pia hakuwa mchoyo waliopata madaraka walikuwa Dar wala huo mpango wa ghafla hawakuujua. Baada ya muda mfupi wakamgeuka, hatujui sana lakini wengi wanasema ni sababu ya itikiadi yake na ugeni.

Jamani wa Zanzibar tupendane na kuachana na haya maitikadi ya wageni yanayotubagua.
 
Even nowadays only the new comer weather from Asia o Africa especially Mainland are the one carring the economy ahead, workers from Mainland are seriously wanted in all big European investors companies
 
John okello alionesha mchango mkubwa sana ingawa alichafuliwa na viongozi kwa maslai yao na kuwajaza wananchi ijinga
 
Kweli jamani Wazenji please waenzini basi watu waliotoa afya zao kwa ajili ya ukombozi wenu, acheni kuficha majina yao kwa sababu za kiitikadi nk. Kwa kufanya hivyo mnaweza kuepuka majanga mengine yanayotokana na hiyo laana

Mwka 1964 siku thelathini baada ya uhuru wa bandia wa Zanzibar, wanamapinduzi kumi na nne wakiongozwa na mpigania uhuru John Okello aliwaongoza kwenye mapinduzi ya Zanzibar yaliyokuwa na umwagaji mkubwa wa damu.

Baada ya mapinduzi kufanikiwa John Okello [kiongozi wa mapinduzi] alichukua jukumu la kutangaza mapinduzi kwenye radio Zanzibar, ikumbukwe pia wakati mapambano yakiendelea ..aliyekuja kuwa rais wa Zanzibar mzee Karume na Babu walikuwa mafichoni na hawakushika wala bisibisi kwenye mapinduzi na hata ukiangalia ile picha ya wanamapinduzi ya kwanza John Okello amevalia kipolisi na amekaa kama kiongozi rasmi.

Baada ya hali kutulia Okello anamtangaza Karume rais na Abdulrahman Babu kuwa Waziri mkuu. Na ndie aliyeenda kumpokea Karume kutoka alikokuwa amejificha kwa siku kadhaa.

Baada ya siku chache mzee Karume akamfukuza Zanzibar kama mbwa John Okello [Field Marshal] na bila kujali mchango wake anatokomea kusikojulikana na historiaa ya mapinduzi ikafutwa na nafasi ya Okello ikaja kuwa mkwezi, mpiga tofali ambaye alibahatika kupiga picha [akiwa amekaa kitini katikati tu kwa sababu ya kuwa na kipaji cha kuongea - (kumbuka kuwa hata kiswahili chake kilikuwa 0kibovu)]

Naomba kuchokoza mada kuhusu nafasi ya John Okello kwenye mapinduzi, kwa nini historia ilifunikwa?

Je aliishia wapi,..wapenda historia ya kweli wameshatamani hata kujua lilipo kaburi lake..kumbukeni wenzetu Kenya baada ya kugundua hila wanahaha kutafuta kaburi la Field Marshal Dedan Kimathi...mbona wapenda hitoria Zanzibar na Tanganyika kwa jumla hamumtendei haki JOHN OKELLO [FIELDMASHAL]?
 
kila siku Karume baba wa mapinduzi! Kuna kitabu niliwahi kusoma huyu Karume anaesemwa kiongozi wa mapinduzi alikuwa ni mwoga kweli kweli alipoambiwa kuandaa mapinduzi aliogopa, hakuwakubalia wenzake akiofia kunyongwa na Sultan, alitanguliza sana familia yake katka harakati hizo! na siku ya mapinduzi inasemekana alikimbia visiwa kujificha bara na wala hakushiriki kabisa! na kikubwa ni kwamba alipokwenda chuo kikuu cha Dar es salaam baada ya mapinduzi, aliulizwa na mwanafunzi kuwa, wewe (marehemu Karume) tunafahamu haukushiri katika mapinduzi, yuko wapi Field Marshal John Okello? jamaa akajikanyaga! niliona majuzi kwenye gazeti la Raia Mwema mchambuzi mmoja wa bara akichambua kifasaha kabsa mapinduzi hayo na ushiriki wa FM Okello akimlinganisha na Che Guevara na Fidel Castro lakini mwandishi huyo akapokea CRITICS KALI kutoka kwa mwandishi mwenzake kutoka visiwani akidai FM Okello HASTAHILI tunu kama ya Che kwamba FM Okello alikuwa ni GAIDI! kwa hiyo waweza ona fikra za wazenj kwa mtu huyu aliye watoa mikononi mwa Sultan aliyekuwa akiwa nyanyasa ndani ya ardhi yao! LALA PEMA FIELD MARSHAL JOHN OKELLO!
 
daaah nashukuru sna wadau hapa kwa kweli nimegain sna hz info sikuwanazo nashukuru sna the great thinkers!!
 
