Wakuu, kama bado hukuwa na taarifa ya kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi wa Maisha Magic Bongo ndani ya DSTV Barbara Kambogi na msaidizi wake bwana Onesmus Ndarite, tafadhali pitia hapa
This is exclusive! Mkurugenzi wa vipindi wa kitengo cha tamthilia za kiswahili zinazoruka kupitia kisimbuzi cha DSTV mwanamama Mtanzania Barbara Kambogi sambamba na msaidizi wake bwana Onesmus Ndarite yeye akiwa ni Mkenya wamesimamishwa kazi kwa tuhuma nzito za rushwa. Mwanamama huyo na...
www.jamiiforums.com
Leo tutaangazia ripoti iliyotumwa Afrika ya Kusini na mtayarishaji wa filamu nchini bwana Isike Samweli kwa undani.
Tofauti na tuhuma za rushwa zenye ushahidi alizotuma makao makuu ya DSTV Afrika ya Kusini, bwana Isike hakuziacha nyuma tuhuma za mapenzi kugubika katika uongozi wa juu wa DSTV na waandaaji, watayarishaji, wazalishaji na hata waigizaji ili kurahisishiwa kupokelewa na kupewa nafasi kwa kazi zao kuonekana DSTV kupitia kitengo cha tamthilia hizo za Kiswahili.
Bwana Isike alituma ushahidi usio na chembe ya shaka kuhusiana na mahusiano ya kimapenzi baina ya Mkurugenzi msaidizi bwana Onesmus Ndarite na mzalishaji mkuu na mwanzilishi wa kipindi cha vichekesho, Kitimtim bibie Gladness Kifaluka almaarufu Pili.
Mapenzi yaliponoga bwana Onesmus akageuka sehemu ya kipindi hicho, na kwa kutumia mamlaka hayo akawaondosha katika kipindi hicho waigizaji wakuu wawili Dullvani ‘Da Zuu’ pamoja na mpenzi wake katika maigizo hayo Masantula.
Waigizaji hao waliondoshwa kwa amri kutoka kwa bwana Onesmus aliyejitwalia madaraka ndani ya kipindi hicho cha vichekesho baada ya waigizaji hao kuomba waongezewe maslahi kwa kuwa kipindi hicho kilipata kukubalika kati ya watazamaji walio wengi nao umaarufu wao kuongezeka.
Hivi ninavyoandika hapa waigizaji hao wawili sio sehemu tena ya maigizo hayo ya vichekesho na ni kwa wao kuomba stahiki zao za nyongeza katika maslahi.
Kupitia madaraka aliyokuwa nayo ndani ya kitengo hicho cha tamthilia za Kiswahili ndani ya DSTV, bwana Onesmus alitumia nafasi hiyo kukipa muda zaidi kipindi hicho cha mahabuba wake Gladness Kifaluka kuliko ambavyo kilistahili kutokana na ufinyu wa ubora wake.
Mpaka sasa kipindi hicho kingalipo, japo msisimko umepungua baada ya waigizaji hao viongozi kuondoshwa kwa maagizo ya mpenzi wa boss wao bwana Onesmus.
Pichani ni muanzilishi na mzalishaji mkuu wa kipindi cha vichekesho, Kitimtim bibie Gladness Kifaluka.
Video ni muigizaji mkongwe na mtayarishaji nguli wa filamu nchini bwana Deogratius Shija ‘Shija’ akithibitisha tuhuma za rushwa katika tasnia ya maigizo na filamu nchini.
Ni yuleyule ripota kutokea hapa JF, mwenye chanzo chake nyeti…
Tofauti na tuhuma za rushwa zenye ushahidi alizotuma makao makuu ya DSTV Afrika ya Kusini, bwana Isike hakuziacha nyuma tuhuma za mapenzi kugubika katika uongozi wa juu wa DSTV na waandaaji, watayarishaji, wazalishaji na hata waigizaji ili kurahisishiwa kupokelewa na kupewa nafasi kwa kazi zao kuonekana DSTV kupitia kitengo cha tamthilia hizo za Kiswahili.
Dstv wameinunuwa Mnet kupitia kampuni ya mult choice.
Ninachojuwa Mimi Mnet na Dstv vilikuwa ni ving'amuzi vya kampuni tofauti, kwa sasa Mnet ni Channel ndani ya Dstv inayomilikiwa na kampuni ya Mult choice.
Hicho ndicho ninachokumbuka maana na ni issue ya miaka Mingi sana.
Tukilipata la kukunyoosha ni hadi upepo upite, lazima uteseke kwanza.
Ila katika hili kiwanda cha filamu bongo kimeoza.
Baada ya kutoa taarifa hii nimepokea malalamiko mengi kuhusiana na jinsi hali ilivyo mbaya na zaidi Azam TV nao kuangaziwa Wakurugenzi wa huko.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.