Mapokezi ya Tundu Lissu: Jeshi la Polisi na Viongozi wa CHADEMA wana wajibu wa kutunza utulivu

Mapokezi ya Tundu Lissu: Jeshi la Polisi na Viongozi wa CHADEMA wana wajibu wa kutunza utulivu

MAPOKEZI YA TUNDU LISSU: JESHI LA POLISI NA VIONGOZI WA CHADEMA WANA WAJIBU WA KUTUNZA UTULIVU

View attachment 1517994​

Tarehe 6 Novemba 2005 nilirejea nchini na British Airways kutokea Heathrow, London, Uingereza nikiwa na mke wangu na mtoto wetu wa kiume baada ya kuishi nje ya nchi kwa miaka kadhaa. Huku Tanzania tuliacha timu kubwa ya watu ambao kabla nilikuwa nikiwaongoza katika huduma za watoto, shule na vijana kupitia Umoja wa Kujisomea Biblia (Scripture Union of Tanzania). Wao waliniona mimi kama kiongozi wao na mimi nilijihisi hivyo.

Siku hiyo tulipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere, tulishangaa kukuta umati wa vijana wale wamekuja kutupokea! Furaha na fahari yao ilikuwa ni kumpokea kiongozi wao! Familia ilipisha maandalizi na ratiba yao. Hakukuwa na haja ya kuomba kibari kutoka kwa RPC, OCD, RC, DC wala Meneja wa Uwanja wa Ndege! Simba au Yanga wakitoka mbali kucheza mpira nao hupokelewa na washabiki wao.

Tundu Lissu aliondoka nchini pasipo kuaga na wala hakupenda kuondoka. Mazingira ya kuondoka kwake yalihuzunisha wengi akiwemo Rais ambaye alitoa pole kwake na kumtakia apone haraka. Watu wengi walishiriki kumuombea hata wasiomjua.

Sasa anarejea nchini baada ya kupona! Ndugu zake, rafiki zake, wanachama wenzake na hata watu wengine wasio wanachama wanayo hamu ya kumuona na kumpokea. Lissu sio mhaini. Ni raia wa Tanzania mwenye dhamana ya Uongozi katika Chama chake. Anayo haki ya kupokelewa na mtu ye yote na kupita katika barabara zilizojengwa kwa kodi za Watanzania akiwemo yeye mwenyewe.


Wakati Nyerere anarudi kwao Butiama baada ya kustaafu Urais au kung'atuka, mimi nilikuwa mkazi wa Kipawa. Tulijipanga barabarani kumuaga na wala yeye hakusimama kutuhutubia! Nelson Mandela alipokuja mwaka 1990, mimi nilikuwa mkazi wa Temeke. Tulitoka kila kona ya jiji pasipo kujali mvua kubwa siku ile, tulijipanga barabarani na wala hakutuhubia zaidi ya kufurahia upendo wetu kwake!

Vivyo hivyo, kama watu watajitokeza kumpokea Lissu ni haki yao, ni hiari yao, ni uhuru wao, ni mapenzi yao. Wanachotakiwa kufanya ni kuepuka kuwabugudhi wengine au kufanya vitendo vya uhalifu na uvunjifu wa amani.

Viongozi wa CHADEMA wawe makini, wasiruhusu kufanya mkutano wa hadhara pale Uwanja wa Ndege. Watu wasizuie barabara ingawa wanaweza kukaa pembeni mwa barabara. Watu wasizuie wasafiri wengine pale Uwanjani. Polisi wanaweza kuwepo kulinda usalama lakini sio kuwazuia watu wasimpokee kiongozi wao.

Jeshi la Polisi liepuke kufanya jitihada au maandalizi ya kimkakati kwa lengo la kutaka kuwazuia au kuwatawanya watu wanaokwenda kumpokea kiongozi wao kwa amani. Kufanya hivyo ni kuamsha hisia za watu pasipo sababu ye yote ya msingi. Jeshi la Polisi na Uongozi wa CHADEMA waonyeshe nia njema kwa kushirikiana katika kutunza utulivu na amani siku hiyo.

