Mara yangu ya kwanza kukutana na malaika(1987)

itakuwa na eneo lako wamekupa kabisa ikibidi anza kujenga
 
Za masaa wana JF.

Leo nimeona ni vyema kuwaletea kisa kilichonitokea mwaka 1987 nikiwa kidato cha tano huko Ilboru secondary school. Nilikuwa nikisikia tu habari za malaika kwenye ibada za kidini.

Siku hiyo niliamka usiku kwenda kusoma darasani kama kawaida yangu, yapata saa nane za usiku. Hakukuwa na mtu yeyote darasani bali mimi tu. Wakati naendelea na kubukua ghafla ukatokea mwanga mkali mbele yangu. Ukaniangazia, niliingiwa na hofu na kuanza kutetemeka. Mara nikasikia sauti ya binadamu ikitoka kwenye mwanga ule. Ikiinita jina langu David, David usiogope tazama hapa.

Nilijawa na nguvu na kukaza macho yangu kuutanzama ule mwanga. Ghafla nimuona kiumbe afananae na mwanadamu rangi yake ya silver inayong'aa sana. Mdomo wangu ulikuwa mzito nilishindwa kuongea. Yule kiumbe alinisogelea na kuniambia "Nimekuja kukupa siri ya ulimwengu" Ndipo kiumve hicho kilinigusa kidevu changu, nilihisi kupigwa shot ya umeme. Akaendelea kusema mimi ni malaika, nimekuja kujidhilisha kwako. Ndipo mwili wangu wote ulianza kutetemeka. Alinishika na nikajikuta nipo katika eneo ambalo sijawahi kuliona ni zuri sana.

Akaniambia hapa ndipo huja watu wanapokufa duniani. Alinionesha watu mbalimbali waliokufa, walikuwa pale wakiwa na furaha. Nilimuona mwalimu wangu wa Hisabati kidato cha pili aliyekufa kwa ajali ya gari. Nilimuona akiwa na furaha.

Malaika huyo aliniambia usiogope kuhusu kifo maana ni sehemu ya ukamilisho.

Ni mambo mengi mno niliyapata siku hiyo. Kwa leo naongelea haya tu. Mpaka sasa malaika mbalimbali huwa wanakuja. Nimeshawazoea na tunaongea nao mambo mengi tu.

Nitakuja kuwaeleza namna yetu sisi tulivyofungwa kwenye kifungo cha hapa duniani. Na namna gani ya kuuona ulimwengu wote.

Asante kwa sasa.
Wenu mtiifu D.
Aisee, 1987 nilikua hata tumbon simo.
 
Hapa nadhani unaongea tisa na kenda.
Namna gani utakuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo pasipo hisia!?

Unaongelea jambo lilelile tu. Yaani uhakika wa mambo ya tarajiwayo ni kuhisi kuwa kitu kile unacho wakati huna.

Nakusihi tuliza akili kwanza uupitie uzi huu ukiwa upo open minded. Zaidi sana utakuwa unaongelea hicho hicho nilichokiandika.

Imani ipo moyoni(Nafsi), imani ni hisia.
Nikikutukana ukapata hasira ni hisia kuwa unaamini kile nilichokisema kinautwenza utu wako.

Safi kabisa uliposema hasira ni hisia very good.
We jamaa nimekkubari unaongea vitu vipo very above common human understanding.!
 
Huenda unakaribia pia kufa,sema tu umesahaulika.
Miaka 35 tangu kutokewa na huyo malaika sio haba,omba sana ufike February 2022
 
Kumbe malaika nao wanaonge kama wale watu wa kweny movie ya yesu..
 
Mkuu umezima private messages. Naomba unicheki Whatsapp 0676434611. Kuna Jambo nataka nikushirikishe. Asante
 
Samahanini sana. Kumekuwa na mixed feelings hapa. Nitakuwa nimeanzie mbele zaidi. Labda nianze na vitu simple.
Huyo malaika kwani alikuambia uandike vitu simple?

Kwani walikuambia uwaandikie wasio na mixed feelings?

Kwani Bible imeandikwa vitu simple?

Hii lack of consistency kwako inawafanya watu waone hii ni story ya kutunga na zaidi ni chai!

Tembea na beat uliokuwa unatembea nao kama hv: ..... mwenye ufahamu na asikie...

Full stop!
 
[emoji817]
 
Za masaa wana JF.

Leo nimeona ni vyema kuwaletea kisa kilichonitokea mwaka 1987 nikiwa kidato cha tano huko Ilboru secondary school. Nilikuwa nikisikia tu habari za malaika kwenye ibada za kidini.

Siku hiyo niliamka usiku kwenda kusoma darasani kama kawaida yangu, yapata saa nane za usiku. Hakukuwa na mtu yeyote darasani bali mimi tu. Wakati naendelea na kubukua ghafla ukatokea mwanga mkali mbele yangu. Ukaniangazia, niliingiwa na hofu na kuanza kutetemeka. Mara nikasikia sauti ya binadamu ikitoka kwenye mwanga ule. Ikiinita jina langu David, David usiogope tazama hapa.

Nilijawa na nguvu na kukaza macho yangu kuutanzama ule mwanga. Ghafla nimuona kiumbe afananae na mwanadamu rangi yake ya silver inayong'aa sana. Mdomo wangu ulikuwa mzito nilishindwa kuongea. Yule kiumbe alinisogelea na kuniambia "Nimekuja kukupa siri ya ulimwengu" Ndipo kiumve hicho kilinigusa kidevu changu, nilihisi kupigwa shot ya umeme. Akaendelea kusema mimi ni malaika, nimekuja kujidhilisha kwako. Ndipo mwili wangu wote ulianza kutetemeka. Alinishika na nikajikuta nipo katika eneo ambalo sijawahi kuliona ni zuri sana.

Akaniambia hapa ndipo huja watu wanapokufa duniani. Alinionesha watu mbalimbali waliokufa, walikuwa pale wakiwa na furaha. Nilimuona mwalimu wangu wa Hisabati kidato cha pili aliyekufa kwa ajali ya gari. Nilimuona akiwa na furaha.

Malaika huyo aliniambia usiogope kuhusu kifo maana ni sehemu ya ukamilisho.

Ni mambo mengi mno niliyapata siku hiyo. Kwa leo naongelea haya tu. Mpaka sasa malaika mbalimbali huwa wanakuja. Nimeshawazoea na tunaongea nao mambo mengi tu.

Nitakuja kuwaeleza namna yetu sisi tulivyofungwa kwenye kifungo cha hapa duniani. Na namna gani ya kuuona ulimwengu wote.

Asante kwa sasa.
Wenu mtiifu D.
Mpaka hapo story yako inapingana na biblia hivyo ni dhahiri hao ni Malika wa giza wanajaribu kukutumia kukutoa ktk njia na kuongoza kuwatoa wengine ktk misingi ya kweli za biblia.
Cha kufanya washirikishe wengine wakusaidie mfunge pamoja kukemea na kuomba neema ya Mungu na roho hao wachafu watakoma kukufuata
 
Vijana vuteni bangi original! Kushabu zinaharibu akili
Mzee mbona mmengangana bangi bangi..wew unakiamin ulichofundishwa kanisan au msikitini..what if si kwel...so watu wakija na bahar nyingne why usisome na kutulia uka judge mwenyew..unabak kusema bang bang...hii dunia ina watu 8bil...wakristu ni 20 % waisilamu sijui ..inamana hao wengne woote ni wajinga na iman wanazoamin...so ikiletwa hoja usikimbilie tu kusema bangi bangi....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom