Kenya 2022 Mapingamizi ya uchaguzi wa Rais Kenya: Yanayoendelea Mahakama ya Juu

Kenya 2022 General Election
Kama kawaida, mikikimikiki haikosekani kwenye matukio kama haya🙂
"MAPEMA: Mwanaharakati mwenye utata Julius Kamau alifurushwa na walinzi kutoka Mahakama ya Juu baada ya kuvamia ukumbi na kusababisha fujo wakati wa kongamano la kesi."

 
Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Githu Muigai kuwakilisha IEBC katika kesi ya kesi ya uchaguzi.
 
Kesi ni nzito. Lets wait and see
Hakuna kesi hapo. Odinga hana ushahidi wowote, hoja 9 alizowakilisha ni kutaka tume ithibitishe kuwa njia walizotumia kufikia matokeo hazitoi mwanya wa kufanyika udanganyifu.

Hawana ushahidi wa wizi wa kura. Ni kama tu wanataka kura zihesabiwe upya.

Majaji wanatakiwa kutupilia mbali hii kesi, Haina foundation!
 
Yani unasema kesi haina foundationa na wakati huo huo kuna jopo la majaji saba wanaketi kusikiliza 'kesi isiyokuwa na foundation'.Inaelekea Mkuu una ufahamu mkubwa sana wa hii kesi kuliko Koome na jopo zima la majaji wa SCOK.Tupunguzeni ujuaji tuwaachie magwiji wa sheria pale Mahakama ya Upeo wafanye maamuzi sahihi ya kile kilichopelekwa hapo.
 
Yani unasema kesi haina foundationa na wakati huo huo kuna jopo la majaji saba wanaketi kusikiliza 'kesi isiyokuwa na foundation'.Inaelekea Mkuu una ufahamu mkubwa sana wa hii kesi kuliko Koome na jopo zima la majaji wa SCOK
Hapana dada yangu mpendwa, Kila mtu ana haki ya kusikilizwa.

Wanachofanya majaji ni kutoa haki ya kumsikiliza Odinga, ametaka baadhi ya vituo kura zihesabiwe tena wamemkubalia. Hana ushahidi ni kama anabahatisha bahatisha tu.

Utaniambia mwisho wake, Ukuniwila, ango?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…