MARA: Mbunge wa Serengeti(CHADEMA), Mwl Marwa Ryoba Chacha ajivua uanachama na kujiunga CCM

Hizi zama zitapita na huu ujinga utapita tu.

Hoja ya Zitto kuhusu kile kifungu inazidi kupata nguvu kadri siku zinavyokwenda.

Kamwe hamtakuja kuniona namuunga mkono huyu mtu maana ni sawa na mhujumu uchumi.

Zama za ajabu na ujinga mkubwa.
 
Mungu hatakusamehe yani taifa lipo kwenye maombolezo lakini wewe unaona ni bora utangaze ujinga waka sasa? Yani taifa liingia hasara ya kuwafariji wafiwa hlfu na wewe pia kurudia uchaguzi? Hutasamehewa
 
Kuna kitu wapinzani wanachelewa sana kukitambua. Wanachotakiwa sasa hivi ni kubadili uelekeo wa harakati. Harakati zinazotakiwa kufanywa sasa ni kupigani uwepo wa demokrasia na kuondoa kiini macho kiitwacho demokrasia kilichopo sasa hivi. Hizo ni harakati kama zile za kudai uhuru ingawa tofauti yake ni kuwa serikali ya kikoloni ya wakati hhuo haikuwa katili kama serikali ya ... tuliyonayo sasa hivi
 
Jamani tuache UCHAMA kabisa,
Mtu akiamua kuhama Chama huo ni uamuzi wa Hiari na sio lazima,hakuna haja ya Kulalamika kabisa.
Hilo ni chaguo lake mwenyewe,kwani nyie CHADEMA hamwezi kupata watu wengine wazuri zaidi ya Hawa wanaenda Chama Kingine.
#I LOVE TANZANIA,the better is not enough,best is yet to come#
 
Afu vyuo karibu vinafunguliwa, kama kawaida kutakuwa na vilio vya wanafunzi wa wanyonge kukosa mikopo na kurejea makwao.. Ila za kununulia hawa watumwa wa kisiasa na kurudia chaguzi zipo tele!
 
Huy

Mbunge wa jimbo la Serengeti kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Marwa Ryoba Chacha amejivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) muda mfupi uliopita kwa kile alichodai kuunga mkono juhudi za Mhe. John Pombe Magufuli katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo.

Amesema hajashurutishwa na yeyote kuchukua maamuzi haya.

Marwa amewasihi wana Serengeti kumchagua wanayeona anafaa, anayeunga mkono juhudi za Mhe. Rais Magufuli katika kuleta maendeleo.

Akitangaza kujivua uanachama amesema,

Mimi Marwa Ryoba Chacha, mbunge wa jimbo la Serengeti na mwanachama wa CHADEMA, leo tarehe 27/08/2018 nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushinikizwa na mtu yeyote kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na Chama cha Mapinduzi. Nawaomba wananchi wa Serengeti, mlinipa imani kubwa ya kuwatumikia lakini imefikia sehemu kupitia CHADEMA naona kama siwatendei haki.

Nimeamua nijivue uanachama na kujinga na chama cha mapinduzi ili kuunga mkono juhudi za maendeleo ambazo anazifanya Rais Magufuli. Niwaombe wananchi wa Serengeti, nafasi ipo kwenu chagueni mtu mnayemuona anawafaa kuwawakilisha ambaye ataungana na Rais Magufuli kuwaletea maendeleo.
Asanteni sana.

VIDEO:

​

Huyu mwalimu hamna cha kuunga mkono wa juhudi za Raisi tatizo yeye nimojawapo ya wanasiasa njaaa ambao Wamechukuli ubunge kama Ndo Kazi Yao pekee yakumwingizia kipato sasa inapofika anaangalia upepo anaonakabisa Kuwa 2020 kibarua kinaweza kuota nyasi akiwa kwenye chama chama chake Hivyo anaamua kutafta kibarua upande wa pili, poor kabisa mwali
 
Huyu alijivua ubungetokea mwezi mmoja uliopita na kutangaza leo?

Nadhani itabidi tukubali tu kuwa kila anayejivua ubunge toka chama chochote na kwa sababu yoyote, hiyo ni haki yake na hastahili kulaumiwa.
Na chama anachokihama mbunge, sio wakati wa kukaa chini na kulia. Ni wakati wa kusimama na kujizatiti kama kweli chama hicho kuna wanayoyasimamia kwa dhati ya mioyo yao na si kwa matumbo yao.
 
Mbunge wa jimbo la Serengeti kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Marwa Ryoba Chacha amejivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) muda mfupi uliopita kwa kile alichodai kuunga mkono juhudi za Mhe. John Pombe Magufuli katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo.

Amesema hajashurutishwa na yeyote kuchukua maamuzi haya.

Marwa amewasihi wana Serengeti kumchagua wanayeona anafaa, anayeunga mkono juhudi za Mhe. Rais Magufuli katika kuleta maendeleo.