Hivi wale wazanzibar jinsi walivyo waoga na wazembe wangejaribu kweli kufanya mapinduzi wenyewe?

FM Okello aliwasadia sana, kama si yeye nafikiri mpaka leo wazanzibar wangekuwa chini ya Sultani.
 
kila siku Karume baba wa mapinduzi! Kuna kitabu niliwahi kusoma huyu Karume anaesemwa kiongozi wa mapinduzi alikuwa ni mwoga kweli kweli alipoambiwa kuandaa mapinduzi aliogopa, hakuwakubalia wenzake akiofia kunyongwa na Sultan, alitanguliza sana familia yake katka harakati hizo! na siku ya mapinduzi inasemekana alikimbia visiwa kujificha bara na wala hakushiriki kabisa! na kikubwa ni kwamba alipokwenda chuo kikuu cha Dar es salaam baada ya mapinduzi, aliulizwa na mwanafunzi kuwa, wewe (marehemu Karume) tunafahamu haukushiri katika mapinduzi, yuko wapi Field Marshal John Okello? jamaa akajikanyaga! niliona majuzi kwenye gazeti la Raia Mwema mchambuzi mmoja wa bara akichambua kifasaha kabsa mapinduzi hayo na ushiriki wa FM Okello akimlinganisha na Che Guevara na Fidel Castro lakini mwandishi huyo akapokea CRITICS KALI kutoka kwa mwandishi mwenzake kutoka visiwani akidai FM Okello HASTAHILI tunu kama ya Che kwamba FM Okello alikuwa ni GAIDI! kwa hiyo waweza ona fikra za wazenj kwa mtu huyu aliye watoa mikononi mwa Sultan aliyekuwa akiwa nyanyasa ndani ya ardhi yao! LALA PEMA FIELD MARSHAL JOHN OKELLO!
Huyu John Okelo lawezi kupewa heshima anayostahili kwa sababu ya dini yake,hawa wazenji wanaona aibu kwa nchi ambayo asilimia zaidi ya 98 kuongozwa katika mapinduzi na mtu ambaye ni Kafir!
 
Huyu John Okelo lawezi kupewa heshima anayostahili kwa sababu ya dini yake,hawa wazenji wanaona aibu kwa nchi ambayo asilimia zaidi ya 98 kuongozwa katika mapinduzi na mtu ambaye ni Kafir!

Historia inakawaida ya kukutafuna hasa pale unapo shindwa kuikubali, ila ni muda mwafaka wazenj kumkubali na kumpa heshima anayostahili FM Okello na si kuelendelea kuficha ukweli na ndo sasa tunaona wameanza kuja jamaa za masultan kwa kofia ya Zanzibar huru...wataona muda si mrefu matunda ya marejeo ya Sultan ndipo wataanza kukumbuka watu majasiri kama Okelo hawapo Zanzibar tena....
 
Hivi wale wazanzibar jinsi walivyo waoga na wazembe wangejaribu kweli kufanya mapinduzi wenyewe?

He! kumbe sifa anazopewa Karume kumbe c zake? kumbe hawa jamaa kunguru wa unguja (waoga) halaf wazembe, duh?
 
Lakini cha ajabu nasikia NYERERE ndiye aliyekuwa anamfahamu Okello kwa unadni na ndiye aliyemleta Zanzibar.. Mara baada ya Okello kujitangaza kuwa ndiye Kiongozi wa mapinduzi nasikia Karume alikuja kumshtaki kwa mwalimu na mwalimu akamzuia kurudi TZ(alikua safarini nje ya nchi KENYA au UGANDA)na tokea hapo akaptea kabisa sijui kama simulizi hizi ni za kweli au la..
 