Katika kipindi hiki ambapo nchi iko katika maombolezo, ni vizuri wote wakiwemo Jeshi la Polisi, viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao kuenzi utamaduni wa maombolezo kwa kuwa watulivu. Tahadhari ya Jeshi la Polisi kuhusu 'kusanyiko' la kumpokea Lissu ni muhimu kiusalama, lakini isilenge katika kutaka kuwazuia wala kuwatawanya watu. Jeshi la Polisi lisiwachokoze watu ambao hawajaonyesha dalili za kufanya vurugu! Uwanja wa Ndege siyo sehemu ya kufanyia mikutano ya hadhara! Hivyo haitarajiwi pia kama Lissu ataanza kuhutubia watu mahali pale kama hakuna maandalizi na mawasiliano na mamlaka husika.

NB: Nimeweka picha iliyoandaliwa na JamiiForums ambao ndio waliotoa taarifa kuhusiana na tukio hilo. Picha hiyo imebeba ujumbe wa Jeshi la Polisi kuhusiana na tukio hilo.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian Ia Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani
Vyombo vya habari vya kimataifa huenda pia vikafuatilia ujio wa Lissu na kipi kinaweza kutokea katika mapokezi yake na hivyo kukitangaza katika vyombo vyao vya habari.
 
Nami naomba Amani itawale nchi yetu sote kusitokee mwenye kukusudia kuvuruga amani
 
Punguza jazba
Wajibu wangu Kama mlei ni huu nilioufanya wa kuandika hapa mpaka wewe umereact.

Pili viongozi wa kanisa katoliki Tanzania Wana mafungamano yasiyo mema kwa taifa na gvt imagine mtu anapigwa risasi 32 kina Ben Saanane wamepotea wao wako kimya ila kwenye madhabahu wanawakaribisha wanasiasa kuinajis altare wakiomba tuwaombee eti wako kwenye Vita ya kiuchumi jinga kabisa my bishops.
Punguza jazba maana haitakufaa kitu kwani huna unalolijua isipokuwa jina kubwa la kanisa katoliki. Maana naona ndio hoja yako dhaifu imejificha nyuma ya jina kubwa la kanisa katoliki.
 
Tumeona viongozi wakihimiza wananchi kwenda uwanja wa ndege kupokea ndege. Tumeona mamia ya watu wakienda uwanja wa ndege kupokea timu zao. Tumeona wakati wa misiba yaRuge na Mengi watu wakienda uwanja wa ndege na wengine kujipanga kando ya barabara kuwapokewa na hata wakati mwingine barabara kufungwa ili kupisha misafara hiyo.

Hiyo ni mifano michache tu ya mikusanyiko ya mapokezi ya furaha na huzuni pia na polisi hawajawahi kuizuia kwa kisingizio cha mikusanyiko isiyo halali.

Baada ya kutangazwa kurejea kwa Lissu na watu kuhimizana kwenda kumpokea tayari polisi wameibuka na kusema hawata ruhusu kwakuwa siyo mkusanyiko halali. Tangazo hilo la polisi maana yake ni kuwa wamejipanga kukabiliana na shamra shamra za mapokezi ya Lissu kwa mabomu na virungu na si ajabu kusikia watu wamejeruhiwa, kukamatwa, kuuawa na mali kuharibika. Kisa ni polisi hawataki kuona watu wanampokea Lissu.

Juzi juzi baada ya CCM kuchagua mgombea wao Zanzibar kulikuwa na maandamano ya kumpokea mitaani na kisha mikutano ya hadhara. Kwa polisi hiyo ni mikusanyiko halali kwa kuwa ni ya chama tawala.

Haileweki toka lini kumpokea ndugu au rafiki ikahitaji kibali cha polisi. Kisingizio kitakuwa ni msiba lakini je shughuli zote zimesimama? Watu hawafanyi kazi? Tubasubiri kuona busara ya polisi kama ipo.
 
Nina miaka 6 sasa sitoi na wala sitatoa sadaka yoyote. Pesa zangu nawapa maskini mkono kwa mkono sio kipitia mikono michafu

Mkuu bora hata ww hutoi sadaka, mimi hata kanisani siendi kabisa. Mambo ya mtu kuongea huku mishipa imemtoka kama anafanyiwa wiring, lakini akitoka hapo anafanya mambo ya ajabu, kisha anasema fuata maneno yake, wala usiangalie matendo yake! Kama hayo anayosema ni ya kufuatwa yeye kinamshinda nini? Shubaamit, maeoneo ya kwenda kulishana habari bila kuhoji, akili yangu imepiga marufuku.
 
Dakika 9 zilizopita,Lissu kaandika hivi kupitia twitter:

Boarding Ethiopian Airlines flight ET 805 from Bole International Airport Addis Ababa to Dar Julius Kambarage Nyerere International Airport now. Tukutane Dar in slightly over three hours-Tundu Lissu on twitter.

Wacha tuone nini kitatokea baada ya muda huo wa masaa 3.
 
If Magufuli and the CCM vegetables had adequate gray matter they should have used Tundu Lisu homecoming by extending and olive leaves and not sending the brutal Tanpol for attacking the those who would meet their leader at JKNIA people must be allowed to freely go !
 
Wanachi wanawapuuza sana. Sijui muwe mnatumia lugha gani wawaelewe.
 
Dakika 9 zilizopita kaandika:

Boarding Ethiopian Airlines flight ET 805 from Bole International Airport Addis Ababa to Dar Julius Kambarage Nyerere International Airport now. Tukutane Dar in slightly over three hours-Tundu Lissu on twitter.

Wacha tuone nini kitatokea baada ya muda huo wa masaa 3.
Natamani kujua kama utakuwepo JNIA Terminal 3 au ni mashabiki wa mitandaoni tu
 
If Magufuli and the CCM vegetables had adequate gray matter they should have used Tundu Lisu homecoming by extending and olive leaves and not sending the brutal Tanpol for attacking the those who would meet their leader at JKNIA people must be allowed to freely go !
Unakumbuka mwaka ule Magufuli aliwahi kusema atakayeandamana atapigwa kipigo kikal hadi aende akasimulie kwa baba yake.
 
Polis Leo wanahitajika kuwepo airport kulinda usalama Wa watu na sio kuwatawanya watu, waziri Wa mambo ya ndani awe makini na utendaji wa jeshi la polisi.

Kwa jeshi la polisi linalofanya kazi kama robots, usitegemee weledi wowote. Wao wameagizwa na kiongozi wa kisiasa wa chama kinachogawa rushwa kama njugu huko kwenye kura za maoni, hawana chochote cha kujiuliza zaidi ya kutekeleza ajenda zake za kisiasa za huyo mwanasiasa, kwa kisingizio cha kulinda amani ya nchi.
 
Juzi juzi baada ya CCM kuchagua mgombea wao Zanzibar kulikuwa na maandamano ya kumpokea mitaani na kisha mikutano ya hadhara. Kwa polisi hiyo ni mikusanyiko halali kwa kuwa ni ya chama tawala.

Haileweki toka lini kumpokea ndugu au rafiki ikahitaji kibali cha polisi. Kisingizio kitakuwa ni msiba lakini je shughuli zote zimesimama? Watu hawafanyi kazi? Tubasubiri kuona busara ya polisi kama ipo.
Ni rahisi kutafuta na kuiona dushulele ya jogoo kuliko kuiona busara katika polisi wa Tanzania.
 
Dakika 9 zilizopita,Lissu kaandika hivi kupitia twitter:

Boarding Ethiopian Airlines flight ET 805 from Bole International Airport Addis Ababa to Dar Julius Kambarage Nyerere International Airport now. Tukutane Dar in slightly over three hours-Tundu Lissu on twitter.

Wacha tuone nini kitatokea baada ya muda huo wa masaa 3.
Mmh kwenye ndege kuna network?
 
Anayewapa polisi amri za kuwatendea unyama wanacdm ni kiongozi wa ccm. Kwakuwa Lisu anataka kuja kupambana naye kumtoa madarakani, ni lazima awaagize polisi kumgasi mshindani wake. Hivyo polisi wajue fika kuwa wanatumika na mwanasiasa kutekeleza amri batili, kwa faida yake kisiasa. Ni vyema hao polisi wangetumia hizo nguvu kuwakamata watia nia wa ccm wanaogawa rushwa waziwazi, badala ya kujionyesha wana nguvu kwa kuonea watu wasiovunja sheria yoyote.
 
Back
Top Bottom