msovero
JF-Expert Member
- Jun 30, 2019
- 929
- 1,764
Mwaka jana kuna taarifa zilisambaa kua kuna walimu wa kiswahili wamepangwa kufundisha hesabu,vivyo hivyo hata mwaka huu tutarajie hali hiyo kujirudia. Sababu zinazochangia makosa kama haya ni pamoja na:
Kama serikali ina dhamira ya kweli ya kukabiliana na upungufu mkubwa wa walimu wa masomo ya Sayansi mashuleni, basi ifanyie kazi mapungufu niliyotaja vinginevyo tatizo la uhaba walimu wa sayansi halitaaisha.
N:B kama kuna mapungufu mengine uliyoyaona share hapa yafanyiwe kazi.
- Mfumo ulioandaliwa na TAMISEMI kutokuwa na uwezo wa kutambua masomo (Teaching subjects) ya mwalimu husika; vyeti vyote havina sehemu yoyote iliyoandikwa huyu ni mwalimu wa Fizikia au Kiswahili zaidi ya 'degree program' na kozi alizosoma kwa mihula yote. Hapa TAMISEMI ndo wanapodanganywa, kuna msemo unasema ili upate ajira andika Fizikia na Hesabu, hapa ndo unakuta hata watu waliosoma kiswahili wanajaza kufundisha Fizikia, na masomo mengine ya sayansi. Hapo serikali inakuwa imeamini imeajiri mwalimu wa sayansi kumbe kiuhalisia ni mwalimu wa sanaa. Wengine wanachagua masomo zaidi ya kumi wanaita 'betting'.
- Umakini mdogo wa watendaji wa TAMISEMI; kuna uwezekano mkubwa wa watendaji wa tamisemi kupangia watu ajira pasipo kuangalia vyeti vyao ndio maana hata mtu mwenye cheti kilichoandikwa Bachelor of art with/in education ni rahisi kuajiriwa kama mwalimu wa kwenda kufundiasha Fizikia au Kemia au Biolojia.