Mara yako ya kwanza kutongoza/kutongozwa ilikuwaje?

Pengine huyo jamaa uliyekua na bifu nae wala hakua kamla huyo demu,huenda nae alikua anaongopa tu kama wewe,au ilitumika kama silaha ya kukutia maumivu coz washkaji zako walijua ni demu wako tayari,

Uliamini kirahisi sana kua demu kaliwa.
Kumbee? Yawezekana aisee
 
mimi barua yangu ilikamata ikasomwa parade nilichekwa na wanafunz shule nzima wengine walinipa big up ...na huo ukawa mwanzo wa kujiamini,mshipa wa aibu ukatoka

kazi ikaendelea..
🀣🀣🀣
 
Nimecheka kifala. Ulikuwa kama zombie mkuu.
 
Nilimfanya 'demu' apurure maua ya watu, maana alikuwa anachuma jani moja baada ya jingine bila kujua...

Dorah, popote ulipo mama limoyo langu bado latetema kama nimepigwa ngeta
 
2011 nilimwandikia dogo kibarua nikaweka mistari ya kufa mtu.alafu Kuna vipengele nilikuw nakoleza na kalamu nyekundu (utoto bana[emoji3][emoji3]).
Nilimpa mahkaj akampelekea katkat nimeweka noti ya 500 ile noti ya zaman (wakulungwa usikute na mm nlichangia mademu kuomb hela[emoji3][emoji3])

Nmerudi home nakuta wazaz wa Yule dogo wapo sebulen na wazaz wangu barua imewekwa mezan.

Aseeeeee sitoisahau siku ile na sitaki kusimulia yalonikuta ila malipo n hapa hapa dunian Yule Dem sav n single maza Ana watoto wawil kila mtoto Ana baba yake.life limemchakaza haswaaa
 
Dhaaaa sentence ya mwisho
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Haha! Umenikumbusha mbali kweli.

Nilichelewa kuingia katika mitongozo. Muda naanza kutongoza nipo kidato cha tatu.
Demu nilikuww namkubali ila nashindwa kumwambia ingawa naye aligundua hilo.

Na kinokia changu tulikaa namuonesha picha za watu mbalimbali. Kila mtu ninayemuonesha namuuliza unajua huyu. Mtoto anasema anamjua.
Mwishini nikamuonesha maandishi yameandikwa I LOVE YOU. Nikamuuliza unamjua huyu. Mtoto akaamka akitabasmu huku akijificha uso akaondoka.

Sikukata tamaa kidume. Kwa kuwa mimi ni mtunzi wa shairi nikamuandikia shairi moja zuri sana lenye maudhui la kutongoza
Nikalihariri kwenye kompyuta kisha nika-print.

Siku akawa anakuja kuchota maji nyumbani, nilivyogundua kuwa anakuja kubeba ndoo ya mwisho nikatoa karatasi nikaiweka chini ya njia anapopita.
Akaiona akaiokota. Akataka aisome palepale nikamkataza. Akaikunja akaondoka.

Kesho yake akaja nyumbani dukani, muda wa kuondoka nikamfwata nyuma. Nikamuita kwa jina Adikupi, akaitikia akasimama. Nikamuuliza umeisoma ile karatasi. Akajibu akisema "nisije nikamchezea nikamuacha"

Tangu muda huo hadi leo hii mtoto Adikupi ndiye demu wangu wa kwanza na ndiye ex wangu wa kwanza. Popote ulipo binti Adikupi Mungu akupe maisha marefu.
Nimekusamehe kwa sababu utoto wako ndio ulisababisha tuachane. Na kwa hakika ulikuwa ni mtoto wakati ule.

Na najua hadi leo unanihitaji, ila mimi huwa naenda mbele siku zote sirudi nyuma.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] khaaaaah
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…