wambura marwa
JF-Expert Member
- Mar 7, 2015
- 2,172
- 1,128
yaani nachanganyikana vile uhuru bandia je siku ya mapinduzi nani alipinduliwa?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Big Gift,Waafrika wanapenda kujitwalia masiwa ili waonekane mashujaa bana.
Marekani alisema hadharani uhuru wao mwaka 1776 ulipatikana kwa msaada wa wafaransa kuondoa utawala wa waingereza.
Afrika hii na sehemu nyingine duniani ni ngumu mambo kama hayo kufanyika.
Marehemu mtikila aliwahi kumsema vibaya kagame kuwa ana koloni lake DRC na rais wa huko yani joseph kabila ni mtutsu wala sio mtoto halisi wa marehemu/rais wa zaman laurent desire kabila na ni kweli huyu bwana amekua mgumu sana kupima DNA ili itambulike ukweli hapo nimeshuhudia mwenyewe so hapa na muunga mkono mtikila
Pia mtikila huwa alikua anapenda sana kusema nchi ya tanganyika huenda alikua hautambui huu muungano na kuna sababu zake za kutoutambua.
Alikua hamtambui Nyerere kama baba wa taifa, alikua anamuona ni mtu wa kawaida tuu, hapa nako alikua na sababu zake.
sasa mimi naweza kusema malipo ni hapa hapa dussanyahG niani kwa sababu okelo alifukuzwa kama mbwa zanzibar kilichomkuta marehemu karume mnakijua hata sitaki kuongea sana. ila what goes around comes around. wangemlipa haki yake kwa shuhuli aliyoifanya na Mungu angeshusha baraka zake nyingi tuu zanzibar.
Waafrika wanapenda sana kuonekana mashujaa kumbe hamna lolote ila kwa kuwa hao viongozi walikua na nia njema na nchi zao basi ni heri kuliko wangelikua wana nia mbaya ya kujitwalia madaraka.
auakweli utabakia okelo ndie shujaa wa mapinduzi ya zanziba.
naadika kwa uchungu sana kuhusu unyama aliofanyiwa ila Mungu anaona.
mkuu naomba unitumie pdf hiko kitabu nifanye upembuzi wangu,Big Gift,
Mimi naweza nikafanya mjadala wa Okello na nafasi yake katika Mapinduzi ya Zanzibar
1964.
Kiitabu kilichoandika historia ya kweli ya mapinduzi ni kitabu cha Dr. Harith Ghassany,
msomi wa Harvard na ni Mzanzibari.
![]()
Mohamed Omari Mkwawa akionyesha kitabu, nyumbani kwa Mwandishi Tanga 2010
Kitabu chake kinaitwa, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' (USA 2010).
Dr. Ghassany alinichukua mimi kama Mtafiti Msaidizi.
Kwa ajili hii nina mengi kuhusu Okello na ambalo ninaloweza kukwambia ni kuwa hakuwa
shujaa wa mapinduzi.
Nakushauri ufungue uzi mwingine In Shaallah tujadili.
![]()
Mwandishi na Dr. Harith Ghassany
Big Gift,mkuu naomba unitumie pdf hiko kitabu nifanye upembuzi wangu,
Nashukuru mkuu.
Big Gift,Nashukuru mkuu.
Havanna,Inasemekana ndio alikuwa masterminde wa revolution ila kutokana na kuwa mganda aliondoka/alifukuzwa na wenye nchi
Havanna,Mmh basi vitabu nilivyovisoma vyote wameelezea kuwa ndio sababu mojawapo ya mapinduzi
Asante kwa kuniongezea chakula cha ubongoHavanna,
Wenye mapinduzi yao wanasema walimvisha Okello blanketi na
likamwenea na akawa, ''Filed Marshal,'' na yeye mwenyewe kwa
ujinga aliokuwanao akaamini kweli yeye ni, ''Field Marshal.''
Yaani yeye na Field Marshal Josip Broz Tito aliyeongoza jeshi
la Partisan, Yugoslavia wakati wa Vita Vya Pili Vya Dunia dhidi ya
Hitler vyeo vyao ni sawa.
Hakujua kama yeye ni, ''Field Marshal,'' wa Mamluki wa Kimakonde
kutoka mashamba ya mkonge ya Sakura na Kipumbwi kutoka
Tanga.
Historia za viongozi wa Afrika zina matatizo makubwa sana.
![]()
Kushoto Dk. Harith Ghassany na Mohamed Omar Mkwawa wakati wa utafiti wa kitabu, ''Kwaheri Ukoloni
Kwaheri Uhuru.''
Havanna,Asante kwa kuniongezea chakula cha ubongo