MARA: Mbunge wa Serengeti(CHADEMA), Mwl Marwa Ryoba Chacha ajivua uanachama na kujiunga CCM

MARA: Mbunge wa Serengeti(CHADEMA), Mwl Marwa Ryoba Chacha ajivua uanachama na kujiunga CCM

Nakumbuka siku chache zilizopita,huyu mheshimiwa alimtangaza kwa Rais Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kuwa ni mwizi.
Tukio hilo lilitokea mbele ya wananchi wa wilaya hiyo wakati Rais akiwa ziarahani Mkoani Mara.
Kumbe ulikuwa utani akijua kuwa muda sio mrefu atahama chama.
 
Hawa wakurya sijui wamepatwa na nini, ndio kabila tulikuwa tunaona ni ngamgari, sasa limekuwa kama mlenda

Hawa wajamaa yaanii huwezi amini siku hizi ...mfano hapa mtaani kwetu kuna kijana ni shoga mzuri tu na anahonga wanaume wakati baba na mama yake ni damu ya Utegi Tarime
 
Ooh yule alikua mkurya Wa dar sasa huyu no mkurya original from Mara

Jitafakarini viongozi
 
Nawaonea huruma sana hawa, siasa za CCM hawaziwezi. 2020 hawapati kitu. Time will tell
 
Mama Anne Makinda nilimpenda saana alipokuwa akiendesha Bunge,hasa alipokuwa akimuita Halima Mdee kwa jina lake la kwanza tu bila kuweka Mheshimiwa.Hii ilikuwa ina maana kubwa saana,na alifanya hivyo wakati Mdee anapokuwa mkali kama mbogo bungeni.
Mama Makinda ALLAH akujaalie umri mrefu.
 
huyu aliwaambia wananchi mnanizomea hamjui naweza kuhamia CCM!
 
Viongozi wa chadema.
Tunaomba hao wanaokwenda ccm muwaweke kwenye kitabu cheusi.wasije tena kuomba kurudi chadema.
Huyo anayewadanganya muda wake umebaki mchache sana.
Atapita kama wenzake walivyopita.atakuja mwingine wakiona ugali Hamnaa huko watataka warudi chadema.
Kuweni nao makini.
 
Huu ni upepo utapita tu wanachadema tusivunjike moyo.
 

Mbunge wa jimbo la Serengeti kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Marwa Ryoba Chacha amejivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) muda mfupi uliopita kwa kile alichodai kuunga mkono juhudi za Mhe. John Pombe Magufuli katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo.

Amesema hajashurutishwa na yeyote kuchukua maamuzi haya.

Marwa amewasihi wana Serengeti kumchagua wanayeona anafaa, anayeunga mkono juhudi za Mhe. Rais Magufuli katika kuleta maendeleo.

Akitangaza kujivua uanachama amesema,

Mimi Marwa Ryoba Chacha, mbunge wa jimbo la Serengeti na mwanachama wa CHADEMA, leo tarehe 27/08/2018 nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushinikizwa na mtu yeyote kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na Chama cha Mapinduzi. Nawaomba wananchi wa Serengeti, mlinipa imani kubwa ya kuwatumikia lakini imefikia sehemu kupitia CHADEMA naona kama siwatendei haki.

Nimeamua nijivue uanachama na kujinga na chama cha mapinduzi ili kuunga mkono juhudi za maendeleo ambazo anazifanya Rais Magufuli. Niwaombe wananchi wa Serengeti, nafasi ipo kwenu chagueni mtu mnayemuona anawafaa kuwawakilisha ambaye ataungana na Rais Magufuli kuwaletea maendeleo.
Asanteni sana.


VIDEO:

​
Njaa n a usaliti kama wa yuda kwa yesu
 
Jamaa kagundua kua hata uchaguzi ukiitishwa Chadema watasusia atapita bila kupingwa.

Tubadili katiba, kama mtu anataka kuhama chama ahame bila kutuingiza kwenye hasara za uchaguzi.

Nchi hii bado masikini, vipaumbele ni vingi sana, pesa iende kwenye mambo ya msingi na sio kila siku ni uchaguzi.

By t way kuna majimbo zaidi ya 150 ya yanayoongozwa na ccm toka 2015, wabunge wake wanaunga mkono CCM since then, sioni tofauti yake ya maisha na majimbo yasiyo ya CCM. Kuunga mkono au kutounga sijaona tofauti.

Tufanye wabunge wote wa upinzani waunge mkono jitihada za rais, je itabadili hali yetu ya maisha na kua mazuri zaidi, Tanzania itaanza kutiririka maziwa na asali? Kwamba kutokuunga mkono ndio kunazuia hayo?

Mwalimu alipambana na matatizo kama ujinga, maradhi, nk lakini hili la ujinga bado ni tatizo. Mtu anasema akiunga mkono analeta maendeleo, mbona maendeleo hayapo kwenye wabunge ambao ni wa ccm toka 2015?
Ujinga, ujinga,ujinga. Umeniamsha vyema siku yangu leo natumaini itaenda vizuri. Thank you brother lost id
 
Elimu bure, ujenzi wa SGR, miradi ya ujenzi wa vituo vya afya na uboreshaji wa hospital nchini, miradi ya upatikanaji wa maji kwa wananchi mjiji na vijijini, miradi ya usambazaji umeme Mjini na Vijijini, vita dhidi ya ufisadi, rushwa na dawa za kulevya, usimamizi wa nidhamu na uwajibikaji kwa watendaji na watumishi wa umma, uzalishaji umeme wa gharama nafuu nk

Nidhamu kwa watendaji wa umma ndio hiyo kivuko kupakia zaidi ya watu 200? Huyo mbunge ni kama alichelewa kurudi ccm. Nimeshukuru sana yeye kurudi ccm.
 
Bila shaka Jamaa alisikiliza kwa makini hotuba ya Mh. Rais ya Jana akaamua afuate kile alichosema Kwamba njooni huku tuendeleze gurudumu la maendelezo.Haya kila la kheri huko aendapo
 
Back
Top Bottom