Marafiki hawadumu wanakuja na kuondoka, tuliowahi kuwa mabesti nao leo tunaishia kuchunguliana status hata "hi" hakuna

Urafiki una kanuni na mvuto wake.
Urafiki unaweza kutengenezwa na;
1. Mazingira yanayofanana..eg mko darasa au shule au chuo kimoja...nje ya hapo urafiki unajifia kifo cha kawaida.

2. Urafiki unaweza kutengenezwa kwa kazi au biashara inayofanana ukifilisika ..urafiki ndio umegota.

Kuna urafiki usio na sababu yaani mmejikuta tu mna urafiki huu mara nyingi hudumu.

Asante sana rafiki yangu mwema...(mwana jf) sijawahi kujuta wewe kuwa rafiki yangu.
 
Huyo jamaa wa mwisho wa ulinzi hautakiwi kuwa karibu naye kabisa kwa namna yeyote ile,maana ni mtu anajali Mali kuliko utu.
Mtu sahihi,hawezi kataa salamu,pongezi Wala ushauri,kwa namna yeyote ile
mwisho saikolojia inasema:-If your are not loosing friends you can't grow
 
Naona ulivyokuwa unahangaika kumfukuzia classmate wako mwenda Kwa miguu ktk jitihada za kutaka kumdhihirishia kuwa umetoboa, hata pale ambapo hakuwa tayari kuonana na wewe! hii ni aina flani ya ulimbukeni, mafanikio Yako ni Yako, and you don't need to seek recognition to anyone..!
 
Marafiki zangu wanasema nawakaushia eti kisa nimetoboa kumbe kwangu ngoma ngumu na hakuna anaeamini

Napiga kazi masaa 22 muda wa kupiga story sina labda chatting ukimcheki mshikaji hakujibu kana kwamba analipiza

Nina madeni kibao japo sio ya marafiki mshikaji akinicheki nikimwambia sina kitu haamini na kusambaza sifa mbaya eti mimi mbahili

Napenda maendeleo ya kuonekana hasa ujenzi wa nyumba na ununuzi wa viwanja hilo ni kosa kubwa maana mashikaj wanajua nafanya vitu vikubwa ila wakitaka msaada sina na kweli sina kwa anaejua ujenzi wa kudunduliza sio mgeni na hili

Mchakato ni pale ninapokuwa na shida hakuna anaekuelewa hata ma business mate wangu aiseeh

Jinsi unavyozidi kukua neno rafiki linazidi kufutika kabisaa
 
You will never lost fighting for your family:-
1.ukipigania mtoto wako amjue mungu,utapunguza majambazi,makahaba,wadangaji,matapeli,mafisadi etc
2.Mabadiliko ya kweli huanzia kwenye familia yako
3.Ukiifundisha vizuri familia yako:hawatakuja kuwa masimp wa kutokujua kwamba urafiki hutegemea na eneo Fulani,ila uthubutu,ukweli,uadilifu,roho nzuri, hivi vitu hudumu maisha yote
Kwa shuhuda hizi inaonesha Bora upambanie familia Yako tu.
 
Hayo ya kawaida Sana mkuu Kuna jamaa yangu tumesoma na kukua nae pamoja aliingia vikosini kitambo sofar senior mabegani nilikuwa nikimjulia hali mara kibao kishkaji no response sasa akawa anakwepa simu zangu labda alihisi nampigia mikuki na hata whatsap blue tick 2 hajibu siku ya siku kanikuta mahali ambapo hakuamini baadae anatuma sms kuwa "ndg yangu kumbe upo hapo bwana basi tuwe tnawasilana wewe ni mtu muhimu" utaratibu wangu ni kwamba Sasa kila mtu akale alipolima nimekata net nae kumbe urafiki wa kinafiki kibarua changu ndo kifanye urafiki? No na sms yake sikumjibu mwaka unakaribia
 
Pole sana,kama mwanadamu yeyote Ile inumiza sana kumpoteza mtu uliyemuamini,lakini nikufundishe kitu kimoja.
Saikolojia inasema when you are genuine,real and pure,you will never loose people,they will loose you
Yaani mfano unapata ridhiki halali unasaidia mayatima,wasiojiweza,unatoa,misaada,unajenga magorofa ya watoto yatima,unasaidia watu kupata kazi,elimu,etc........hautokuja kuishi kwa upweke na hata watu waliofanikiwa wakiondoka hautaumia,.
Maumivu hutokea kama unategema returns
 
