Mapokezi ya Tundu Lissu: Jeshi la Polisi na Viongozi wa CHADEMA wana wajibu wa kutunza utulivu

Mapokezi ya Tundu Lissu: Jeshi la Polisi na Viongozi wa CHADEMA wana wajibu wa kutunza utulivu

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,767
Reaction score
288,340
MAPOKEZI YA TUNDU LISSU: JESHI LA POLISI NA VIONGOZI WA CHADEMA WANA WAJIBU WA KUTUNZA UTULIVU

1595809260163.png

Tarehe 6 Novemba 2005 nilirejea nchini na British Airways kutokea Heathrow, London, Uingereza nikiwa na mke wangu na mtoto wetu wa kiume baada ya kuishi nje ya nchi kwa miaka kadhaa. Huku Tanzania tuliacha timu kubwa ya watu ambao kabla nilikuwa nikiwaongoza katika huduma za watoto, shule na vijana kupitia Umoja wa Kujisomea Biblia (Scripture Union of Tanzania). Wao waliniona mimi kama kiongozi wao na mimi nilijihisi hivyo.

Siku hiyo tulipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere, tulishangaa kukuta umati wa vijana wale wamekuja kutupokea! Furaha na fahari yao ilikuwa ni kumpokea kiongozi wao! Familia ilipisha maandalizi na ratiba yao. Hakukuwa na haja ya kuomba kibari kutoka kwa RPC, OCD, RC, DC wala Meneja wa Uwanja wa Ndege! Simba au Yanga wakitoka mbali kucheza mpira nao hupokelewa na washabiki wao.

Tundu Lissu aliondoka nchini pasipo kuaga na wala hakupenda kuondoka. Mazingira ya kuondoka kwake yalihuzunisha wengi akiwemo Rais ambaye alitoa pole kwake na kumtakia apone haraka. Watu wengi walishiriki kumuombea hata wasiomjua.

Sasa anarejea nchini baada ya kupona! Ndugu zake, rafiki zake, wanachama wenzake na hata watu wengine wasio wanachama wanayo hamu ya kumuona na kumpokea. Lissu sio mhaini. Ni raia wa Tanzania mwenye dhamana ya Uongozi katika Chama chake. Anayo haki ya kupokelewa na mtu ye yote na kupita katika barabara zilizojengwa kwa kodi za Watanzania akiwemo yeye mwenyewe.


Wakati Nyerere anarudi kwao Butiama baada ya kustaafu Urais au kung'atuka, mimi nilikuwa mkazi wa Kipawa. Tulijipanga barabarani kumuaga na wala yeye hakusimama kutuhutubia! Nelson Mandela alipokuja mwaka 1990, mimi nilikuwa mkazi wa Temeke. Tulitoka kila kona ya jiji pasipo kujali mvua kubwa siku ile, tulijipanga barabarani na wala hakutuhubia zaidi ya kufurahia upendo wetu kwake!

Vivyo hivyo, kama watu watajitokeza kumpokea Lissu ni haki yao, ni hiari yao, ni uhuru wao, ni mapenzi yao. Wanachotakiwa kufanya ni kuepuka kuwabugudhi wengine au kufanya vitendo vya uhalifu na uvunjifu wa amani.

Viongozi wa CHADEMA wawe makini, wasiruhusu kufanya mkutano wa hadhara pale Uwanja wa Ndege. Watu wasizuie barabara ingawa wanaweza kukaa pembeni mwa barabara. Watu wasizuie wasafiri wengine pale Uwanjani. Polisi wanaweza kuwepo kulinda usalama lakini sio kuwazuia watu wasimpokee kiongozi wao.

Jeshi la Polisi liepuke kufanya jitihada au maandalizi ya kimkakati kwa lengo la kutaka kuwazuia au kuwatawanya watu wanaokwenda kumpokea kiongozi wao kwa amani. Kufanya hivyo ni kuamsha hisia za watu pasipo sababu ye yote ya msingi. Jeshi la Polisi na Uongozi wa CHADEMA waonyeshe nia njema kwa kushirikiana katika kutunza utulivu na amani siku hiyo.

Katika kipindi hiki ambapo nchi iko katika maombolezo, ni vizuri wote wakiwemo Jeshi la Polisi, viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao kuenzi utamaduni wa maombolezo kwa kuwa watulivu. Tahadhari ya Jeshi la Polisi kuhusu 'kusanyiko' la kumpokea Lissu ni muhimu kiusalama, lakini isilenge katika kutaka kuwazuia wala kuwatawanya watu. Jeshi la Polisi lisiwachokoze watu ambao hawajaonyesha dalili za kufanya vurugu! Uwanja wa Ndege siyo sehemu ya kufanyia mikutano ya hadhara! Hivyo haitarajiwi pia kama Lissu ataanza kuhutubia watu mahali pale kama hakuna maandalizi na mawasiliano na mamlaka husika.

