Uchaguzi 2020 Mapingamizi halali kisheria dhidi ya mgombea nafasi ya Urais

Mbona mnatia huruma hivyo! Lissu tunamkatafunua kwenye sanduku mapema sana ili azidi kuchanganyikiwa! TL hawezi kuwa Raisi wa Tanzania, labda awe raisi wa Twitter.
Mkate kwenye sanduku kwa haki..no problem ndio demokrasia hiyo..nini povu sasa?

Kama unatumia demokrasia kumkata kwenye sanduku,then it is right!

Mengine ni ya uungu mtu mnatuletea hapa....yaani Tume ipo chini yenu,hakuna nchi hapo!
 
So na ujanja wako wote huo unasubiri hayo yatokee kisha ukakojoe ukalale badala ya kuja na mechanism ya kukabiliana na huo uhuni.
Mkuu

Mawe yupo juu ya sheria

Tume iko chini yake.....Mahakama iko chini yake....

Huyu dikteta alipokua anaua hizi institutions kua chini yake watu wazima nchi hii walikua wanapiga makofi...

Ujanja wa ku-overcome hili ni hizi kelele zinazopigwa na Amsterdam,pia lazima elders wa hii nchi waongee wazi wazi na mengine mengi
 
Mapingamizi namba 4 na 5 yanavunja misingi ya haki ya Watanzania kuchaguliwa uongozi.

Nafikiri hata Ripoti ya Jaji Nyalali ilishauri tuondoe sharti la wagombea kuwa wanachama wa vyama vya siasa.
Serikali ilishashindwa kesi na walipewa muda kurekebisha hicho kipengele ila hatuna watu kama mtikila kwa sasa
 
Mahakama ya Rufaa ilitengua uamuzi wa Mahakama Kuu, hivyo, Mtikila alipoteza kesi.
Mahakama ya afrika ilimpa ushindi na ikaipa muda serikali kutekeleza wakati huo tulikuwa na bunge la katiba wakasingizia kipengele hicho kimewekwa lakini tunajua mwisho wa bunge la katiba kwani hakuna kinachotekelezwa
 
Mahakama ya afrika ilimpa ushindi na ikaipa muda serikali kutekeleza wakati huo tulikuwa na bunge la katiba wakasingizia kipengele hicho kimewekwa lakini tunajua mwisho wa bunge la katiba kwani hakuna kinachotekelezwa
Mahakama ya Haki za binadamu ya Afrika haina meno ni toothless dogo.
 
Elder aliyekuwa anasikilizwa na Magufuli ni Mkapa peke yake, wengine wote walishaambiwa wanawashwawashwa.
 
Watamkata na Hashimu Rungwe ili kuonyesha sio Lisu pekee
 
Nasikia CCM wameongezea la kwao kwamba
1. Lissu kaanza kampeni mapema
2. Lissu katoa maneno ya uchochezi wakati wa kutafuta wadhamini...
3. Kufanya maandamano na mikutano ya hadhara bila mufuata taratibu za kisheria.

Haya ndiyo makosa ya Lissu according to Lumbumba yanayomuondolea sifa ya kugombea Urais wa Jamhuri yetu.
 
#15! Utawekaje pingamizi wakati hajaanza kuzitumia gharama za uchaguzi!
 
Kiwekwe kipengele cha kuwapima Mental health wagombea
Madikteta wengi huwa wanamatatizo hayo na ni vigumu wao kuyakubali kuwa ni matatizo

Mathalan huyu anaeondoka madarakani
 
Hapo namba 15 inaondoka na lisu.
Si mlisema Lisu hana pesa za kampeni CHDEMA imteuwe Nyalandu?! Au ameshapata pesa? Alafu muulize Lijualipole, si Mbowe amekula ile pesa ya kampeni bilion ngapi sijui!! Number 15 haiwezi, na wala mboga mboga yeyote mwenye akili kisude tu, hatadhubutu kuitumia kumwekea Lisu pingamizi! Kwanini msiseme ni Mkenya, aliongezewa damu na Wakenya!!
 
Tatizo lako ni mtu wa matukio hukui nini kilifata baada ya mahakama ya rufani kutengua uamuzi huo ingia hata google tafuta hukumu ya mgombea binafsi Tanzania utapata mwendelezo

Mimi sijui naomba unielimishe kuhusu bindingness nature na execution ya hukumu ya Mahakama ya Haki za binadamu ya Afrika.

Je serikali ya Tanzania ikikataa kuheshimu hukumu ya Mahakama ya Haki za binadamu inaweza kuchukuliwa hatua gani za kisheria?

Naomba unielimishe kuhusu haya maswala mawili.
 
Tunataka vifungu vya sheria Kama hivi. Hongera sana mleta maada. Sio watu mnabishana Mambo ya kisheria halafu hamna kifungu chochote mlicho note
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…