I am Groot
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,929
- 10,747
Tupe tu jina la hiyo movie tukaiangalie wenyewe.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sijaja kibiblia mkuu, huo mstari ni maana ya Imani, ni katika kuthibitisha hoja yangu wala sio katika kuanzisha mabishano.Halafu somo la imani haliishii katika tafsiri hiyo moja tu. Imani ni jambo kubwa mno.
Kwa sababu umekuja kwa njia ya biblia. Hebu soma hapa:-
"zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. "
Waefeso 6:16
Tunafundishana sote kwa pamoja. Mwenye hiki anamgawia mwenzake asichokuwa nacho. Na siyo suala la kubishana. Tukifundishana, tufundishane tu si kwa nia mbaya bali kwa nia ya kujengana.Sijaja kibiblia mkuu, huo mstari ni maana ya Imani, ni katika kuthibitisha hoja yangu wala sio katika kuanzisha mabishano.
Hahahaaa nguvu za giza ndo hizo hizo za mwanga maana yake Mungu ana pande mbili upande mwanga na upande giza yaani amekamilika ok sawaTulipoishia.... Nikiwa na malaika kwenye mji wa waliokufa duniani.
Alivyokuwa akiendelea kuongea na mimi, nilipata nguvu ya kuongea. Nikamuuliza... Je, wewe umetoka wapi na jina lako ni nani. Akajibu akisema jina langu huwezi kulitamka utalijua, maana mimi najulikana si kwa jina bali kwa nguvu mimi ndivyo nilivyo, utakavyo nilivyo. Hakika siku ile sikuelewa alikuwa anaongelea nini. Vilevile akanijibu mimi sijatokea popote mimi nilikuwepo nipo na nitakuwepo. Majibu yale yalikuwa magumu sana kwangu yalipita tu.
Akiniita David wewe nimekufunulia leo habari kuu za ulimwengu, ongea na wote wenye kujua na wenye moyo mkunjufu wataelewa na kufuata haya nitakayo kuambia leo hii.
Waambie hakuna mkuu wa dunia zaidi ya mtu mwenyewe. Mtawala wa mtu ni yeye mwenyewe. Waambie wapate kujua kuwa yeye atakaye ufalme wa mwili atapata na atakaye ufalme wa milele atapata. Umeona wale wafu wa dunia, walikuwa wakifanya mambo yao kwa faida ya mwili, hakika nakuambia mwili ni ulimwengu wa macho, katika ulimwengu huo unapitia na kujifunza mengi. Lakini mwisho utafika kwenye uhalisia wako.
Waambie, mambo haya mawili humpata mtu akiwa katika ulimwengu wa macho, yeye huzaliwa na yeye hufa. Waambie hakuna tofauti katika hilo. Anayezaliwa leo hajui utajiri, mali, na vitu vingine kama hivyo. Anapozaliwa hutoa kilio, maana ameingia kwenye sehemu ya maisha mengine.
Mtu hufa ndilo tukio jingine akipotalo. Hilo ni kielelezo cha kuonesha kuwa ulimwengu wa macho si wa kudumu bali ni wa muda. Ni kielelezo cha kufahamu kuwa yote yaliyopo kwenye ulimwengu wa macho ni yakupita. Chuma hupata kutu, kinalika na kuisha, masika huja na kuondoka, maua huonekana mazuri na kisha hunyauka, utawala na ufalme huja na kupita. Haya yote ni kielelezo cha kukukumbusha kuwa kuna jambo unatakiwa ufanye muda ni sasa.
Waambie wenye ufahamu, waambie wenye akili wapate kujua siri za ulimwengu huu. Jambo utalo waambia ni hili, kwenye ulimwengu wa mwili yapo mambo mawili, hayo mambo hayapingani bali yanafanya ukamilisho. Kuna kuzaliwa na kufa, kuna giza na mwanga, kuna kulia na kushoto, kuna juu na chini, kuna hasi na chanya. Yote haya yawe kielelezo kwao wajue kuwa nguvu za giza ndizo hizo hizo ni nguvu za mwanga.