MWANAHARAKATI John Gidion Okello,
kama alivyokuwa mkombozi wa Cuba,
Ernesto “Che Guevera”, ni mmoja wa
wanamapinduzi nadra na mashuhuri
duniani walioendesha mapambano
kukomboa nchi zisizo zao, kisha
wakafukuzwa kama watu wasiotakiwa.
Lakini tofauti na “Che Guevera”, raia wa
Argentina aliyeongoza mapambano
yaliyofaulu, kupindua Serikali dhalimu ya
dikteta Fulgencio Batista nchini Cuba,
wakishirikiana na wanaharakati
wazalendo, akiwemo Fidel Castro na
wengineo, baada ya hapo akawa Waziri
nchini humo; John Okello, kwa upande
wake, baada ya kufanikisha mapinduzi
nchini Zanzibar, Januari 12, 1964,
alifukuzwa, akapigwa teke bila huruma
wala shukrani kama mtu asiyetakiwa.
“Mimi nilimfanya Sultani apoteze ufalme
wake, lakini hali yangu ni mbaya zaidi
kuliko yake. Sultani alipokelewa vizuri
Uingereza, lakini mimi ndugu zangu
(Waafrika) wenyewe wamenifukuza”,
alilalama miezi michache baada ya
kufukuzwa Zanzibar.
Na katika kuhakikisha kwamba historia ya
ushiriki wake katika mapinduzi hayo ya
kihistoria inatupwa na kufunikwa chini ya
zulia isahaulike na kupotea, viongozi wa
Zanzibar wamehodhi historia ya
mapinduzi ili waweze kujikweza kwa
kujipachika sifa kuwa wao ndio
wakombozi wa Zanzibar kutoka utawala
wa Sultani.
Ni kwa sababu hii, natofautiana na
Mwandishi wa habari gwiji, mkongwe na
wa kimataifa, Ahmed Rajab, katika mada
yake: “Siku Field Marshal John Okello
alipotimuliwa Zanzibar”, kwenye gazeti hili
la 22 – 29/2/2012 alipodai kwamba,
mwanamapinduzi “Field Marshal” John
Okello, raia wa Uganda, hakuwa muhimu
na mwenye nafasi duni isiyohesabika
katika mapinduzi ya Zanzibar.
Mwanahabari Ahmed Rajab anaeleza,
pamoja na mambo mengine (na hapa
ndipo utata ulipo), kwamba, makada 200
wa Chama cha Afro-Shirazi (ASP),
wakiongozwa na Yusuf Himid, ndio
walioongoza mapinduzi hayo, na kwamba
hawakukabiliwa na upinzani wowote.
Anasema, haijulikani ni nani hasa aliyepiga
risasi ya mwanzo au ya mwisho katika
mapinduzi hayo, ila kwamba, waliokuwa
wakiongoza mambo tangu mapinduzi
yaanze hadi siku ya pili, Januari 13, 1964,
walikuwa Aboud Jumbe (ASP), Thabit
Kombo (ASP) na Badawi Qullatein wa
Umma Party [UP].
Anaeleza, hakuna uhakika mpaka sasa
nani alimpeleka Okello kujichanganya na
wanamapinduzi na pia kutangaza kwenye
redio juu ya kufanikiwa kwa mapinduzi
hayo, na kwamba, Aboud Jumbe
alipomwona na mabastola yake alishtuka
akauliza: “Nani huyu? Katokea wapi?”
Kadri ninavyomfahamu Ahmed Rajab,
alivyo mdadisi wa mambo kabla ya
kuandika, nalazimika kuamini kwamba,
ameiandika simulizi hii kabla ya kufanya
utafiti wa kina; na pia kwamba (kama
anavyokiri mwenyewe) ameandika “baada
ya kuzungumza na walioshiriki katika
mapinduzi hayo” na ambao kusema kweli,
wengi wao ndio wenye kupotosha historia
ya mapinduzi.
Mapinduzi ya Januari 12, 1964 yalitabirika.
Vuguvugu la chini kwa chini lilianza pale
Serikali ya Uingereza ilipokabidhi uhuru
kwa Serikali ya mseto ya vyama vya
Zanzibar Nationalist Party (ZNP) na
Zanzibar and Pemba People’s Party
(ZPPP), Desemba 10, 1963 kutokana na
uchaguzi mkuu wa 1963, ambapo
Mohamed Shamte wa ZPPP, aliteuliwa
kuwa waziri.
Wazanzibari wengi, hasa wanachama wa
vyama vya ASP na Umma Party (UP) cha
Abdulrahman Mohamed Babu, waliona
wameuzwa kwa kuwa uchaguzi huo
haukuwa huru na wa haki. Hiki ndicho
kilikuwa kichocheo kikuu cha mapinduzi.
Katika uchaguzi huo, Muungano wa ZNP/
ZPPP ulipata viti vya Bunge 18 na ASP 13
kati ya viti 31 vilivyogombewa.
Itakumbukwa kuwa, siku ya uhuru, Babu
alipoombwa kutoa salaam za Uhuru kwa
niaba ya chama chake mbele ya
Waingereza, Sultani na wageni wa
