Mara yangu ya kwanza kukutana na malaika(1987)

Mara yangu ya kwanza kukutana na malaika(1987)

Venus Star

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2018
Posts
26,519
Reaction score
78,311
Za masaa wana JF.

Leo nimeona ni vyema kuwaletea kisa kilichonitokea mwaka 1987 nikiwa kidato cha tano huko Ilboru secondary school. Nilikuwa nikisikia tu habari za malaika kwenye ibada za kidini.

Siku hiyo niliamka usiku kwenda kusoma darasani kama kawaida yangu, yapata saa nane za usiku. Hakukuwa na mtu yeyote darasani bali mimi tu. Wakati naendelea na kubukua ghafla ukatokea mwanga mkali mbele yangu. Ukaniangazia, niliingiwa na hofu na kuanza kutetemeka. Mara nikasikia sauti ya binadamu ikitoka kwenye mwanga ule. Ikiinita jina langu David, David usiogope tazama hapa.

Nilijawa na nguvu na kukaza macho yangu kuutanzama ule mwanga. Ghafla nimuona kiumbe afananae na mwanadamu rangi yake ya silver inayong'aa sana. Mdomo wangu ulikuwa mzito nilishindwa kuongea. Yule kiumbe alinisogelea na kuniambia "Nimekuja kukupa siri ya ulimwengu" Ndipo kiumve hicho kilinigusa kidevu changu, nilihisi kupigwa shot ya umeme. Akaendelea kusema mimi ni malaika, nimekuja kujidhilisha kwako. Ndipo mwili wangu wote ulianza kutetemeka. Alinishika na nikajikuta nipo katika eneo ambalo sijawahi kuliona ni zuri sana.

Akaniambia hapa ndipo huja watu wanapokufa duniani. Alinionesha watu mbalimbali waliokufa, walikuwa pale wakiwa na furaha. Nilimuona mwalimu wangu wa Hisabati kidato cha pili aliyekufa kwa ajali ya gari. Nilimuona akiwa na furaha.

Malaika huyo aliniambia usiogope kuhusu kifo maana ni sehemu ya ukamilisho.

Ni mambo mengi mno niliyapata siku hiyo. Kwa leo naongelea haya tu. Mpaka sasa malaika mbalimbali huwa wanakuja. Nimeshawazoea na tunaongea nao mambo mengi tu.

Nitakuja kuwaeleza namna yetu sisi tulivyofungwa kwenye kifungo cha hapa duniani. Na namna gani ya kuuona ulimwengu wote.

Asante kwa sasa.
Wenu mtiifu D.
 
Tulipoishia.... Nikiwa na malaika kwenye mji wa waliokufa duniani.

Alivyokuwa akiendelea kuongea na mimi, nilipata nguvu ya kuongea. Nikamuuliza... Je, wewe umetoka wapi na jina lako ni nani. Akajibu akisema jina langu huwezi kulitamka utalijua, maana mimi najulikana si kwa jina bali kwa nguvu mimi ndivyo nilivyo, utakavyo nilivyo. Hakika siku ile sikuelewa alikuwa anaongelea nini. Vilevile akanijibu mimi sijatokea popote mimi nilikuwepo nipo na nitakuwepo. Majibu yale yalikuwa magumu sana kwangu yalipita tu.

Akiniita David wewe nimekufunulia leo habari kuu za ulimwengu, ongea na wote wenye kujua na wenye moyo mkunjufu wataelewa na kufuata haya nitakayo kuambia leo hii.

Waambie hakuna mkuu wa dunia zaidi ya mtu mwenyewe. Mtawala wa mtu ni yeye mwenyewe. Waambie wapate kujua kuwa yeye atakaye ufalme wa mwili atapata na atakaye ufalme wa milele atapata. Umeona wale wafu wa dunia, walikuwa wakifanya mambo yao kwa faida ya mwili, hakika nakuambia mwili ni ulimwengu wa macho, katika ulimwengu huo unapitia na kujifunza mengi. Lakini mwisho utafika kwenye uhalisia wako.

