Mapya yaibuka sakata la Wakurugenzi DSTV kusimamishwa, mapenzi pia yahusishwa!

Mapya yaibuka sakata la Wakurugenzi DSTV kusimamishwa, mapenzi pia yahusishwa!

Lol...ndio ni subjective, ila unaweza usipende kitu lakini ukajua ni kazi nzuri ya sanaa.

Hiyo Jua Kali nimeiona na bado sana haijafikia kiwango cha kusema eti ni tamithilia kali. Umeshawahi kuona tamthilia kali?

Ikiwa wameshindwa tu kwenye uandishi wa matukio ambao ndio msingi wa hii sanaa ndio utaita kali?

Kumbe watazamaji standard zetu zipo chini ndio maana tunaletewa takataka tuangalie. Lol.
Unaonekana kuwa na ufahamu kuhusiana na masuala ya filamu na script, lakini naona kukubalika kwa tamthilia mbovu kuna mawili…

Standard za watazamaji kuwa chini, hawajui kilicho bora na kawaida.

Kukosekana kwa hizo bora kabisa, watu wanajikuta tu wanapenda hizohizo mbovu maana hawana machaguo mengine.
 
Wakuu, kama bado hukuwa na taarifa ya kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi wa Maisha Magic Bongo ndani ya DSTV Barbara Kambogi na msaidizi wake bwana Onesmus Ndarite, tafadhali pitia hapa

Leo tutaangazia ripoti iliyotumwa Afrika ya Kusini na mtayarishaji wa filamu nchini bwana Isike Samweli kwa undani.

Tofauti na tuhuma za rushwa zenye ushahidi alizotuma makao makuu ya DSTV Afrika ya Kusini, bwana Isike hakuziacha nyuma tuhuma za mapenzi kugubika katika uongozi wa juu wa DSTV na waandaaji, watayarishaji, wazalishaji na hata waigizaji ili kurahisishiwa kupokelewa na kupewa nafasi kwa kazi zao kuonekana DSTV kupitia kitengo cha tamthilia hizo za Kiswahili.

Bwana Isike alituma ushahidi usio na chembe ya shaka kuhusiana na mahusiano ya kimapenzi baina ya Mkurugenzi msaidizi bwana Onesmus Ndarite na mzalishaji mkuu na mwanzilishi wa kipindi cha vichekesho, Kitimtim bibie Gladness Kifaluka almaarufu Pili.

Mapenzi yaliponoga bwana Onesmus akageuka sehemu ya kipindi hicho, na kwa kutumia mamlaka hayo akawaondosha katika kipindi hicho waigizaji wakuu wawili Dullvani ‘Da Zuu’ pamoja na mpenzi wake katika maigizo hayo Masantula.

Waigizaji hao waliondoshwa kwa amri kutoka kwa bwana Onesmus aliyejitwalia madaraka ndani ya kipindi hicho cha vichekesho baada ya waigizaji hao kuomba waongezewe maslahi kwa kuwa kipindi hicho kilipata kukubalika kati ya watazamaji walio wengi nao umaarufu wao kuongezeka.

Hivi ninavyoandika hapa waigizaji hao wawili sio sehemu tena ya maigizo hayo ya vichekesho na ni kwa wao kuomba stahiki zao za nyongeza katika maslahi.

Kupitia madaraka aliyokuwa nayo ndani ya kitengo hicho cha tamthilia za Kiswahili ndani ya DSTV, bwana Onesmus alitumia nafasi hiyo kukipa muda zaidi kipindi hicho cha mahabuba wake Gladness Kifaluka kuliko ambavyo kilistahili kutokana na ufinyu wa ubora wake.

Mpaka sasa kipindi hicho kingalipo, japo msisimko umepungua baada ya waigizaji hao viongozi kuondoshwa kwa maagizo ya mpenzi wa boss wao bwana Onesmus.

Pichani ni muanzilishi na mzalishaji mkuu wa kipindi cha vichekesho, Kitimtim bibie Gladness Kifaluka.

Video ni muigizaji mkongwe na mtayarishaji nguli wa filamu nchini bwana Deogratius Shija ‘Shija’ akithibitisha tuhuma za rushwa katika tasnia ya maigizo na filamu nchini.

Ni yuleyule ripota kutokea hapa JF, mwenye chanzo chake nyeti…

Nifah.

View attachment 2827382
View attachment 2827385
Shikamoo Nifah

Simamia hapo hapo kwenye weledi hadi wanyooke
 
Unaonekana kuwa na ufahamu kuhusiana na masuala ya filamu na script, lakini naona kukubalika kwa tamthilia mbovu kuna mawili…

Standard za watazamaji kuwa chini, hawajui kilicho bora na kawaida.

Kukosekana kwa hizo bora kabisa, watu wanajikuta tu wanapenda hizohizo mbovu maana hawana machaguo mengine.
Umeandika vyema.
Waandaji wanajua hata kama kazi ni mbovu itaangaliwa kwakuwa watazamaji wanapenda vya kwao.

Tutawakosoa tu ili wajirekebishe.
 
ivi tuhuma mpaka zitumwe afrika kusini kwani huyu baraka shelukindo si bosi wa dstv afrika mashariki kwann asiamue izo kesi
Kwamba hujui chain za upigaji bongo mkuu? Huenda huyo Baraka anafahamu vizuri sana hayo.

Isike kwa kulijua hilo akatuma malalamiko yake makao makuu ambako yamezaa matunda.
 
Asante mwaya, nashukuru.

Tatizo nikisema nifanye hivyo mtaniunga mkono kweli kwenye kunipa maokoto? Lols

Na sasa hivi ndio nina maumbea mazito ya kutikisa nchi! Hayo maubuyu hadi dada yetu yule hana.
Tutakuunga mkono ikiwa tu unatuletea na umbea wa viongozi wa serikali wayafanyayo mitaani na bungeni wakiwa na machangu wao
 
Tofauti na tuhuma za rushwa zenye ushahidi alizotuma makao makuu ya DSTV Afrika ya Kusini, bwana Isike hakuziacha nyuma tuhuma za mapenzi kugubika katika uongozi wa juu wa DSTV na waandaaji, watayarishaji, wazalishaji na hata waigizaji ili kurahisishiwa kupokelewa na kupewa nafasi kwa kazi zao kuonekana DSTV kupitia kitengo cha tamthilia hizo za Kiswahili.
Rushwa ni priority number one kwa hapa kwetu
 
Msaada kwenye tuta, kutofautisha DStv, mnet na labda multi choice.....sizipati vizuri tofauti zake
Dstv wameinunuwa Mnet kupitia kampuni ya mult choice.

Ninachojuwa Mimi Mnet na Dstv vilikuwa ni ving'amuzi vya kampuni tofauti, kwa sasa Mnet ni Channel ndani ya Dstv inayomilikiwa na kampuni ya Mult choice.

Hicho ndicho ninachokumbuka maana na ni issue ya miaka Mingi sana.
 
Tukilipata la kukunyoosha ni hadi upepo upite, lazima uteseke kwanza.

Ila katika hili kiwanda cha filamu bongo kimeoza.
Baada ya kutoa taarifa hii nimepokea malalamiko mengi kuhusiana na jinsi hali ilivyo mbaya na zaidi Azam TV nao kuangaziwa Wakurugenzi wa huko.
Nifah hujawahi kuniangusha content imeshiba yaan ukitoa maelezo unaongezwa contents zingine,
 
Back
Top Bottom