kimataifa, alitamka maneno
yaliyomsisimua kila Mzanzibari na
kuwakanganya watawala wapya. Alisema:
“Salaam kwa Wazanzibari na wapenda haki
wote. Umma Party na Wazanzibari kwa
ujumla, wanasubiri kunyakua utawala wa
nchi na kuuweka mikononi mwao saa
itakapowadia”.
Maneno haya yaliashiria kwamba, Babu na
Chama chake, pamoja na wanamapinduzi
wengine, walikuwa na fundo dhidi ya
Serikali mpya; walipenda kuona
ikipinduliwa nafasi ikitokea.
Baada ya kuingia madarakani, Serikali ya
ZNP/ZPPP ilianzisha programu ya
kuwarejesha makwao Bara, Askari Polisi
wa Kiafrika, wengi wao wakiwa wa kabila
la Makonde kutoka Tanganyika na
Msumbiji na wengine kutoka Kenya, na
nafasi zao kuchukuliwa na Wamanga,
Waasia na Wazanzibari asilia
waliochaguliwa kwa umakini mkubwa kwa
hofu ya usaliti.
Kwa kufanya hivyo, Serikali ilijipunguzia
nguvu ya usalama wa ndani kisiasa na
kiulinzi, licha ya kuua morali ya jeshi la
polisi kwa ujumla. Kwa sababu hii, ilianza
kuajiri kwa njia ya dharura, walinzi wasio
na mafunzo. Hivyo ni dhahiri kwamba,
kama Serikali mpya ingeshambuliwa
kutoka nje wakati huo, isingeweza kuhimili
kishindo kwa sababu ya kuwa na walinzi
wasio na uzoefu wala mafunzo.
Mbaya zaidi ni kwamba, Serikali mpya
haikuwa na mkataba wa kijeshi wa ulinzi
na Uingereza kuweza kusaidiwa, kama
ilivyokuwa Serikali ya Sultani kuanzia
miaka ya 1890 hadi Uhuru, Desemba 10,
1963.
Vigogo hawakutaka mapinduzi
Licha ya kulalamikia matokeo ya uchaguzi
yaliyoiweka Serikali ya Vyama vya ZNP/
ZPPP madarakani, Viongozi wakuu wa ASP
hawakupendelea kuiondoa madarakani
Serikali mpya kwa njia ya mapinduzi. Si
Karume, Kombo wala Aboud Jumbe
aliyekuwa na wazo la mapinduzi hadi
yalipotokea.
Itakumbukwa baada ya uhuru, Karume
alimwendea Waziri Mkuu Shamte,
kumbembeleza akubali kuundwa kwa
Serikali ya mseto wa Vyama vyote
vilivyoshiriki uchaguzi vya ZNP, ZPPP na
ASP; lakini Shamte akamkatalia katakata
akisema: “Uhuru maana yake si kugawana
mateka; hakuna mateka wa kugawana
hapa”, aling’aka na kumtaka avunje
Chama chake cha ASP.
Shamte alidai kuwa nafasi kama hiyo
ilitolewa mara mbili kwa Karume, mwaka
1962 na 1963, wakati wa mazungumzo ya
Lancaster House, pale viongozi wa ASP,
ZNP, ZPP na Umma Party, walipokutana
mjini London na Waziri wa Makoloni wa
Uingereza kuzungumzia mchakato wa
Katiba na Uhuru wa Zanzibar, lakini
(Karume) alikataa kwa matarajio kwamba
ASP kingeshinda “kwa kishindo”.
Moja ya makubaliano yaliyofikiwa na
vyama vyote katika mikutano yote miwili,
kuanzia na uliofanyika kati ya Machi 19 na
Aprili 6, 1962, na wa Septemba 20 – 24,
1964 ni Zanzibar kupata uhuru Desemba
10, 1963 chini ya Waziri Mkuu, na Sultani
kuwa Mkuu wa nchi, kama zilivyo sasa
Canada, Australia na New Zealand ambazo
pamoja na kwamba zilipata uhuru kutoka
kwa Waingereza, lakini ziliendelea kubakia
kuwa chini ya himaya (monarch) ya Malkia
wa Uingereza.
Ndiyo kusema, kwa makubaliano hayo,
hata kama ASP kingeshinda, kisingeweza
kubadili mfumo huo. Wakuu wa ASP
wamedai mara nyingi kwamba walikubali
mfumo huo kwa matarajio wangefanya
mapinduzi baadaye. Lakini je,
ingewezekanaje wakati wao wenyewe
walikuwa watii kwa Serikali na waoga wa
umwagaji damu?
Katika hali ya kukata tamaa, Karume
alisema, “Inshallah, Mungu yupo, siku
moja nasi atatutunuku ushindi”; kisha
akaendelea kuwataka vijana wa ASP
wasifanye vurugu wala kuichokoza Serikali
isije ikapata kisingizio cha kutumia nguvu
ya ziada kwao na Chama cha ASP.
Kwa mawazo ya Karume na wenzake,
ilikuwa bora kuendeleza mapambano hadi
ushindi kwa njia ya sanduku la kura kwa
kujizatiti zaidi katika uchaguzi unaofuata.
 