Akitangaza kujivua uanachama amesema,

Mimi Marwa Ryoba Chacha, mbunge wa jimbo la Serengeti na mwanachama wa CHADEMA, leo tarehe 27/08/2018 nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushinikizwa na mtu yeyote kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na Chama cha Mapinduzi. Nawaomba wananchi wa Serengeti, mlinipa imani kubwa ya kuwatumikia lakini imefikia sehemu kupitia CHADEMA naona kama siwatendei haki.

Nimeamua nijivue uanachama na kujinga na chama cha mapinduzi ili kuunga mkono juhudi za maendeleo ambazo anazifanya Rais Magufuli. Niwaombe wananchi wa Serengeti, nafasi ipo kwenu chagueni mtu mnayemuona anawafaa kuwawakilisha ambaye ataungana na Rais Magufuli kuwaletea maendeleo.
Asanteni sana.

VIDEO:

​
Kumbe gulio la ccm bado linaendelea kwenye mashamba ya CHADEMA!
 
Hivi hakuna sheria inayomtaka mtu anayegombea nafasi ya uongozi wa kupigiwa kura awe mwananchama wa chama hicho kwa muda maalum? Mtu anaingia tu ndani ya chama na hapo hapo anapewa nafasi ya kugombea ubunge?
 
Jamaa kagundua kua hata uchaguzi ukiitishwa Chadema watasusia atapita bila kupingwa.

Tubadili katiba, kama mtu anataka kuhama chama ahame bila kutuingiza kwenye hasara za uchaguzi.

Nchi hii bado masikini, vipaumbele ni vingi sana, pesa iende kwenye mambo ya msingi na sio kila siku ni uchaguzi.

By t way kuna majimbo zaidi ya 150 ya yanayoongozwa na ccm toka 2015, wabunge wake wanaunga mkono CCM since then, sioni tofauti yake ya maisha na majimbo yasiyo ya CCM. Kuunga mkono au kutounga sijaona tofauti.

Tufanye wabunge wote wa upinzani waunge mkono jitihada za rais, je itabadili hali yetu ya maisha na kua mazuri zaidi, Tanzania itaanza kutiririka maziwa na asali? Kwamba kutokuunga mkono ndio kunazuia hayo?

Mwalimu alipambana na matatizo kama ujinga, maradhi, nk lakini hili la ujinga bado ni tatizo. Mtu anasema akiunga mkono analeta maendeleo, mbona maendeleo hayapo kwenye wabunge ambao ni wa ccm toka 2015?
Uncivilised.....Ni fedheha Sana
 
Nilimsikia siku ile kwenye mkutano Wa Magu akisema msinizomee na Mimi naweza kuwa mwanaccm
Kumbe ndo huyu jamaa duhh /alimtuhumu mkurugenzi kuwa mwizi mbele ya Rais kumbe na yeye alikuwa kwenye list ya manunuzi ambapo kila tenda inayotangazwa ya kununua madiwani na wabunge then CCM lazima ishinde tenda hiyo/kweli we are in a right track
 
Mbunge wa jimbo la Serengeti kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Marwa Ryoba Chacha amejivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) muda mfupi uliopita kwa kile alichodai kuunga mkono juhudi za Mhe. John Pombe Magufuli katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo.

Amesema hajashurutishwa na yeyote kuchukua maamuzi haya.

Marwa amewasihi wana Serengeti kumchagua wanayeona anafaa, anayeunga mkono juhudi za Mhe. Rais Magufuli katika kuleta maendeleo.

Akitangaza kujivua uanachama amesema,

Mimi Marwa Ryoba Chacha, mbunge wa jimbo la Serengeti na mwanachama wa CHADEMA, leo tarehe 27/08/2018 nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushinikizwa na mtu yeyote kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na Chama cha Mapinduzi. Nawaomba wananchi wa Serengeti, mlinipa imani kubwa ya kuwatumikia lakini imefikia sehemu kupitia CHADEMA naona kama siwatendei haki.

Nimeamua nijivue uanachama na kujinga na chama cha mapinduzi ili kuunga mkono juhudi za maendeleo ambazo anazifanya Rais Magufuli. Niwaombe wananchi wa Serengeti, nafasi ipo kwenu chagueni mtu mnayemuona anawafaa kuwawakilisha ambaye ataungana na Rais Magufuli kuwaletea maendeleo.
Asanteni sana.

VIDEO:

​

HILI NILISHAONA DALILI LITAJIUNGA, ILIKUWA DHAHIRI TU SIKU ALIPOMCHOMEA MKURUGENZI
 
Naendelea kusisitiza hawa wanaohama wasibezwe, kwanza ni haki yao, pili wanahoja za msingi, na tatu wameona mbali kuwa 2020, hakuna mpinzani atarudi bungeni, hivyo kuliko kusubiri 2020 upotee, wameamua bora wajihakikishie nafasi mapema, na kichocheo cha kuhama ni ile ile rushwa ya ahadi, ukihama, tutakusimamisha wewe.
Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja? - JamiiForums
P.
 
Kuna Yule Dada Wa Nigeria Mercy Chinwo
Aliimba Wimbo Wake Mzuri Sana Unaitwa Access Love
 
Back
Top Bottom