Mara ya mwisho umemtafuta na kuongea na mama yako lini?

Amina mkuu, nikionaga post kama hizi nafikiri if my mummy were alive .
Ningejitahidi kumlipa mazuri yote aliyonifanyia.
Naomba nisimkufuru Mungu wanasema kazi ya mola haina makosa.
 
Haaa sijajua ulikuwa unaishiji na mama yako na sifahamu ulimpoteza mwaka gani.
Mimi mama yangu alifariki mwaka 1994 ila bado sijamsahau kwa kweli
Mwamba 94 na bado unakumbuka ? Unatumia k vant au ulishawai itumia ?

Mimi kasepa 2006 .

Leo sina habari zake .unaijua k vant ?😁
 
Nje ya mada

Mara ya mwisho umempigia baba yako lini?

Kina mama wako overrated kinyama! Kina baba nao wana moyo
Kwanini wanamama wanatritiwa kama special group 😁
Wapuuzi sana hawa watu, alafu maajabu midume ndio inaongoza kuwakandamiza baba zao inasahau nayo itakuwa mababa wa watoto hapo mbeleni ambapo watoto watawatenda kama wao wanavyowatenda baba zao.
Kumsifiasifia mama na kumsahau baba ni upuuzi na ubaguzi mbaya sana, kwanza inatia hofu mwanaume kupiga piga simu kwa mama eti muongee mnaongea nini kila siku kama si umbea?, mwanaume anaemuendekeza mama kila muda hawezi kudumu katika mahusiano maana akili yake inakua imetekwa na wivu wa kike kutoka kwa mama.

Wapendeni wazazi wote, hiyo tabia ya ubaguzi na kujidekeza kwa mama zenu mijitu mizima mnaboa.
 
Mwamba 94 na bado unakumbuka ? Unatumia k vant au ulishawai itumia ?

Mimi kasepa 2006 .

Leo sina habari zake .unaijua k vant ?😁
Nilishatumiaga miaka ya 2010 hadi 2020 kwa sasa ninaiogopa ilikuwa nikinywa asubuhi sikumbuki matukio ya usiku .
Kwa sasa nakunywa bia tu hizi laini windoek na serengeti lite pombe kali nakunywa za nje za ndani konyagi.
Pamoja na yote siwezi kumsahau siwezi kumsahau marehemu mama yangu .
Pamoja na marehemu Baba yangu .
Baba ndiye alikuwa na hela nyingi ,elimu kubwa na cheo kikubwa hela zake tulikuwa tunazipata kupitia kwa mama.
Mama alipofariki msure ndio akawa mpole akawa anatupa hela yeye mwenyewe .
 
Aisee k vant NI shughuli.just image unaweza sahau mzazi lakini kuhisahau pombe inaitwa k vant inakuwa ngumu 😁
 
Huu ni ukweli mtupu
 
Daaaah mimi nimetafuta hata picha yake tu ni mwaka wa 30 sijawahi ipata, naishia kuambiwa tu alikuwa anafanana hivi mara vile.

Endelea kupumzika kwa Amani Mama, msalimie na Baba, na Dada na mdogo wangu huko.
 
AMEEEEEEEEEEEEEEN

POLE SANA MTU WANGU

🕊️✝️🙏🏽
 
Nje ya mada

Mara ya mwisho umempigia baba yako lini?

Kina mama wako overrated kinyama! Kina baba nao wana moyo
Kwanini wanamama wanatritiwa kama special group 😁
Hakika umenena...
 
Nje ya mada

Mara ya mwisho umempigia baba yako lini?

Kina mama wako overrated kinyama! Kina baba nao wana moyo
Kwanini wanamama wanatritiwa kama special group 😁
Juzi nilitoka labour kumchukua mzazi aliyejifungua kwa operation,acha tuu hao wanawake waheshimie.
Ila baba naye apewe stahiki zake
 
Juzi nilitoka labour kumchukua mzazi aliyejifungua kwa operation,acha tuu hao wanawake waheshimie.
Ila baba naye apewe stahiki zake
Ni kweli waheshimiwe,hata hivyo ni nature imeamua wazae...jinsia ya kiume haiwezi kusaidia kuzaa

Lakini haibadilishi ukweli kwamba baba bora pia anatakiwa kukumbukwa
 
Dedication kwa wazazi wetu na waliotangulia basi tuseme

Raha ya milele uwape eeh bwana, na mwanga wa milele uwaangazie, wapumzike kwa amani Amina.

Hakika kibao Chao DDC mlimani park, hakiachi kugonga nyonyo za walio wengi juu ya wazazi

Nawashukuru wazazi wangu wakati wowote,

Ushauri wao umeniletea mafanikio mema,

sasa naishi na watu vizuri eeh, sasa naishi na watu vzr eeh

Huku nilipo wazazi wangu Sina ndugu,

Lakini kutokana na wosia wazazi wangu,

najiona kama nipo babati,

Najiona nipo mang'ola ,
Najiona kama nipo machame,

Najiona kama nipo kibosho,

Najiona kama nipo kahama,

Najiona kama nipo bukoba,

Najiona kama nipo usseri,

Najiona kama nipo mashima,

Najiona kama nipo kilemae,
Najiona nipo tukuyu,

Najiona kama nipo mafinga,

Najiona kama nipo kilolo eeh mama,

cc secretarybird Intelligent businessman Dr am 4 real PhD
 
Kuna huyu Mwamba jana nimemsikia clouds
Hajaonana na Mama yake kwa miaka 35
Ni hapo Kilosa na yeye anaishi Dar
 
Leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…