Wakati Tunasherehekea siku ya mapinduzi Zanzibar yaliyofanyika January 12,1964,Mapinduzi hayo ya Zanzibar yamenifanya nimkumbuke Mwanamapinduzi Field Marshal John Gideon Okello aliyetoa mchango mkubwa katika mapinduzi hayo yaliyoleta Ukombozi wa Zanzibar pamoja na kwamba walikuwa na zana duni sana,Field Marshal Okello aliweza kuwashtukiza polisi na waliweza kuchukua madaraka.
Field Marshal Okello hakupaswa kusahaulika katika nchi zote mbili yaani Uganda na nchi aliyoikomboa ya Zanzibar,Kitu cha mhimu sana jamaa na ndugu za Field Marshal Okello wanaishi katika maisha ya ufukara na umaskini mkubwa sana wakati wa vita vya Kagera nimewahi kufika katika kijiji chake alikozaliwa na baadhi ya Wanajeshi tuliokuwa nao tulipenda sana kuwaona ndugu na jamaa za Mwanamapinduzi huyo.Tuliweza kufika katika kijiji cha Iyama huko Moroto, Tuliikuta familia ya Field Marshal Okello inaishi maisha ya kimaskini kabisa Utafikiri familia hiyo haijafanya chochote tulikaa pale kwa siku nzima na mimi nilibahatika kupata kitabu alichokiandika field marshal okello kiitwacho Revolution in Zanzibar kitabu hicho kinaelezea mengi sana kuhusiana na mapinduzi hayo ya Zanzibar kuna sehemu field marshal john okello aliandika; , “ I understand African thinking and I understand that what I did in Zanzibar, had it been done in any other country for the sake of Africans, I would still have been judged wrong and borne blame. But I acted alone during the revolution and had to remain alone afterwards. If anyone can claim he was with me during the planning and thinking through of the Revolution, let him come forward and explain it” Okello then went on by saying that “ Only God almighty knows what went on in Zanzibar. If anyone claims to have trained me or taught me to act as I did, let him come forward and describe it. I had been an ordinary worker in Zanzibar and went originally to work. A man of class and limited education certainly could not have gone abroad easily and why should I have known by or been acceptable to, and nothing proves this more than the wild claims made about me after the revolution and yet no one knew anything about me at all. I was reported to be a jaluo man from Kenya and a former member of Zanzibar police, yet a check of records in Zanzibar would not reveal my name on any police employment rolls, other people claimed they had seen me in Cuba and in Cairo and in some socialist countries. But there has been any evidence to refute any claims that I have never been outside East Africa to assert that I was an agent of some power, is foolish. How would anyone known I could manage revolution? And why did no one know me after the revolution?
God alone knows and still knows what is happening with me. He is my teacher and whatever he taught me about revolutionary activities is within me and no one on earth can discern it. My power in regard to the revolution was as a messenger of God, and God alone helped to master and eradicate the imperialists on the Island. Tulipigwa na butwaa kuona familia ya mwanamapinduzi huyo kuishi maisha kama hayo ya shida wakati yeye alifanya kazi kubwa ya ukombozi wa Zanzibar
Historia yake