Huyo ego inamtesa na ego is real enemy--------Anguko lake linakuja ama linakaribia
Mtu yeyote anayetaka ufanye vizuri hata kama anakutuhumu kitu cha uongo,akidhani kua unachofanya sio sahihi,huyo sio adui
1.Unapowapima watu wea.ama wabaya,wapime Kwa intensions zao,na si matendo yao,......mtu mbaya anaweza kukupa hela ili ulewe/utumie madawa ya kulevya
 
Rafiki wa kweli ni familia yako tu.
Hapana hata familia yako,inawesa kukugeuka,unifahamu KESI ya bilionea msuya,unaifahamu KESI ya bilionea Davis Mosha,.......kwa umri uliofikia haujawahi ona watoto,make,mume wanaikimbia familia?
rafiki kwa kweli,ni:-
1.Ile dhamira Yako ya kutaka watu wafanikiwe,yaani urafiki ni Hali na sio mtu.
2.wewe muajiri,manager,boss,
Kitendo Cha kutaka kampuni/ofisi Yako,iwe na output kubwa huku wafanyakazi wakinufaika ,hapo tayari utakua na marafiki wengi mno
3.Upo mtaani unawasidia wasiojiweza,wajane unawasapoti kuwasomeshea watoto wao,hata siku ukiumwa huna damu,rundo la watu litakuja kukutolea damu.
4.Ila una watoto wanna wanasoma IST,FEZA etc........unawafundisha kula mapizza,uchoyo,ulevi uzinzi etc.....siku ukiumwa watatokea club kuja kukuona na hata mmoja hatakua na sifa ya kukutolea damu,maana wote watakua miili Yao imejaa tattoos
 
Huwezi kua unatafuta pesa,unapata riziki na hauna bajeti ya kuwasaidia wenzako,review Tena hustle zako
 
Kama ilivyo muhimu kwa Ndugu, kwenye maisha ya mtu ndivyo ilivyo muhimu kwa Rafiki/Marafiki.

Tatizo wengi wetu tumejikita kubomoa Urafiki kuliko kuujenga linapotea tukio tusilo tarajia. Fikiri Urafiki ulijengeka kwa machozi, jasho na damu, Unakufa, sababu tu ya Event fulani.

Life has Ups and Downs, kulitambua hili ni muhimu sana. Fikiri Urafiki umeruhusu Uvunjike mara ngapi, sababu tu Umeona tukio moja, na kusahau mengi mema yaliyotengeneza huo Urafiki.

Btw happiness from friends is not permanent,hata hao Marafiki wazuri uliowapata sasa, yawezekana ipo siku wakakuumiza tu.
 
Kabisa ukioa si mke anakuweka mbali na marafiki na ndugu zako.
 
Huwezi kua unatafuta pesa,unapata riziki na hauna bajeti ya kuwasaidia wenzako,review Tena hustle zako
Yap nakubali vimisaada vya hapa na pale muhimu na huwa sibanii izo mishe za kuwaungia mashkaj

Inshu ni pale wengi wanaona kama nimetusua wakati kwangu ni apeche alolo mtu anakuomba umewezeshe kitu kikubwa kulingana na anavyokuona while behind the scenes ni msoto mkali
 
Kama unafanya hivo,inatosha.......wapo watakaokuombea maisha yako yote,huwezi mridhisha kila mtu
 
Kama unafanya hivo,inatosha.......wapo watakaokuombea maisha yako yote,huwezi mridhisha kila mtu
Pamoja mkuu rafiki ni zaidi ya ndugu hasa pale mtakapokuwa na level sawa za kimaendeleo na fikra
 
Usitengeneze marafiki bali tengeneza jamaa.Ukiwa na rafiki ukiisha ama kuvunjika utaumia sana kwakuwa rafiki anajua mambo yako mengi na siri zako pia.
Jamaa ni yule unakuwa naye karibu kwa nia ya kushirikiana shughuli za kimaendeleo ama kijamii.
Jamaa unawatengeneza kulingana na umri wako ama kiwango chako cha kiuchumi.
 
Ni kweli kabisa ,hapo ndio utajua nafasi ya familia yako na ndugu...Wale mliokuwa sehemu moja labda kazi au masomoni kila mtu ana maisha yake mkiachana kidogo tu.
even within families, hasa kama baba aliwakusanya kutoka mama tofauti, lakin mkakua pamoja, wengine wakitoboa, kukawa na economic gap, nyie si ndugu tena, labada mtaunganishwa na MISIBA, HARUSI na MATAMBIKO (kwa wanao practice hizo rituals)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…