Waambie wajue .......
Ni Uislamu na usitie shaka juu ya hilo..Akitokea siku nyingine mwambie aje kwangu Megamind nina maswali mengi sana.
Kama hatoweza muulize hili swali muhimu, Ipi ni dini ya kweli?
NyumbanBarabarani au angani?
Mkuu acha bangi aka kushabu🤣Za masaa wana JF.
Leo nimeona ni vyema kuwaletea kisa kilichonitokea mwaka 1987 nikiwa kidato cha tano huko Ilboru secondary school. Nilikuwa nikisikia tu habari za malaika kwenye ibada za kidini.
Siku hiyo niliamka usiku kwenda kusoma darasani kama kawaida yangu, yapata saa nane za usiku. Hakukuwa na mtu yeyote darasani bali mimi tu. Wakati naendelea na kubukua ghafla ukatokea mwanga mkali mbele yangu. Ukaniangazia, niliingiwa na hofu na kuanza kutetemeka. Mara nikasikia sauti ya binadamu ikitoka kwenye mwanga ule. Ikiinita jina langu David, David usiogope tazama hapa.
Nilijawa na nguvu na kukaza macho yangu kuutanzama ule mwanga. Ghafla nimuona kiumbe afananae na mwanadamu rangi yake ya silver inayong'aa sana. Mdomo wangu ulikuwa mzito nilishindwa kuongea. Yule kiumbe alinisogelea na kuniambia "Nimekuja kukupa siri ya ulimwengu" Ndipo kiumve hicho kilinigusa kidevu changu, nilihisi kupigwa shot ya umeme. Akaendelea kusema mimi ni malaika, nimekuja kujidhilisha kwako. Ndipo mwili wangu wote ulianza kutetemeka. Alinishika na nikajikuta nipo katika eneo ambalo sijawahi kuliona ni zuri sana.
Akaniambia hapa ndipo huja watu wanapokufa duniani. Alinionesha watu mbalimbali waliokufa, walikuwa pale wakiwa na furaha. Nilimuona mwalimu wangu wa Hisabati kidato cha pili aliyekufa kwa ajali ya gari. Nilimuona akiwa na furaha.
Malaika huyo aliniambia usiogope kuhusu kifo maana ni sehemu ya ukamilisho.
Ni mambo mengi mno niliyapata siku hiyo. Kwa leo naongelea haya tu. Mpaka sasa malaika mbalimbali huwa wanakuja. Nimeshawazoea na tunaongea nao mambo mengi tu.
Nitakuja kuwaeleza namna yetu sisi tulivyofungwa kwenye kifungo cha hapa duniani. Na namna gani ya kuuona ulimwengu wote.
Asante kwa sasa.
Wenu mtiifu D.
Ni imani yako tu. Kama inakupatia faida ni kheri kwako lakini kama imani yako inajenga chuki kwa wengine jaribu kufanya adjustment ya imani hiyo. Usitumie imani tu aka hisia, hebu jaribu kutumia na akili kisogo.Kwa maneno haya tu itoshe kusema ulikuwa unaongea na mashetani.
"Baba na Mama wakiungana na kufanya kwa pamoja watajenga familia. Mawazo ya Shetani na mawazo ya Mungu yakiungana tutapata amani."
Nataka uelewe kuwa umizimu ujibadilisha kulibgana na kipindi na uelewa wa mtu.
Mwambie kwa Jina la BWANA apotee halafu amini
Kwa namna ulivyo taja Yesu. Najua wewe ni mkristo. Hebu nakuomba usome kwenye biblia katika maandiko haya kisha uniletee maana yake:-Ninaweza nisipate nafasi ya kukuona face to face mimi nikutahadharishe kwa wema kabisa kuwa makini mashetani hujigeuza kuwa kama malaika wa nuru.
Swali je utajuaje?
Kipimio ni Neno la Mungu
Ikiwa atatamka maneno ambayo ni kinyume na Neno la Mungu lililoandikwa elewa sio. MKATALIE.
Maana hata Yesu alitokewa na kiumbe kama huyo