NB: Nimeweka picha iliyoandaliwa na JamiiForums ambao ndio waliotoa taarifa kuhusiana na tukio hilo. Picha hiyo imebeba ujumbe wa Jeshi la Polisi kuhusiana na tukio hilo.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian Ia Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani
 
BAK,

Umenena vyema kabisa Baba Askofu Mwamakula.

Ninaamini kabisa kuwa viongozi wa Chadema wataupokea kwa mikono miwili ushauri huo mzuri

Wasiwasi wangu ni ushauri huo namna utakavyopokelewa na hawa watawala wetu, kwa kuwa wao wanaamini kuwa "wanamiliki" chombo cha dola cha Jeshi la Polisi na wana uwezo wa kuliagiza Jeshi hilo la Polisi, kufanya kitu kinyume cha Katiba kwa kuwazuia mashabiki wa Chadema kutoweza kumpokea shujaa wao Tundu Lissu, hapo ndipo watakapoleta vurugu kubwa.
 
Ni ujumbe mzuri.

Polisi wao wamekwishatoa msimamo wao hasi kuhusu mapokezi ya Tundu Lissu. Hiyo taarifa tayari ipo hapa mtandaoni.

Polisi wanakazia "kutokiukwa kwa sheria", pamoja na kwamba hawataji vifungu vya sheria vinavyohusu mapokezi ya wageni hapo uwanjani. Kwa hiyo ni wao pekee ndio wanaozifahamu sheria hizo wanazotaka zisikiukwe.

Kama tujuavyo, inapotolewa taarifa ya kijumla kama hivyo, maana yake ni kwamba wao polisi watatumia njia kuhakikisha kwamba wanaofika hapo kwenye mapokezi watasababishwa waonekane wanavunja sheria kwa njia mbali mbali.

Mamluki wanaweza kupandikizwa kati ya watu ili kuanzisha vurugu maksudi kuwapa nafasi polisi kisingizio cha kutawanya watu. Hili linajulikana vyema katika hali ya nchi yetu iliyopo sasa. Kuna mifano ya matukio ya namna hii yaliyosababisha viongozi wa CHADEMA kutiwa hatiani.

Kwa hiyo, ni vigumu sana kusema viongozi wa CHADEMA washirikiane na polisi kuhakikisha vurugu toka kwa washabiki wao hazitokei. Ni kuwaonea tu CHADEMA, kwa sababu hawana uwezo wa kuzuia mambo mabaya yaliyopangwa yasitokee.
 
Askofu wangu wa kikatoliki anasubiri sadaka yangu jumapili huu ubaya wa polisi hutasikia wakiukemea aibu na Iwe juu yenu.
Mkk 'super', sijui kama kazi ya Askofu wa kikatoliki kweli ni "kusubiri sadaka"; lakini ninakubaliana na wewe kuhusu ukimya wake(wao) juu ya "ubaya wapolisi na kutoukemea."

Lakini kama sikosei utaratibu katika kanisa hilo juu ya nafasi ya walei na waumini wa kawaida..., ni nini mchango wao katika kuonyesha wasiwasi wao juu ya hali ya nchi, na kulazimisha viongozi wa kanisa nao wauwekee umhimu?

Kiufupi nauliza tu: wewe na waumini wenzako mmeonyesha wasiwasi wowote na kulifikisha swala hilo kwa viongozi wenu? Wewe huna mchango wowote katika ukimya unaoonyeshwa na Askofu wako?

Sababu iliyokufanya uingie na kuwa muumini wa kanisa hilo sio kumfurahisha Askofu kwa michango/sadaka unayotoa kanisanai. At least huu ndio uamini wangu. Pengine wewe unaamini tofauti na mimi mkuu 'burg' na mkuu mwingine kule chini 'Pythagoras', ambaye pia yupo kwenye hali kama uliyo nayo wewe.

Nimalizie tu kwa kusema haya machache:
Sijui ni jambo gani waliloambiwa hawa viongozi wa dini wakati ule walipokutana na mkuu wa nchi, na hasa baada ya ule waraka wa Pasaka walioutoa.

Sijui kama walipewa vitisho vikali sana kiasi kilichowafanya ule msimamo waliokuwa wameanza nao kwenye ule waraka uwe ni batili moja kwa moja. Siamini kamwe kwamba kuna vitisho vinavyoweza kufanywa dhidi yao na kubadili mwelekeo juu ya kile walichokuwa wamekizungumzia.

Kama waliahidiwa mabadiliko, hayo mabadiliko sikuyaona yakitokea kuwa na unafuu toka kwenye ile hali waliyoizungumzia mwanzo.

Mwenye kujua sababu za mabadiliko, bila shaka ataeleza hapa.
 