Field Marshal John Gideon Okello alizaliwa mwaka 1937 huko wilaya ya Lango sasa hivi ni Lira Alipokuwa kijana ni mambo machache sana yanayofahamika kuhusiana na maisha yake hata hivyo Field Marshal John Gidion Okello alikuwa Mkristo na alibatizwa akiwa mdogo na jina lake la Ubatizo aliitwa Gidion,alipofikisha miaka 11 wazazi wake walifariki na alilelewa na ndugu zake wa karibu.
Alipofikisha miaka 15 alianza kutembelea nchi mbali-mbali za Afrika mashariki kutafuta kazi na kuna wakati alifanya kazi ya ukarani na kazi za nyumbani na shambani,pia alifundishwa kazi ya kutengeneza matofari ya kuchoma,kuna kipindi alikamatwa na Polisi huko Nairobi,Kenya sababu haikujulikana na alifungwa miaka miwili na katika kipindi hicho alipendezwa sana na Fikra za kimapinduzi vile vile kulikuwa na fununu kuwa Okello alikuwa ameishi Cuba na alifundishwa Ukominist na Fidel Castro
Mwaka 1959 aliondoka na kuelekea Pemba ambako alijaribu pia kutafuta kazi katika shamba moja,lakini badala yake alipata kazi ya Polisi na mwaka huohuo alijiunga na chama cha Afro-Shirazi cha Sheikhe Abeid Karume na akawa mwanaharakati shupavu aliweza pia kuwakusanya vijana na kuwaunganisha ili kupinga unyanyasaji wa waarabu huko visiwani. chama hiki kilikuwa kinapinga ukiritimba wa waarabu katika visiwa vya Zanzibar na Pemba.
Mwaka 1963 Okello aliondoka Pemba na kuelekea Zanzibar, Ambako alikutana na viongozi wa vijana wa Afro-Shiraz Umoja huo wa vijana wa Afro-Shiraz ulikuwa na mikakati ya kufanya mapinduzi ili kuondoa nguvu ya Waarabu huko Zanzibar,Okello pia alikuwa mwanachama wa chama cha wapaka rangi majumba maana naye siku ambazo hakuwa na kazi ya kufanya alikuwa anafanya kazi ya kupaka majumba rangi pia aliunda kikosi kidogo cha wazalendo kilichokuwa kinadhamini U-afrika kikosi hiki kilikuwa na miiko ya kutofanya mahusiano na wanawake,Kutokula nyama na kutokunywa pombe
January 12, 1964,akiwa na kikosi chake cha watu zaidi ya 600 Kwa kuungwa mkono na jamii ya visiwa waliokuwa wananyanyaswa na waarabu,Okello na kikosi chake walipigana kuelekea mji mkuu wa Zanzibar ambako Sultan alikuwa akikaa pamoja na kwamba walikuwa na zana duni,Okello na kikosi chake walilishtukiza Jeshi la Polisi la Zanzibar na kuweza kuteka silaha nyingi na ghala la silaha lilikuwa chini yao hivyo waliweza kuchukua madaraka,Wakati wa kutangaza mapinduzi hayo kwa njia ya Radio Okello alijitangaza mwenyewe kuwa yeye ni Field Marshal wa Zanzibar na Pemba na alimpa Sultan Amri ya kuwauwa familia yake na baadaye ajiue yeye mwenyewe la sivyo Okello angewauwa yeye mwenyewe,Hata hivyo Okello alikuwa amechelewa maana Sultani alikuwa amekimbilia kwenye meli ya Uingereza lakini waziri mkuu na mawaziri wengine hawakuweza kutoroka walikamatwa na walifungwa miaka mingi.Katika mapinduzi hayo zaidi ya waarabu 20,000 waliuliwa hasa hasa waliokuwa Zanzibar kati ya January 18 na 20, 1964.
Field Marshal John Gideon Okello aliunda Baraza la mapinduzi na alimchagua kiongozi wa Afro Shiraz Abeid Karume kuwa Rais na Sheikhe Abdulrahman Muhamad Babu kuwa waziri Mkuu,Kipindi hicho Karume na Babu walikuwa wanaishi Tanganyika,Na hawakujulishwa mapema kuhusiana na mapinduzi hayo, lakini walienda Zanzibar baada tu ya kukaribishwa na Okello.
Kuna habari pia kuwa Karume alikuwa anajua kutatokea nini maana alijulishwa na Field Marsha Okello kuwa wanampango wa kufanya mapinduzi hapo 12/01/1964 hivyo aliwataka viongozi wa juu wa Afro Shiraz Party kuondoka Zanzibar ili kama Zoezi litashindikana basi viongozi hao wawe salama na asiwepo wa kuwahisi kuwa walikuwa wanajua njama hizo za Mapinduzi.
Kufikia January 3,1964 Zanzibar ilirudia hali yake ya kawaida na Karume alikuwa amekubalika na jamii kuwa Rais,Field Marshal John Okello aliunda kikosi cha Jeshi kilichokuwa kikiitwa Freedom Military Force(FMF)kutoka kwa vikosi vilivyokuwa vikimuunga mkono ambavyo vilianza kufanya doria mitaani na sehemu zingine mhimu baada ya mapinduzi kupita okello aliweza kusafiri kwenda dar-es-salaam aliporudi alikuta hali si nzuri kwake askari wake walikuwa wameanza kupokonywa silaha hii iliashiria kuchafuka tena kwa hali ya hewa kwa Field Marshal John Gideon Okello.
The People's Liberation Army (PLA)Jeshi la Ukombozi wa wananchi liliundwa mwezi April 1964 na lilikamilisha kazi ya kuwapokonya silaha askari wote wa Okello,Tarehe 26/04/1964 Karume alitangaza kuwa amefanya mazungumzo ya kuingia kwenye Muungano na Tanganyika na kuunda nchi moja ya TANZANIA Haikuweza kujulikana mapema ni nini ilikuwa nia ya Karume kuingia kwenye Muungano huo lakini wengi walisema Karume aliingia kwenye muungano na Tanganyika ili kuwazuia watu wenye siasa kali toka chama cha Umma wasichukue nchi au kupunguza uwezekano wa kuwavutia wakominist katika afrika mashariki. Na wengine walihisi kuwa kwa sababu Field Marshal John Okello na karume kulikuwa na sintofahamu kati yao ndiyo maana aliamua kufanya muungano na Tanganyika ili asichukue madaraka tena toka kwake.kwa ujumla okello alikumbana na shida nyingi sana baada ya mapinduzi hayo.
Tatizo lingine alilopata ni kutokana na Dini yake yeye alikuwa Mkristo na ASP yote walikuwa Waislam hivyo alionekana mbele yao kama KAFIR hivyo hakusitahili kuongoza waislamu, wengine walihisi hivyo ndiyo maana jeshi lake lilipokonywa silaha na wafuasi wa Karume na wale waliotoka chama cha Umma,Na baada ya yeye kwenda Tanganyika aliporudi kwenye uwanja wa ndege Sheikh Karume alimwita Okello na kati ya mambo yaliyozungumzwa ni ya yeye kukataliwa huko visiwani hakuruhusiwa kuongea na yeyote,baadaye mamlaka ya mapinduzi walimzuia kuingia Zanzibar na inasemekana sheikh karume aliongea na nyerere ili naye oangee na rafiki yake obote asimruhusu okello kurudi Zanzibar tena.
Baadaye Okello alikaa Kenya,Congo-Kinshasa mwishowe Uganda alikuwa akizunguka katika nchi hizi mara kwa mara mwaka 1971 alionekana akiwa na Rais wa Uganda Idd Amin baadaye alitoweka maana Idd Amin hakupendezwa nayeye Okello kujiita Field Marshal maana alijiuliza watakuwa ma-Field Marshal wangapi Uganda hata hivyo Amin hakumwamini alimwona kama ni kitisho katika utawala wake hivyo inasadikiwa Idd Amin aliamua kummaliza mwaka 1971 baada tu ya kuchukua madaraka toka kwa Rais Obote.
 
Tunapoelekea kwenye kilele cha sherehe za Mapinduzi ningependa tujiulize swali hilo ambalo limekuwa na mkanganyiko sana kutokana na Itikadi mbalbal za watu. je baba wa Taifa la ZANZIBAR NI NANI KATI YA HAWA?
(a)John Okelo
(b)Abeid Karume
(c)Sultani bin Said
 
Back
Top Bottom