Marafiki wa kweli ni wa utotoni

Marafiki wa kweli ni wa utotoni

Mimi sina bahati ya Marafiki [emoji24]
Sina Rafiki wa Utotoni wala wa Ukubwani,
Hua natamani sana nikiona Marafiki wameshibana, wanataniana, wanasaidiana, wanaambatana sehemu pamoja, hata nikiangalia movies inayoonesha marafiki fulani wamepambana pamoja hua nawish na mimi ningempata Mtu/Watu wa namna hiyo,

What is wrong with me [emoji24][emoji24][emoji24]
You broke my heart kwa hii comment,🥲
We talked about it and i'm trying my best, i thought..... anyway i'm calling you now pick it up
 
Usiumizwe sana na marafiki wa ukubwani
Usiwaamini sana marafiki wa ukubwani
Wachache sana huwa wakweli na wasio na agenda kificho
Marafiki wa kukutana high school
Marafiki wa kukutana vyuoni
Marafiki wa kukutana makazini
Marafiki wa kukutana ukubwani kwenye biashara, uchumba nknk.. Si marafiki halisi bali ni marafiki kwa sababu fulani

Hawa ni mpaka mkae muda mrefu sana pamoja kwenye hali zote shida na raha, kukosa na kupata, kuumia na kuumizwa! Wengi wao rangi zao halisi hujifunua huku!

Rafiki uliyekua naye mkasoma wote shule ya msingi, mkacheza pamoja, mkachunga pamoja,mkalima pamoja mkatembeleana, mkacheka pamoja mkalia pamoja, familia zenu zinafahamiana ndugu zenu wanafahamiana.. Hawa ndio huwa marafiki wa kweli kwakuwa bond wanayoijenga huwa na vyanzo vingi.. Hawadahauliani na ni vigumu mno kusalitiana!

Tunakutana na watu wapya kila siku, wema na wabaya! Na wabaya waliojificha kwenye joho la wema! Sio dhambi kuwa na marafiki wapya! Maisha ni watu bila watu hakuna maisha ama maisha yanakuwa hayana maana!

Rai tangu ni hii kuwa makini sana unapochagua marafiki wa ukubwani.. Wengi ni marafiki wa agenda.. Wengi ni marafiki kwa sababu . Agenda ikiisha/ikifa ama sababu ikikoma na urafiki nao hufika tamati

Ninao marafiki wengi na ninawaamini sana ila baadhi wameniachia makovu .. Siumii kwakuwa natambua marafiki wa kweli ni wale wa utotoni[emoji2827]View attachment 2519891
Nilikua na rafiki moja wa utotoni nilio muamini na akaniamini, ila bahati mbaya nilivo rudi nchini nili ambiwa amefariki Iliniuma kweli kweli mpaka sasa sina rafiki hata moja, inauma sana kukosa mtu wakuamini, hu ni mwaka wa tano natafuta rafiki wa dhati lakini wapi loh!
 
Mimi sina bahati ya Marafiki [emoji24]
Sina Rafiki wa Utotoni wala wa Ukubwani,
Hua natamani sana nikiona Marafiki wameshibana, wanataniana, wanasaidiana, wanaambatana sehemu pamoja, hata nikiangalia movies inayoonesha marafiki fulani wamepambana pamoja hua nawish na mimi ningempata Mtu/Watu wa namna hiyo,

What is wrong with me [emoji24][emoji24][emoji24]
We kama mimi tu ...nothing is wrong tuendelee tu kusukuma gurudumu la maisha.
 
Usiumizwe sana na marafiki wa ukubwani
Usiwaamini sana marafiki wa ukubwani
Wachache sana huwa wakweli na wasio na agenda kificho
Marafiki wa kukutana high school
Marafiki wa kukutana vyuoni
Marafiki wa kukutana makazini
Marafiki wa kukutana ukubwani kwenye biashara, uchumba nknk.. Si marafiki halisi bali ni marafiki kwa sababu fulani

Hawa ni mpaka mkae muda mrefu sana pamoja kwenye hali zote shida na raha, kukosa na kupata, kuumia na kuumizwa! Wengi wao rangi zao halisi hujifunua huku!

Rafiki uliyekua naye mkasoma wote shule ya msingi, mkacheza pamoja, mkachunga pamoja,mkalima pamoja mkatembeleana, mkacheka pamoja mkalia pamoja, familia zenu zinafahamiana ndugu zenu wanafahamiana.. Hawa ndio huwa marafiki wa kweli kwakuwa bond wanayoijenga huwa na vyanzo vingi.. Hawadahauliani na ni vigumu mno kusalitiana!

Tunakutana na watu wapya kila siku, wema na wabaya! Na wabaya waliojificha kwenye joho la wema! Sio dhambi kuwa na marafiki wapya! Maisha ni watu bila watu hakuna maisha ama maisha yanakuwa hayana maana!

Rai tangu ni hii kuwa makini sana unapochagua marafiki wa ukubwani.. Wengi ni marafiki wa agenda.. Wengi ni marafiki kwa sababu . Agenda ikiisha/ikifa ama sababu ikikoma na urafiki nao hufika tamati

Ninao marafiki wengi na ninawaamini sana ila baadhi wameniachia makovu .. Siumii kwakuwa natambua marafiki wa kweli ni wale wa utotoni[emoji2827]View attachment 2519891
Daaaah!umenikumbusha mwanangu sana raymond benedict enzii hizoo skuli ya nursery loooh!tunapitia ndani ya fenc y nyumba ya mapadri pori t pori kama maofficers wa tanapa hahahahahaha
Screenshot_2022-12-27-11-36-03-16~2.jpg
 
Unataka kusema wenye tabia mbovu hawana marafiki?
Mimi nawaona Walevi na Wazinzi kila siku wameshibana na kusaidiana halafu wataka kusemaje,

Kila Mtu huambatana na wa kuendana nae.

Urafiki hua unakujaga automatically na haunaga maslahi,ubinafsi,wivu….., ikishaingia maslahi tuu urafiki ushaharibika. Maslahi yakiisha urafiki hufa….

Unaweza kuta wenye tabia mbovu wana marafiki wenye tabia nzuri, walevi wana marafiki sio walevi.
 
Uncle huu uzi, umegusa uhalisia, binafsi kuna marafiki hata niende nchi gani i never stop kuwasiliana nao na hata ipite miezi tunapowasiliana ni kama mnawasiliana kila siku, wengi ni wale wa primary school.

Urafiki huu hamnaga maslahi,hamnaga wivu, mnakosoana kirahisi kwa utani, mnapeana tafu bila kuuliza, ni rahisi kumsoma mwenzio kwenye hali zote.

Hawa ndio hata ukute wakibadilika na tabia za ukubwani mfano, mteja, mlevi, malaya kumtenga inakuwa ngumu…
 
Back
Top Bottom