Polis Leo wanahitajika kuwepo airport kulinda usalama Wa watu na sio kuwatawanya watu, waziri Wa mambo ya ndani awe makini na utendaji wa jeshi la polisi.
 
Asante sana Askofu Mwamakula. Ningependa sana na wewe leo uwepo kumpokea shujaa wetu Tundu Antipas Lissu
 
CHADEMA

Ujio wa Lissu ni karata yenu ya mwisho, mkiitumia vyema itawarudishia heshima na mkiitumia vibaya itawaangamiza na kuwafuta katika ramani ya siasa Tanzania na Duniani.

Waswahili wanasema "ngoma ikilia sana hupasuka" na "debe tupu ndilo linalovuma sana"

Jumatatu ni leo.
 
Mkk 'super', sijui kama kazi ya Askofu wa kikatoliki kweli ni "kusubiri sadaka"; lakini ninakubaliana na wewe kuhusu ukimya wake(wao) juu ya "ubaya wapolisi na kutoukemea."

Lakini kama sikosei utaratibu katika kanisa hilo juu ya nafasi ya walei na waumini wa kawaida..., ni nini mchango wao katika kuonyesha wasiwasi wao juu ya hali ya nchi, na kulazimisha viongozi wa kanisa nao wauwekee umhimu?

Kiufupi nauliza tu: wewe na waumini wenzako mmeonyesha wasiwasi wowote na kulifikisha swala hilo kwa viongozi wenu? Wewe huna mchango wowote katika ukimya unaoonyeshwa na Askofu wako?

Sababu iliyokufanya uingie na kuwa muumini wa kanisa hilo sio kumfurahisha Askofu kwa michango/sadaka unayotoa kanisanai. At least huu ndio uamini wangu. Pengine wewe unaamini tofauti na mimi mkuu 'burg' na mkuu mwingine kule chini 'Pythagoras', ambaye pia yupo kwenye hali kama uliyo nayo wewe.

Nimalizie tu kwa kusema haya machache:
Sijui ni jambo gani waliloambiwa hawa viongozi wa dini wakati ule walipokutana na mkuu wa nchi, na hasa baada ya ule waraka wa Pasaka walioutoa.

Sijui kama walipewa vitisho vikali sana kiasi kilichowafanya ule msimamo waliokuwa wameanza nao kwenye ule waraka uwe ni batili moja kwa moja. Siamini kamwe kwamba kuna vitisho vinavyoweza kufanywa dhidi yao na kubadili mwelekeo juu ya kile walichokuwa wamekizungumzia.

Kama waliahidiwa mabadiliko, hayo mabadiliko sikuyaona yakitokea kuwa na unafuu toka kwenye ile hali waliyoizungumzia mwanzo.

Mwenye kujua sababu za mabadiliko, bila shaka ataeleza hapa.
Wajibu wangu Kama mlei ni huu nilioufanya wa kuandika hapa mpaka wewe umereact.

Pili viongozi wa kanisa katoliki Tanzania Wana mafungamano yasiyo mema kwa taifa na gvt imagine mtu anapigwa risasi 32 kina Ben Saanane wamepotea wao wako kimya ila kwenye madhabahu wanawakaribisha wanasiasa kuinajis altare wakiomba tuwaombee eti wako kwenye Vita ya kiuchumi jinga kabisa my bishops.
 
Binafsi naamini Jeshi la Polisi lenyewe na polisi wake hawana matatizo kabisa....

Tatizo ni kuwa hizi taasisi za kiusalama (JWTZ, TISS, Polisi wote nk) hutekeleza majukumu yao kwa kutii amri tu toka juu kwa "superiors officers" wao...

Hawa maafisa "superiors" ndiyo tatizo. Wengine ni makada wa vyama vya siasa hususani chama kinachoongoza serikali ambacho kwa sasa ni CCM...

Hawa maafisa "makada" wa chama tawala, wamewekwa ktk nafasi hizo kimkakati. Wanatekeleza amri za jeshi kimkakati kulinda na kukitetea chama chao na lolote linaloweza kufifisha umaarufu wa chama na serikali...

Hawa maskari na maafisa wadogo wadogo wa ngazi za chini wakati mwingine wanakuwa hawana la kufanya bali KUTII na KUTEKELEZA amri tu...

Hata tangazo la polisi la kuhusu kupiga marufuku watu kumpokea Tundu Lissu liko "so vague", halina misingi ya kisheria. Ni amri tu na lazima itekelezwe...

Kwa scenario hii, na kiuhalisia kama kutatokea uvunjivu wa amani wowote leo, chanzo hakiwezi kuwa RAIA wenye furaha kumpokea ndugu yao " aliyefufuka" baada ya kifo...

Chanzo kitakuwa ni polisi mwenyewe kwa maslahi ya wakubwa wao...!!
 
Back
Top Bottom