Waambie, mambo haya mawili humpata mtu akiwa katika ulimwengu wa macho, yeye huzaliwa na yeye hufa. Waambie hakuna tofauti katika hilo. Anayezaliwa leo hajui utajiri, mali, na vitu vingine kama hivyo. Anapozaliwa hutoa kilio, maana ameingia kwenye sehemu ya maisha mengine.

Mtu hufa ndilo tukio jingine akipotalo. Hilo ni kielelezo cha kuonesha kuwa ulimwengu wa macho si wa kudumu bali ni wa muda. Ni kielelezo cha kufahamu kuwa yote yaliyopo kwenye ulimwengu wa macho ni yakupita. Chuma hupata kutu, kinalika na kuisha, masika huja na kuondoka, maua huonekana mazuri na kisha hunyauka, utawala na ufalme huja na kupita. Haya yote ni kielelezo cha kukukumbusha kuwa kuna jambo unatakiwa ufanye muda ni sasa.

Waambie wenye ufahamu, waambie wenye akili wapate kujua siri za ulimwengu huu. Jambo utalo waambia ni hili, kwenye ulimwengu wa mwili yapo mambo mawili, hayo mambo hayapingani bali yanafanya ukamilisho. Kuna kuzaliwa na kufa, kuna giza na mwanga, kuna kulia na kushoto, kuna juu na chini, kuna hasi na chanya. Yote haya yawe kielelezo kwao wajue kuwa nguvu za giza ndizo hizo hizo ni nguvu za mwanga.

Waambie wajue .......
 
Ninaendelea nilipoishia......

Mwenye ufahamu afahamu haya, na mwenye kuona aone haya. Ulimwengu wawili mambo ni mawili. Utakapo fanya haya mawili kuwa kimoja hakika utaangaziwa.

Kusema kweli malaika alikuwa akiongea na mimi sikujua maana ya hicho alichoniambia. Akanisogelea na kunigusa kinywa na macho yangu. Matakwa yako na hisia zako vikiungana utaangaziwa.

Baba na Mama wakiungana na kufanya kwa pamoja watajenga familia. Mawazo ya Shetani na mawazo ya Mungu yakiungana tutapata amani.

Mshirika kwenye biashara asiwe mtumwa, kutakuwa hakuna kuuwana. Basi mambo haya yawe hekima kwako na uyaelewe.

Uliambiwa kwenye imani yako kuwa Ibrahimu alitoa sadaka ya kuteketezwa. Hiyo ilikuwa ni kuunganisha hisia yake na matakwa. Hisia ipo moyoni matakwa yapo kwenye akili. Basi akili yako na moyo wako vipatane.

Nakusihi uwaambie katika kila jambo linaloogopwa kuna kizuri ndani yake. Moto ukitumiwa tunapata maendeleo, lakini moto huo huo ni hatari sana. Ndivyo hivyo waambie nguvu utakayo ipata utaitumia kwa utashi na si kwamba nguvu hiyo itakufundisha kuitumia.

Mwenye ufahamu ayafahamu haya....
 
Aliendelea kuniambia,

Imani ni hisia, imani ipo moyoni. Basi sasa imani pasipo matakwa, imani pasipo akili haiwezi kufanya chochote.

Vivyo hivyo matakwa, akili pasipo imani haiviwezi kufanya chochote. Basi sasa mwenye imani lazima awe na akili. Na mwenye akili lazima awe na imani.

Kisha malaika akanichukua na kunipeleka sehemu nyingine. Akanionesha eneo kubwa lililojaa viumbe waliofanana na wanadamu. Miiliyao siyo ngozi kama za kwetu, ngozi zao mithili ya chuma. Malaika akaniambia, umeona wale!? Nikasema ndio nimewaona. Hao ni watu kama wewe wapo katika ulimwengu wa mwili mwingine. Wamevaa miili ya chuma maana ulimwengu unaoishi wewe ni tofauti na huu. Hapo wapo katika makutano makuu kwa imani yao wanamwabudu Mungu wao.

