Marafiki hawadumu wanakuja na kuondoka, tuliowahi kuwa mabesti nao leo tunaishia kuchunguliana status hata "hi" hakuna

Ni message ya kikatili sana hii, ni basi tu utakuwa strong ukiwa nje lakini ndani ya moyo kumejaa maumivu, ni vitu vinavyochukua muda mrefu kupona ila vinaacha makovu ya milele
Hakika hata nikijaribu kurudisha moyo nyuma nashindwa, Kuna siku alinitafuta akawa anaongea as if hakuna kiliwahi kutokea ila nikasema hapana, wema unintended lkn hii kauli haitotoka milele kwenye moyo
 
Umenena mkuu, rafiki yangu mkubwa ni Mimi yaani najipenda mwenyewe then wanafamilia.
 
Ni kweli kabisa ,hapo ndio utajua nafasi ya familia yako na ndugu...Wale mliokuwa sehemu moja labda kazi au masomoni kila mtu ana maisha yake mkiachana kidogo tu.
Cha kusikitisha ni kwamba hata asilimia kubwa ya ndugu leo hii ni masnitch tu, thamani Yako Kwa ndugu itaonekana kama uko njema kiuchumi, ukiwa lofa hakuna anaekujali..familia yako ndo kila kitu.
 
Marafiki wengi wapo kimasilahi tu ,wakishapata wanachokitafuta wanatafuta marafiki wa level zao na kusahau waliosota bao.

Mimi nina jamaa angu tulikuwa karibu sana ,alipopata kitengo fulani ndio mwisho wa kupokea simu hadi leo

Na wengi sana nimekutana na hayo

#mimi watu kama hao nafuta namba zao , siku tukikutana wakiniomba namba nawapa ya zamani ambayo haipo hewani


Mwingine mkikutana anakuuliza sikuhizi unafanya kazi gani ,badala ya kujuliana hali .


Jino kwa jino
 
Hilo swali la unafanya kazi gani hakika ni swali la kimbea sana,
 
Familia ndiyo rafiki wa kweli.
Marafiki wengi wanaachana pale mmoja anapopiga gepu fulani.
Asap Rock vs Asap Rillei ni case ya kweli kabisaa jamaa anamuonea wivu mshkaji waliosotabtangu utotoni kisa yeye katoboa kwa kumpata Rihanna. Ukitaka kujua watu ni washenzi ukitoboa ndo watakutafuta.
Kingine ni ndoa ukioa wanawake wanajaribu kila njia kukuweka mbali na marafiki zako
 
Yan na namba ya simu nimebadili rasmi jana. Za zaman nimeziacha watsap kwa muda ila nitaziondoa hata huko watsap

Nina kautaratibu kangu hivi , nafikiri ni kazuri tu, anayenikacha huwa sina muda wa kumbembeleza arudi, hata kama nipo maji ya shingo.

Na nikiamua kwenda mbele huwa sirudi nyuma.
Huwa sibadili namba labda wao ndo wabadili… Wakinitafuta nawakaushia.
 
Mimi Kuna marafiki tulikua pamoja na tulishirikiana Sana katika kupeana updates Za nafasi za kazi

Na tulitembea Sana kwenye mikoa tofauti ili mradi tupate check namba

Balaa lilianza baada ya wachache wao kupata ajira mawasiliano yalipungua na mwisho wa siku ukituma message unaulizwa Nani mwenzangu

Basi na Mimi nilikubaliana Na Hali japo baadhi yao niliwasaidia ata kipesa pindi walipokwama
Nashukuru Na Mimi nilikuja kupata kazi maisha mengine yanaendelea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…