Kisha nikamuuliza je, hapo ni wapi!? Sisi tunaweza kufika hapo!?
Akanijibu na kusema hapo ni ulimwengu wa mwili mwingine ili uweze kwenda katika ulimwengu huo wa mwili ni lazima uondoke katika ulimwengu huu wa mwili wako na utaweza kwenda huko. Akaniambia katika ulimwengu wenu wa mwili mnaweza kusafiri kwenda sehemu yoyote ya ulimwengu wenu. Pale mtakapopata na maarifa na kuwa kitu kimoja mtaweza kusafiri katika ulimwengu wote wa mwili. Umesoma kuhusu sayari, umesoma kuhusu nyota ndivyo hivyo mtakuwa na uwezo wa kusafiri kutoka sayari nyingine na kwenda nyingine. Lakini hao unaowaona hawapo katika sehemu ya ulimwengu wenu wa mwili.

Hekima hii mwenye ufahamu aifahamu na mwenye kujua aijue. Ulimwengu wenu upo kwaajili yenu. Ndio maana mnaweza kuuona kwa macho yenu na vifaa vyenu. Lakini ulimwengu mwingine wa mwili hauwezi kuuona kwa macho yenu na vifaa vyenu. Hisia na matakwa yako yatakufanya uweze kuuona ulimwengu mwingine na siyo kuishi ukiwa kwenye mwili huu wa sasa.

Ulimwengu wa mwili upo mwingi tu, kila sehemu yao wanaishi kwa namna yao. Ukiwa katika ulimwengu wa roho utaweza kuuona bali hutaweza kuishi mpaka utakapovishwa mwili wa ulimwengu huo.

Mwenye ufahamu atambue haya....
 
Biblia inawataja malaika kama viumbe wenye muonekano gani?

Kuna ametajwa yeye ni maringi mawili yanayowaka moto.

Kuna mwenye mbawa mia sijui elfu zile.

Basically ni kinyume na hawa manabii wanachotuambia.

Dafuq is this?
 
Biblia inawataja malaika kama viumbe wenye muonekano gani?

Kuna ametajwa yeye ni maringi mawili yanayowaka moto.

Kuna mwenye mbawa mia sijui elfu zile.

Basically ni kinyume na hawa manabii wanachotuambia.

Dafuq is this?

Kwenye bible kuna malaika waliotokea kama watu kawaida...mfano wale walioenda kumtembelea Lutu
 
Yeah walikuwa na muonekano kama bin adam, isipokuwa imeelezwa kwamba walikuwa wanavutia kiasi wakulungwa wa wakati huo wakatamani kuwalala (kuwala kiboga)
Kama biblia ina maelezo haya hizi stori za mabawa, rangi nyeupeeee au silva zinatokea wapi? Kwa sababu biblia imeonyesha pia si kila malaika ana mabawa.

Tumeongopewa for centuries
 
Mwenye ufahamu afahamu haaya....

Kisha malaika akaniambia. Malaika akaniambia, kwa habari ya imani, ni jambo la moyo. Unataka ujue imani yako iendane na akili yako.

Ulimwengu wenu wa mwili mpo na imani zenu, zitumieni hizo imani zenu kujenga umoja ili muweze kuangaziwa. Mkiacha kushindana na kuanza kuaminiana ndipo imani zenu zitakapo zaa matunda.

Mwingine anaamini katika Mungu, mwingine anaamini katika jua, na mwingine anamini katika Miungu wengi. Hakika nakuambia imani ni hisia ni mlango wa kuunganisha mwili na ulimwengu wa roho ili uangaziwe.

Utakapojua kuwa imani ni hisia, utakuwa umeangaziwa. Mwingine imani yake ipo katika majira, mwingine katika mimea na mwingine sehemu tofauti tofuati. Nakusihi uelewe kuwa hayo yote yapo katika moyo ili kujenga hisia na kuzalisha nguvu ya kiroho. Nakuambia hivi leo usingejua kama kuna giza kama mwanga usingekuwepo. Vivyo hivyo mwanga usingekuwa na maana yoyote kama giza halipo. Yapo yanatakiwa kufanyika gizani na mengine yapo yanatakiwa kufanyika kwenye mwanga.

Mwenye ufahamu afahamu haya. Imani yako iunganishe na matakwa. Koleza moto wa imani huku akili yako ikiwa sawa.
 
Back
Top Bottom